Kiwango sahihi cha kusikiliza muziki ni kipi?, Siku ya usikivu duniani 2024.
Jana Tarehe 03, Jumapili ilikuwa ni Siku ya Usikivu Duniani, Leo yapo baadhi ya mambo yakuangalia na kukusaidia ili kuilinda afya ya masikio yako.
Kufahamu Zaidi kuhusu tatizo la Kupoteza Usikivu,Soma Zaidi hapa.
Fahamu mambo haya;
Kiwango sahihi cha kusikiliza muziki ni kipi?
Unaposikiliza Muziki kwa kutumia spika za masikioni (earphones/headphone), Hakikisha unatumia sauti ya chini ya asilimia 60 na usisikilize kwa muda wa zaidi ya saa moja kwa siku.
Nini cha kufanya sikio linapotoa usaha?
Kama sikio linatoa usaha, futa Kwa kutumia kitambaa safi .Usiweke pamba kuzuia usaha kutoka.
Nenda kwa haraka kituo cha huduma za afya kwa matibabu.
>> Soma zaidi hapa; Tatizo la masikio kutoa Usaha,chanzo,dalili na Tiba
watoto wasiogelee kwenye maji machafu ili kulinda afya ya masikio.
Tuwafundishe watoto waepuke kuogelea kwenye madimbwi yenye maji machafu au kuingiza maji masikioni ili kulinda afya ya masikio na usikivu.
Credits: elimu_ya_afya