Fahamu Dalili zinazoonyesha hufanyi Mazoezi ya kutosha
Kwa mujibu wa Tafiti mbali mbali zilizofanyika,Mtu akiwa hafanyi mazoezi;Zipo dalili mbali mbali ambazo huweza kujitokeza,na baadhi ya dalili hizo ni pamoja na;
– Kupata shida ya choo kigumu au kukosa choo kabsa(Constipation)
Unapofanya mazoezi, Utumbo mpana au koloni husogea zaidi, na ni rahisi kupata choo hasa kwa muda ule ule ambao umezoea kupata.
Toni ya misuli yenye afya katika tumbo lako na diaphragm pia ni ufunguo wa kuhamisha taka kupitia kwenye njia yako ya utumbo. Mazoezi ya mara kwa mara yanaweza kukusaidia Upate choo vizuri, haswa unapozeeka.
– Kukakamaa kwa joints
Hii pia ni mojawapo ya dalili kubwa kwamba hufanyi Mazoezi,
ingawa wakati mwingine kukakamaa kwa joints huweza kuwa dalili ya matatizo mengine ya kiafya kama vile; Tatizo la arthritis au autoimmune disease.
Lakini fahamu;viungo pamoja na joints vinaweza pia kukakamaa wakati huvitumii vya kutosha. Hakikisha viungo vyako na joints zinafanya kazi.
– Kuishiwa na pumzi haraka
Kama vile misuli ya mikono hudhoofika usipoitumia, misuli inayosaidia mapafu yako kuingiza na kutoa hewa unapopumua hupoteza nguvu usipoifanyia kazi mara kwa mara.
Kadri unavyofanya shughuli chache, ndivyo unavyokosa pumzi, hata wakati wa kazi rahisi za kila siku.
– Kuathiri hali ya kihisia,Moody n.k
Kutokufanya mazoezi huleta madhara zaidi ya kwenye afya yako ya kimwili, Hali hii Inaweza pia kuongeza hisia za wasiwasi,Msongo wa mawazo,huzuni n.k
Hakikisha unachangamsha damu yako mara kwa mara. Mazoezi ya Cardio kama vile kutembea, kuendesha baiskeli, kuogelea, au kukimbia, yataimarisha na kuleta hali nzuri ya kiafya, na hata kuboresha kujistahi kwako yaani “self-esteem”.
– Kuhisi uchovu ambao hauishi
Je, unahisi uvivu na uchovu mara nyingi? Mazoezi husaidia kutoa oksijeni na virutubisho kwa tishu zako. Ikiwa unatumia muda wako mwingi kukaa, Tishu hazipati nguvu ya kutosha ili kukufanya uwe active.
– Kupata Tatizo la kukosa Usingizi
Ikiwa umechoka kuhesabu mabati usiku, inuka na ufanye mazoezi wakati wa mchana. Unapoweka utaratibu wa kufanya mazoezi ya kawaida, unalala haraka, na unalala vizuri zaidi mara tu usingizi unapokukamata.
– Kuanza kusahau vitu mara kwa mara
Mazoezi ya kawaida huambia mwili wako kutengeneza kemikali zaidi zinazojulikana kama “growth factors”.
Hii huongeza uzalishaji wa damu kwenye mishipa ya damu kwenye ubongo wako. Kadiri damu inavyoingia kwenye ubongo wako, ndivyo unavyoweza kufikiria, kukumbuka vizuri na kufanya maamuzi bora Zaidi.
– Tatizo la kupanda kwa Shinikizo la damu(blood pressure)
Kutumia muda wako mwingi kukaa huongeza hatari ya kupata ugonjwa wa moyo. Hiyo ni kwa sababu una uwezekano mkubwa wa kuwa na shinikizo la damu, ambapo ni sababu kubwa ya kuongeza hatari ya kupata matatizo ya moyo ikiwemo; ugonjwa wa mishipa ya moyo na mshtuko wa moyo(coronary artery disease and heart attack).
– Tatizo la kuongezeka kwa Sukari mara kwa mara(Prediabetes)
Ikiwa kufanya Mazoezi ni sehemu ya kawaida ya maisha yako, mwili wako huwa na wakati mzuri na rahisi wa kuweka kiwango chako cha glucose kwenye damu chini ya udhibiti mzuri.
Viwango thabiti vya sukari kwenye damu hukuweka nje ya eneo la hatari la kupata ugonjwa wa kisukari cha aina ya 2.
– Kupata tatizo la kuumwa Mgongo
Wakati misuli yako ya mwili ikiwa ni dhaifu kutokana na kutokufanya mazoezi, haiwezi kusupport mgongo wako jinsi inavyopaswa, hii huchangia uanze kuwa na tatizo la kuumwa mgongo.
– Kula kila mara
kwa kawaida;Inaonekana ungekuwa na njaa mara nyingi zaidi ikiwa ungefanya mazoezi zaidi, lakini kinyume chake ni kweli pia. Mazoezi ya Aerobic kama vile kuendesha baiskeli, kuogelea, kutembea, na kukimbia yanaweza kupunguza hamu yako ya kula kwa sababu hubadilisha viwango vya baadhi ya “homoni za njaa” katika mwili wako.
– Kuumwa mara kwa mara
Tafiti zinaonyesha kadri unavyofanya Mazoezi ndivyo unavyopunguza uwezekano wa kupata mafua au vijidudu vingine. Unapofanya mazoezi kuwa mazoea yako, mfumo wako wa kinga unakuwa na nguvu Zaidi dhidi ya kupambana na magonjwa.
Review via Link;
https://www.webmd.com/fitness-exercise/ss/slideshow-surprising-signs-youre-not-moving-enough