Maumivu ya uume baada ya tendo
Baadhi ya Wanaume hupata tatizo la Maumivu ya uume baada ya tendo au wengine wakati wa tendo, je chanzo chake ni nini?
Zipo sababu nyingi ikiwemo matatizo ya nerves, maambukizi ya magonjwa kama vile genital herpes au hata wasiwasi tu wakati wa tendo n.k
Maumivu haya huweza kuathiri uwezo wako wa kufanya tendo, na kukufanya usifurahie tendo la ndoa, kukufanya ushindwe kumridhisha mke wako, kuwa muoga zaidi wa tendo n.k, Hivo ni muhimu kujua chanzo chake na kupata matibabu.
Maumivu ya uume baada ya tendo,chanzo chake
1. Tatizo la Uume kupinda(Curved Penis)
Tatizo linalojulikana kama Peyronie’s disease au curvature of the penis, ni miongoni mwa sababu kubwa za maumivu ya uume.
Maumivu kwenye uume wako wakati wa tendo inaweza kuwa ishara ya mapema ya hali hii, chanzo halisi cha tatizo hili hakijulikani, lakini watafiti wanashuku majeraha ya papo hapo au majeraha sugu ya uume au magonjwa kama vile autoimmune disease yanaweza kuleta hali hiyo.
2. Maambukizi ya Genital Herpes
Maambukizi ya zinaa kama vile Genital Herpes huweza kupelekea mtu kuwa na vidonda vyenye maumivu sehemu za siri, malengelenge au vipele,
Maambukizi haya ya Zinaa huweza kuathiri jinsia zote, na chanzo cha Genital herpes ni virusi wanaojulikana kama herpes simplex virus (HSV).
3. Kuvimba kwenye ngozi ya mbele ya Uume
Hii pia huweza kuwa Sababu ya Maumivu ya uume baada ya tendo, Tatizo la Kuvimba kwa ngozi ya mbele ya Uume(penis foreskin) kwa kitaalam hujulikana kama balanitis.
Tatizo hili mara nyingi hutokana na maambukizi ya magonjwa, tatizo la allergy(mzio), au baadhi ya matatizo ya ngozi,
Ingawa maambukizi ya Virusi pamoja na Bacteria huweza kuwa chanzo cha tatizo hili, Asilimia kubwa chanzo cha tatizo la balanitis ni maambukizi ya Fangasi.
Tatizo hili la kuvimba kwa ngozi ya mbele ya Uume hutokea Zaidi kwa Watu ambao hawajatahiriwa au wenye ugonjwa wa Kisukari ambao haujadhibitiwa.
4. Matatizo na Neva(Nerve Issues)
Ikiwa unajihusisha na michezo ambayo inaweza kupelekea kugongwa kwenye eneo la sehemu za siri au kutumia muda mrefu wa kukaa (kama vile mchezo wa kuendesha baiskeli n.k), unaweza kupata jeraha kwenye mishipa yako ya fahamu ambayo kwa kitaalam hujulikana kama pudendal nerve.
pudendal nerve ndyo huhusika na hisia kwenye sehemu ya siri.
Kupata maumivu ya Uume wakati wa tendo au hata baada ni dalili mojawapo ya tatizo la kuharibiwa kwa mishipa hii ya fahamu, tatizo ambalo kwa kitaalam hujulikana kama pudendal neuralgia.
5. Tatizo la kuvimba kwa tezi dume(Prostatitis)
Kama unapata maumivu ya uume hasa wakati wa kufika kileleni(ejaculation) unaweza kuwa na Tatizo la kuvimba kwa tezi dume(Prostatitis),
Tatizo hili huweza kusababisha maumivu kuzunguka eneo la njia ya haja kubwa(anus), kwenye uume, kwenye korodani,chini ya tumbo pamoja na mgongoni.
