Dalili za siku ya kushika mimba
Siku ya kushika mimba; Siku za kushika mimba ndyo zile kwa jina lingine hujulikana kama “Siku za Hatari”, hapa tunazungumzia kipindi cha yai kutoka kwenye Ovari(Ovulation) ili likutane na mbegu ya kiume kwa ajili ya Urutubishaji.
Wanawake huwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kushika mimba ndani ya siku moja au mbili baada ya ovulation, ambapo ni wakati ovari hutoa yai.
Hata hivyo, inawezekana kupata mimba katika siku zinazoongozana kwenye ovulation, kwani manii inaweza kuishi kwa siku kadhaa ndani ya mwili wa kike.
Hivo basi, hata wale wanaohitaji kubeba mimba ni lazima Ujue siku za hatari ni Zipi ili ufanye mapenzi kwenye siku ambazo unaweza kushika mimba,
Changamoto inakuja, nitajuaje niko kwenye siku za kushika mimba? hasa kwa wale ambao mzunguko wao wa hedhi haueleweki(Irregular menstrual cycle).
Kupitia Dalili, itakusaidia kujua kama Upo kwenye Siku ya Kushika Mimba, na katika Makala hii tumechambua baadhi ya dalili hizo.
Dalili za siku ya kushika mimba
Hapa tunazungumzia dalili za ovulation kwa lugha nyingine,
Hizi hapa ni baadhi ya Dalili za Siku ya kushika mimba;
– Tumbo kuanza kukaza kidogo sehemu ya chini(mild cramping in the lower abdomen)
– Kutoa ute mweupe Ukeni wenye kuvutika Zaidi kama ule wa Yai,
Ukiona hii ujue upo kwenye siku za hatari.
– Kuongezeka kwa Joto Mwilini(mwili kuwa wa moto)
– Kuwa na hamu Zaidi ya kufanya Mapenzi(higher sex drive) kuliko kawaida
Baadhi ya ishara hizi, kama vile joto la Mwili, zitaendelea kubadilika baada ya ovulation. Kwa sababu hii, mtu haupaswi kutumia halijoto pekee kutabiri kama upo kwenye siku kamili ya yai kutoka.
Inaweza kusaidia kwa mtu kufuatilia ishara kwa miezi michache ili kupata wazo la nini ni kawaida kwa mwili wako.
Lakini Unapaswa kukumbuka kuwa kuna vigezo kadhaa, na wakati wa ovulation unaweza kubadilika, mwezi hadi mwezi.
Chaguo jingine ni kutumia Vifaa vya kutabiri Siku wa mayai kutoka au kichunguzi cha uwezo wa kuzaa.
Ovulation kawaida hutokea kwenye nusu ya mzunguko wako wa hedhi. Hii ni takriban siku 14 kabla ya siku ya kwanza ya kipindi chako kinachofuata katika mzunguko wa Hedhi wa siku 28,
lakini muda kamili unaweza kutofautiana. Ishara kwamba unakaribia kutoa Yai inaweza kuwa tofauti. Hata hivyo, kuna baadhi ya mambo ambayo unaweza kuzingatia na kufuatilia baada ya muda ili kukusaidia kutabiri Siku ya kushika Mimba.
– Dalili Zingine za Siku ya kushika Mimba ni pamoja na;
- Kupata vimaumivu vya matiti
- Kuwa na hamu ya kufanya Mapenzi isiyoyakawaida
- Joto la mwili kuwa juu n.k
NB: Ingawa, kutumia ishara hizi Pekee kutabiri siku ya Kushika Mimba sio njia inayotegemewa zaidi.