Magonjwa
Tatizo la kupoteza Usikivu: Sababu, Dalili, na Matibabu
Tatizo la kupoteza Usikivu: Sababu, Dalili, na Matibabu
Kwa Mujibu wa Shirika la afya Duniani(WHO)
Kufikia 2050 karibu watu bilioni 2.5 wanakadiriwa kuwa na kiwango fulani cha upotevu wa Usikivu na angalau milioni 700 watahitaji urekebishaji wa kusikia yaani hearing rehabilitation.
Tatizo la kupoteza usikivu linaweza kuwa kizingiti kikubwa kwa maisha ya kila siku. Kwa bahati mbaya, tatizo hili la kiafya linaweza kuwaathiri watu wote, wakiwemo watoto, watu wazima, na wazee. Kwa hivyo, ni muhimu kufahamu sababu za tatizo la usikivu, dalili zake, na matibabu yanayopatikana.
YALIYOMO:
- Sababu za Tatizo la kupoteza Usikivu
- Aina za Tatizo la kupoteza Usikivu
- Dalili za Tatizo la kupoteza Usikivu
- Jinsi ya Kutambua Tatizo la kupoteza Usikivu
- Matibabu ya Tatizo la kupoteza Usikivu
- Njia za Kuzuia Tatizo la kupoteza Usikivu
- Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara kuhusu Tatizo la kupoteza Usikivu
- Hitimisho
Sababu za Tatizo la kupoteza Usikivu
Tatizo la kupoteza usikivu linaweza kuchangiwa na sababu nyingi, ikiwa ni pamoja na:
(1) Mtoto
– Swala la kigenetic,uwepo wa genes au vinasaba vya tatizo
– Maambukizi kwa mtoto akiwa bado tumboni yaani intrauterine infections – kama vile ya rubella pamoja na cytomegalovirus infection.
– Mtoto kuzaliwa akiwa na tatizo la kukosa hewa ya oxygen yaani birth asphyxia
– Mtoto kupata tatizo la manjano wakati wa kuzaliwa yaani hyperbilirubinemia (severe jaundice in the neonatal period)
– Mtoto kuzaliwa na tatizo la Uzito mdogo sana(low-birth weight) n.k
(2) Sababu kwa Ujumla
• Kupata maambukizi ya Sikio au masikio kwa muda mrefu
• Kupatwa na tatizo la meningitis pamoja na maambukizi mengine
• Tatizo la Maji kukusanyika kwenye eneo la ndani ya Sikio
• Kuweka maji kwenye sikio mfano wakati wa kuoga au kujisafisha n.k
• Uvutaji wa Sigara,Pia huongeza hatari ya kupata tatizo la kupoteza usikivu
• Kupata ajali au kuumia eneo la masikio pamoja na kichwani
• Kuwa kwenye sehemu zenye makelele sana mara kwa mara
• Tatizo la otosclerosis
• Kuwa na uchafu zaidi ambao umeganda ndani ya sikio au kuziba sikio/masikio
• Upotevu wa usikivu wa gafla kutokana na uharibu wa nerves yaani sudden sensorineural hearing loss.
• Kutumia dawa zinazoweza kuharibu masikio, ototoxic medicines
• Upungufu wa baadhi ya virutubisho muhimu
• Umri kuwa mkubwa zaidi au Kuzeeka
• Kupata mshtuko wa sauti kali n.k
Aina za Tatizo la Kupoteza Usikivu
Kuna aina mbili za tatizo la kupoteza usikivu:
- Tatizo la kupoteza usikivu la kudumu: hili ni tatizo la kudumu ambalo linahitaji matibabu ya kina ili kupunguza athari zake kwa maisha ya kila siku.
- Tatizo la kupoteza usikivu la muda mfupi: hili ni tatizo la muda mfupi ambalo linaweza kuisha bila hata matibabu yoyote.
Dalili za Tatizo la kupoteza Usikivu
Dalili za tatizo la kupoteza usikivu ni pamoja na:
– Mtu Kushindwa kusikia sauti za chini au sauti za juu
– Mtu Kushindwa kusikia wakati wa mazungumzo
– Mtu Kushindwa kusikia sauti za TV au redio
– Kupata maumivu au kutokwa na damu kwenye sikio
– Kutokwa na maji kwenye sikio
– Kupata mshtuko wa sauti kali
– Kusikia kelele isiyo ya kawaida ndani ya masikio yako n.k
Jinsi ya Kutambua Tatizo la kupoteza Usikivu
Kwa kawaida, kama unashindwa kusikia vizuri, au inakuwa vigumu kusikia sauti ya watu wanaokuzunguka, unapaswa kutafuta ushauri wa daktari wa masikio. Madaktari hawa watafanya vipimo ili kujua kwa nini unashindwa kusikia vizuri.
Vipimo hivi ni pamoja na:
- Vipimo vya sikio: Daktari atatumia kifaa maalum cha kujaribu kusikia sauti yako kwenye sikio. Kwa kutumia vipimo hivi, daktari ataweza kujua kama una tatizo la kupoteza usikivu na sababu za tatizo hilo.
