Mwanaume achanjwa mara 217 dhidi ya Uviko ndani ya miezi 29.
Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 62 kutoka Magdeburg, Ujerumani, “kwa makusudi na kwa sababu za kibinafsi“ alichanjwa mara 217 dhidi ya Uviko ndani ya miezi 29.
Ushahidi ulikusanywa na mwendesha mashitaka wa Magdeburg, aliyeanzisha uchunguzi wa madai ya ulaghai lakini hakufungua mashitaka ya jinai.
Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Erlangen-Nuremberg wamemfanyia vipimo mbalimbali mwanamume huyo kuchunguza madhara ya kinga ya mwili.
Mwanamume huyo “hakuripoti madhara yoyote yanayohusiana na chanjo,” waliandika katika jarida la sanyansi la Lancet.
Hakukuwa na dalili kwamba amewahi kuambukizwa Covid, hata hivyo.
>>Soma Zaidi kuhusu; Ugonjwa wa COVID-19
Uganda kuharibu chanjo za Uviko-19 zenye thamani ya dola milioni 7.4.
Uganda itaharibu chanjo za Uviko-19 zenye thamani ya dola milioni 7.4 zilizoisha muda wake, kufuatia kupugua kwa mahitaji ya chanjo hizo, huku dozi zaidi za chanjo hiyo zikitarajiwa kuisha muda wake kufikia mwishoni mwa mwaka.
Taifa hilo lilitumia fedha za mkopo kutoka Benki ya Dunia kuagiza chanjo hizo, na karibu nusu ya dozi milioni 12.6 zimeisha muda wake
COVID-19: Maambukizi yaongezeka kwa asilimia 52 katika mwezi mmoja, yasema WHO.
Shirika la Afya Duniani, WHO, jana limethibitisha idadi ya wagonjwa wa COVID-19 duniani kote inaongezeka kwa kasi na kwamba “tutarajie idadi kubwa zaidi ya wagonjwa katika miezi ijayo ya msimu wa baridi kali kwenye maeneo ya kaskazini mwa dunia.”
Takwimu za hivi karibuni kutoka WHO zikijikita katika wiki nne za kuanzia mwezi Novemba hadi Desemba 17 mwaka 2023 zinaonesha ongezeko la asilimia 52 ya idadi ya wagonjwa ikilinganishwa na siku 28 zilizotangulia.
Msemaji wa WHO Christian Lindmeier, amewajulisha waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi hii jana kuwa ongezeko hilo ni sawa na wagonjwa wapya 850,000, lakini takwimu kamili zinaweza kuwa za juu.
“Unafahamu kuwa duniani kote na umeshuhudia hata wengi wenu kwenye nchi zetu kwamba utoaji wa taarifa umepungua, vituo vya ufuatiliaji navyo vivyo hivyo, kwingine vimevunjwa kabisa au vimefungwa… kwa hiyo hii bila shaka inatupeleka kwenye kukosa picha halisi na tunatarajia kwa bahati mbaya idadi kubwa zaidi ya wagonjwa kuliko tulivyoripoti,” amesema Bwana Lindmeir.
Maambukizi mengi yamesababishwa na aina na mnyumbuliko mpya wa COVID uitwao JN.1 ambao kwa sasa unachunguzwa kwa kina na WHO kama mnyumbuliko unaopaswa kufuatiliwa kwa karibu.
Kwa mara ya kwanza aina hiyo JN.1 ilibainika Marekani kabla ya kusambaa kwenye maeneo mengine kadhaa ya nchi.
Inatokana na mnyumbuliko wa COVID uitwao Omicron ambao ulihusishwa na ongezeko kubwa la maambukizi ya COVID-19 mwaka 2022.
Vituo vya Marekani vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) siku ya Alhamisi vilitoa tahadhari na kuwataka watoa huduma za afya kuongeza chanjo ya mafua, COVID-19 na virusi vya kupumua vya syncytial (RSV).
Mdhibiti wa afya alisema kuwa kuwepo kwa viwango vya chini vya chanjo, pamoja na kuongezeka kwa ugonjwa wa kupumua, kunaweza kusababisha ugonjwa mbaya zaidi na kuongezeka kwa uhitaji wa huduma za afya katika wiki zijazo.
Watoa huduma za afya wanapaswa kupendekeza dawa za kuzuia virusi vya mafua na COVID-19 kwa wagonjwa wote wanaostahiki, haswa wazee na watu walio katika hali fulani ya Kimatibabu, CDC ilisema.
Katika wiki nne zilizopita, Idadi ya watu kulazwa hospitalini kulingana na umri iliongezeka kwa asilimia 200% kwa mafua, 51% kwa COVID-19, na 60% kwa RSV, kulingana na data za CDC.
Kulikuwa na dozi milioni 7.4 za chanjo ya mafua ambazo ni chache kwa ajili ya watu wazima katika maduka ya dawa na ofisi za madaktari ikilinganishwa na msimu wa homa wa Mwaka 2022-2023.