Madhara ya Mafuta ya kupikia
Tafiti zinaonyesha Idadi ya Watu wanene kupindukia Imeongezeka hivi karibuni, Je,Mafuta ya Kupikia nayo ni chanzo? Soma hapa kufahamu...!!!!
Idadi ya watu wanaosumbuliwa na tatizo la unene imeongezeka Sana katika miaka ya hivi karibuni,si katika nchi zilizoendelea pekee bali hata za kipato cha Chini."
Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani, watu wapatao bilioni 2.5 duniani kote walikuwa na tatizo la uzito mkubwa au Uzito kupita kiasi mnamo mwaka 2022.
Lakini pia Unene wa kupindukia miongoni mwa watoto umeongezeka mara nne.
Unene umekuwa tatizo linalotia wasiwasi si miongoni mwa watoto tu bali pia miongoni mwa watu wazima.
Mafuta yakupikia yana Athari gani mwilini?
Mtindo mbaya wa Maisha ikiwemo Ulaji mbaya unatajwa kuwa sababu kuu za kunenepa kupita kiasi.
Hata hivyo, mara nyingi watu hupuuza ukweli kwamba mafuta tunayoongeza kwenye mlo wetu kila siku huchangia tatizo hilo.
Mafuta ya kupikia hutumiwa kufanya chakula chochote kiwe kitamu zaidi.
Kutokana na hili, miili yetu hukusanya mafuta, Na Kwa kuwa hatufanyi mazoezi mengi, mafuta mwilini hayayeyuki."
Pia Asilimia kubwa ya Watu hula Mlo wenye wanga nyingi sana, Wanga huu hubadilika na kuwa mafuta baada ya kuingia mwilini,
Zaidi ya hayo, mafuta pia hujilimbikiza katika miili yetu. Hii huongeza hatari ya unene kupita kiasi."
"Kiwango cha mafuta ya miili yetu huwa juu kila wakati.
Hata kama mtu ni mwembamba, mafuta ya mwili wake bado ni 30-40%, ambayo ni ya juu sana. Kwa upande mwingine, wanariadha wana 7-8% ya mafuta ya mwili."
"Ikiwa tuna mafuta mengi katika miili yetu, Matokeo yake ni uzito wa mwili kuongezeka Zaidi"
"Kutumia mafuta ya kula kuliko kiasi kinachopendekezwa kunapunguza kasi ya ufanyajikazi wa miili yetu,Hii inasababisha kuongezeka kwa mafuta ya mwili na uzito.
Zaidi ya hayo, hutupatia kalori za ziada badala ya kutupa nyuzinyuzi, vitamini muhimu na madini."
Miili yetu hupata kalori zake nyingi kutoka kwenye mafuta,Kwa kila kalori nne tunazopata kutoka kwenye protini, tunapata kalori tisa kutoka kwenye mafuta.
Kwa hivyo, chochote tunachokula na kalori nyingi kinaweza kusababisha kunenepa, hasa kwa watu ambao tayari ni wanene."
Unapaswa kutumia mafuta kiasi gani?
Unene unaweza kudhibitiwa kwa kutumia mafuta kidogo,Kadiri watu wanavyotumia mafuta mengi, kiasi cha mafuta mwilini huongezeka.
Dk. Mahendra Narwaria, rais wa All India Society for Advanced Study and Obesity, anasema, "Chakula cha Wahindi kina wanga na mafuta mengi
Dk. Parmeet Kaur alisema, "Mafuta hutusaidia kuyeyusha vitamini kama vile A, D, E, na K katika miili yetu.
Kwa hiyo, miili yetu inahitaji kiasi fulani cha mafuta."
Pia anasema, "Watu wanapaswa kutumia mafuta kulingana na umri wao.
Hata hivyo, mtu ambaye hana shughuli nzito anapaswa kutumia vijiko 4-5 tu vya mafuta kwa siku.
Hiyo ni, gramu 20-25 za mafuta kwa siku.
Hii ni nyingi kwa mtu mmoja."
Hata hivyo, mafuta sio sababu pekee ya uzito kuwa mkubwa.
Credits Also to:BBC
WEKA COMMENT HAPA..!!!
image quote pre code