Fahamu kuhusu Saratani ya Ovari(ovarian cancer)
Saratani ya Ovari, hii ni Saratani ambayo hutokea kwenye vifuko vya mayai(Ovaries),
Saratani hii huhusisha tatizo la seli hai zilizopo eneo la vifuko vya mayai kukuwa na kuongezeka kuliko kawaida.
Dalili za Saratani ya Ovari
Dalili za Saratani ya Ovari ni pamoja na;
– Mgonjwa kuhisi haja ya kukojoa kila mara
– Mgonjwa kushiba haraka sana wakati wa kula
– Mgonjwa Kuhisi tumbo kujaa sana
– Kubadilika kwa mzunguko wako wa hedhi
– Kublid mara mbili ndani ya mwezi mmoja
– Uzito wa mwili kupungua kwa kiasi kikubwa
– Mgonjwa kupata shida ya choo kigumu
– Wakati mwingine kupata maumivu ya tumbo chini ya kitovu
Kundi ambalo lipo kwenye hatari ya kupata Saratani ya Ovari
WATU AMBAO WAPO KWENYE HATARI YA KUPATA KANSA YA VIFUKO VYA MAYAI NI PAMOJA NA;
• Watu ambao kuna mgonjwa wa tatizo hili katika familia yao
• Watu ambao huanza kuona siku zao za hedhi wakiwa na umri mdogo sana
• Watu ambao huwahi kukoma hedhi yao ya mwezi yaani Menopause
• Wanaotumia vidonge vya uzazi wa mpango hovio
MATIBABU YA Saratani ya Ovari au Saratani ya VIFUKO VYA MAYAI
– Yapo matibabu mbali mbali ya aina hii ya kansa kama vile;
- Njia ya upasuaji na kuondoa ovary moja au zote mbili kama zimeathirika na kansa hii,
- Huduma ya Chemotherapy
- pamoja na matibabu mengine ambayo huhusu zaidi kudhibiti dalili za ugonjwa huu wa kansa ya vifuko vya mayai
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.