Tatizo la kuvimba kwa tezi dume(Prostatitis) huweza kusababishwa na sababu nyingi ikiwemo;
- Madhara ya maambukizi kwenye njia ya Mkojo(U.T.I complications)
- Magonjwa ya Zinaa(sexually transmitted infections (STIs)) n.k
6. Ngozi chini ya Uume kuwa fupi au kukaza(Short or Tight Frenulum)
frenulum ni mkusanyiko wa ngozi sehemu ya chini ya Uume ambayo inaunganisha kichwa cha uume na ngozi ya mbele “glans (the head of the penis) to the foreskin”.
Ikiwa ngozi hii imekuwa fupi au kukaza hujulikana kama frenulum breve,
Tatizo hili huweza kusababisha maumivu ya uume wakati uume ukiwa umesimama au wakati wa tendo la ndoa.
7. Matatizo ya ngozi(Skin Conditions)
Watu wenye matatizo ya ngozi kama vile tatizo la psoriasis, huweza kuwa na Upele au mabaka mabaka yenye magamba sehemu za siri.
maeneo ambayo huweza kuathiriwa ni pamoja na kwenye;
- Korodani
- Eneo ambapo nywele za sehemu za siri huota
- Kwenye kichwa cha uume
- Eneo la katikati ya uume
- Kwenye shina la Uume
- Eneo la matakoni
- Eneo katikati ya ngozi ya korodani(Scrotum) na matako,kwa kitaalam perineum
- Na maeneo yote ya karibu kwenye mikunjo
Pia, ikiwa unaona ngozi ya Uume inakuwa nyembamba zaidi na kuwa na mabaka mabaka meupe unaweza kuwa na shida ya lichen sclerosis,
Watu wenye shida hii huwa kwenye hatari ya kuchanika kwa ngozi ya uume wakati wa tendo au hata wakati uume ukisimama, hali ambayo huweza kusababisha maumivu ya Uume kabla,wakati au baada ya tendo.
8. Wasiwasi au Hofu(Tension or Anxiety)
Maumivu katika eneo la uzazi pia yanaweza kuunganishwa na matatizo ya kihisia. Utafiti mmoja uligundua kwamba wanaume wenye maumivu ya nyonga walikuwa na wasiwasi wa juu na viwango vikubwa vya hofu kuliko wale wasio na maumivu ya pelvic.
9. Ngozi ya mbele ya Uume kukaza sana(Tight Foreskin)
Ikiwa hujatahiriwa, govi lako, ambalo linafunika kichwa cha uume wako, huvutwa nyuma wakati Uume ukisimama. Mkunjo huo wa ngozi unapokwama au kupungua kwenye ncha na haurudi nyuma, unaweza kusababisha maumivu, tatizo hili kwa kitaalam huitwa phimosis.
10. Kufanya sana Tendo la Ndoa(Too Much Sex)
Kufanya mapenzi kupita kiasi Pia huweza kusababisha maumivu ya Uume wakati wa tendo, baada ya tendo au wakati wowote Uume ukisimama.
Maumivu ya uume Wakati wa tendo
Hizi hapa ni baadhi ya Sababu za maumivu ya Uume wakati wa tendo;
– Maambukizi ya magonjwa kama vile; Fangasi, baadhi ya magonjwa ya Zinaa kama vile herpes,chlamydia n.k
– Shida ya ngozi ya mbele ya uume kukaza sana, hali ambayo huweza kupelekea maumivu wakati wa kuingiza uume ukeni,kadri ngozi ya mbele inavyovutwa nyuma.
– Kupata michubuko kwenye uume, vidonda,au kuchanika kwa ngozi ya Uume n.k
– Kupata tatizo la Kuvimba kwa tezi dume (prostatitis) n.k
Matibabu ya Maumivu ya uume baada ya tendo
Matibabu yatatofautiana kulingana na sababu ya maumivu. Kwa mfano, antibiotics au dawa za kuzuia virusi zinaweza kutumika ikiwa maumivu yanatokana na maambukizi. Na Wakati mwingine taratibu za upasuaji zinaweza kufanyika kulingana na Sababu ya tatizo hili.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
>>SOMA PIA: MAUMIVU MAKALI WAKATI WA TENDO KWA MWANAMKE;
Rejea Za Mada hii;