Ugonjwa wa fistula kwa wanaume,chanzo,dalili na Tiba
Watu wengi hawajui kwamba Ugonjwa wa Fistula sio kwa Wanawake pekee, hata wanaume wanaweza kupata Ugonjwa wa Fistula,
Ugonjwa wa fistula ni nini?
Ugonjwa wa Fistula huhusisha kuwepo kwa tundu au uhusiano usio wa kawaida kati ya sehemu mbili za mwili, kama vile kiungo kimoja na kingine,mishipa ya damu,tishu na tishu n.k.
Zipo aina mbali mbali za fistula kama vile;
- Vesicovaginal fistula(kwa wanawake)
- Uterovaginal fistula(kwa wanawake)
- Anal fistula(Kwa wote) n.k
Fahamu kwamba,Hata Wanaume huweza kupata Fistula, na Leo tunachambua zaidi kuhusu Ugonjwa wa fistula kwa wanaume,chanzo,dalili na Tiba yake.
Anorectal fistula ni aina ya fistula ambayo hutokea zaidi kwa wanaume kuliko kwa wanawake, Ingawa fistula aina ya anorectal inaweza kutokea kwa watu wa umri wowote na jinsia yeyote.
Chanzo cha Ugonjwa wa fistula kwa wanaume
Kama tulivyokisha kueleza wanaume hupatwa Zaidi na fistula aina ya Anorectal fistula,
na kwa asilimia kubwa aina hii ya anal fistula husababishwa na maambukizi ya vimelea vya magonjwa ambayo huanza ndani ya tezi linalojulikana kama anal gland,
Maambukizi haya husababisha jipu ambalo hutoka lenyewe au kutolewa kwa upasuaji kupitia ngozi karibu na njia ya haja kubwa.
Sababu zinazoongeza hatari ya Mtu kupata anal fistula
Sababu zinazoongeza hatari ya Mtu kupata fistula aina ya anal fistula ni pamoja na;
1. Kuwa na Jipu eneo la haja kubwa lililotolewa hapo awali
2. Kuwa na magonjwa kama vile;
- Crohn's disease
- Au inflammatory bowel disease n.k
3. Kuumia eneo la haja Kubwa
4. Kupata maambukizi ya vimelea vya magonjwa sehemu ya haja kubwa
5. Kufanyiwa upasuaji eneo la haja kubwa
6. Upasuaji au mionzi kwa ajili ya matibabu ya saratani ya eneo la haja kubwa(anal cancer) n.k
Dalili za anal fistula
Dalili za anal fistula ni pamoja na ;
- Kupata muwasho kuzunguka eneo la haja kubwa
- kupata maumivu eneo la haja kubwa ambayo ni endelevu na yanayozidi wakati wa;
- kukaa,
- kutembea,
- kujisaidia haja kubwa
- au kukohoa
- Kutokwa na uchafu wenye harufu mbaya eneo karibu na njia ya haja kubwa
- Kutokwa na damu au Usaha wakati wa kujisaidia haja kubwa
- Kupata Homa hasa pale ukiwa na jipu n.k
- Eneo la kuzunguka njia ya haja kubwa kuvimba na kubadilika rangi na kuwa jekundu n.k
- Kushindwa kudhibiti haja kubwa, na kutoka pasipo kujizuia wewe mwenyewe.n.k
Matibabu ya Ugonjwa wa Fistula kwa Wanaume
Matibabu ya Ugonjwa wa Fistula hutegemea na chanzo chake, ila kwa ujumla mgonjwa huweza kupata matibabu ya;
- Upasuaji
- Pamoja na Dawa mbali mbali
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.