Madhara ya kidole tumbo,Ukiona hili ujue haya ni madhara yake
Fahamu kwamba ukiwa na tatizo kwenye kidole tumbo(appendix) usipopata tiba, kidole tumbo au appendix huweza kupasuka na kusababisha madhara makubwa ikiwemo maambukizi ambayo huweza kutishia maisha(potentially life-threatening infections).
Katika Makala hii tumeelezea Zaidi kuhusu madhara makubwa yanayoweza kutokea ikiwa una tatizo kwenye Kidole tumbo, lakini pia dalili za tatizo la kidole tumbo(appendix).
Dalili za kidole tumbo(appendix)
Ikiwa una tatizo la kidole tumbo au appendix hizi ni dalili zinazoweza kujitokeza kwako;
1. Kupata Maumivu ya ghafla ambayo huanza upande wa kulia wa tumbo la chini(lower abdomen)
2. Kupata Maumivu ya ghafla ambayo huanza karibu na kitovu na mara nyingi huhamia kwenye tumbo la chini upande wa kulia.
3. Kupata Maumivu ambayo huongezeka wakati wa kukohoa, kutembea au kufanya shughuli zingine zinazohusisha movements.
4. Kuhisi hali ya Kichefuchefu na kutapika mara kwa mara
5. Kupoteza hamu ya kula.
6. Kupata Homa ya kiwango cha chini ambayo inaweza kuongezeka kadiri ugonjwa unavyozidi kuwa mbaya.
7. Kupata tatizo la Kuvimbiwa,kupata choo kigumu au kukosa choo kabsa(constipation)
8. Wengine hupata tatizo la kuharisha
9. Kupata tatizo la Kuvimba kwa tumbo.
10. Tumbo kujaa Gesi mara kwa mara n.k.
Soma Zaidi hapa kuhusu tatizo la kidole tumbo(appendix),chanzo, dalili na Tiba yake
Madhara ya kidole tumbo
yapo madhara ambayo unaweza kuyapata endapo una tatizo la kidole tumbo(appendix);
– Kupata tatizo la kidole tumbo kupasuka:
Ikiwa kidole tumbo(appendix) kina tatizo huweza kuvimba “appendicitis” na kama usipopata tiba ya hali hii kidole tumbo huweza kupasuka na kusababisha madhara makubwa ikiwemo maambukizi ambayo huweza kuhatarisha maisha yako.
NB: Unashauriwa kutafta msaada wa matibabu haraka ikiwa unapata maumivu ya tumbo ambayo huwa makali sana kwa ghafla na husambaa kuzunguka eneo lote la tumbo.
– Kupata tatizo la Peritonitis:
Ikiwa kidole tumbo au appendix imepasuka, kuta za ndani ya tumbo(peritoneum) huweza kupata maambukizi ya bacteria, Hii ndyo hujulikana kama peritonitis.
Maambukizi haya huweza kuhatarisha maisha yako. Pia huweza kuharibu viungo vyako vya ndani(Internal organs).
Dalili za maambukizi haya(peritonitis) ni pamoja na:
- Kupata maumivu makali ya tumbo ambayo ni endelevu
- Kuhisi hali ya kuumwa
- Kupata homa
- Joto la mwili kuwa juu
- Mapigo ya moyo kwenda mbio
- Kukosa pumzi na kupumua haraka
- Tumbo kuvimba
Maambukizi haya yasipotibiwa haraka matokeo yake ni Kifo.
Matibabu ya maambukizi haya(peritonitis);
Kwa kawaida tiba ya maambukizi haya ya bacteria huhusisha matumizi ya dawa jamii ya antibiotics, pamoja na Upasuaji wa kuondoa kabsa kidole tumbo(appendix).
– Kupata tatizo la majipu(Abscesses):
Kwa baadhi ya watu moja ya madhara ambayo huweza kupata ikiwa wana tatizo la kidole tumbo ni pamoja na kuwa na jipu au majipu,
Wakati mwingine jipu hutokea karibu na kidole tumbo kilichopasuka. Huu ni mkusanyiko wenye uchungu wa usaha ambao huundwa wakati mwili unajaribu kupambana na maambukizi.
Na Katika hali adimu, jipu linaweza kutokea kama shida baada ya upasuaji wa kuondoa appendix.
Matibabu:
Wakati mwingine jipu linaweza kutibiwa kwa kutumia dawa jamii ya antibiotics, lakini katika hali nyingi usaha huhitaji kutolewa kwenye jipu(drained).
Njia Hii inaweza kutekelezwa baada ya kufanya vipimo kama ultrasound au CT scan. Utapewa ganzi eneo husika na sindano itachomwa kupitia ngozi yako, ikifuatiwa na uwekaji wa bomba.
Ikiwa jipu litapatikana wakati wa upasuaji, eneo hilo huoshwa kwa uangalifu na kozi ya antibiotics hutolewa.”
**Hayo ndiyo baadhi ya madhara ya Kidole tumbo…!!!!
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.