- Vipimo vya uwezo wa kusikia: Daktari atafanya vipimo ili kujua uwezo wako wa kusikia sauti za aina tofauti.
- Vipimo vya ubongo: Vipimo hivi vinaweza kufanyika ili kujua ikiwa tatizo la kupoteza usikivu limeathiri ubongo wako.
Matibabu ya Tatizo la kupoteza usikivu Usikivu
Matibabu ya tatizo la kupoteza usikivu yanategemea sababu za tatizo hilo,
Ikiwa tatizo la kupoteza usikivu limechangiwa na maambukizi ya sikio, daktari atakupa dawa za kupunguza maumivu na kuzuia maambukizi kuendelea.
Ikiwa tatizo la kupoteza usikivu limechangiwa na uharibifu wa sikio, daktari atakupa chaguzi za matibabu kama vile vifaa vya kusaidia kusikia, matibabu ya upasuaji au vifaa vya kusaidia sikio n.k.
Njia za Kuzuia Tatizo la kupoteza Usikivu
Kuna njia kadhaa ambazo unaweza kutumia ili kuzuia tatizo la kupoteza usikivu, kama vile:
✓ Kuvaa vifaa vya kinga kwenye masikio yako wakati wa shughuli zinazohusisha makele mengi au wakati wa muziki mkubwa.
✓ Kuepuka kutumia vifaa vya sauti kwa muda mrefu sana ikiwa ni pamoja na kuvaa earphone kwa muda mrefu huku ukisikiliza mziki kwa sauti kubwa.
✓ Kuepuka kuweka maji kwenye sikio lako hasa wakati wa kujisafisha au kuoga,jisafishe kwa uangalifu huku ukiepuka kuweka maji ndani ya sikio lako
✓ Kufanya usafi sahihi wa masikio yako ili kuzuia maambukizi.
FAQs:Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara kuhusu Tatizo la kupoteza Usikivu
[sc_fs_multi_faq headline-0=”h3″ question-0=”Ni vipi tatizo la kupoteza usikivu linaweza kutibiwa?” answer-0=”Matibabu ya tatizo la kupoteza usikivu yanategemea sababu za tatizo hilo. Ikiwa tatizo la usikivu limechangiwa na maambukizi ya sikio, daktari atakupa dawa za kupunguza maumivu na kuzuia maambukizi kuendelea. Ikiwa tatizo la usikivu limechangiwa na uharibifu wa sikio, daktari atakupa chaguzi za matibabu kama vile vifaa vya kusaidia kusikia, matibabu ya upasuaji au vifaa vya kusaidia sikio n.k.” image-0=”” headline-1=”h3″ question-1=”Je, kuna njia yoyote ya kuzuia tatizo la kupoteza usikivu?” answer-1=”Njia kadhaa za kuzuia tatizo la kupoteza usikivu ni pamoja na kuvaa vifaa vya kinga kwenye masikio wakati wa shughuli zinazohusisha makelele zaidi au wakati wa muziki mkubwa, kuepuka kutumia vifaa vya sauti kwa muda mrefu sana, kuepuka kuweka maji kwenye sikio lako, na kufanya usafi sahihi wa masikio yako ili kuzuia maambukizi.” image-1=”” count=”2″ html=”true” css_class=””]
Hitimisho
Tatizo la kupoteza usikivu ni tatizo linaloweza kuathiri watu wa umri wowote. Ikiwa una shida ya kusikia, ni muhimu kutafuta ushauri wa daktari wa masikio ili kujua sababu za tatizo hilo na kupata matibabu sahihi,
Kuna njia kadhaa za kuzuia tatizo la kupoteza usikivu, kama vile kuvaa vifaa vya kinga kwenye masikio, kuepuka kutumia vifaa vya sauti kwa muda mrefu sana, na kufanya usafi sahihi wa masikio yako.
Kumbuka, kinga ni bora kuliko tiba, na kuzuia tatizo la kupoteza usikivu kunaweza kusaidia kulinda afya yako ya masikio kwa muda mrefu.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
-
Magonjwa6 days ago
Dalili za acid reflux,Soma hapa Kufahamu
-
magonjwa ya wanawake5 days ago
Dalili za Ectopic pregnancy,Mimba kutunga nje ya kizazi
-
Elimu&Ushauri4 days ago
Afya za watu bilioni 1.8 duniani matatani kwa kutokufanya Mazoezi – WHO
-
Magonjwa2 days ago
Ugonjwa wa ngozi sehemu za siri
-
Events1 day ago
Chad yafanikiwa kuondoa Ugonjwa wa trypanosomiasis,WHO yatangaza
-
News4 days ago
Mlipuko Mbaya wa homa ya nyani watokea tena KIVU KASKAZINI
-
Events6 days ago
Princess Anne alilazwa hospitalini na majeraha madogo kufuatia tukio nyumbani kwake
-
Uzazi/Ujauzito10 hours ago
Dalili za hatari baada ya kujifungua kwa upasuaji