Ticker

6/recent/ticker-posts

Bangi hupelekea Mtu kuona visivyokuwepo,DCEA



Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imesema bangi ni dawa haramu inayoongozwa kwa kupatikana na kutumiwa zaidi nchini ikifuatiwa na heroin,mirungi na cocaine na hivi karibuni methamphetamine ambapo amesema dawa hizo zina madhara ya kiafya ikiwemo Mtu kuona visivyokuwepo na kupelekea kufanya vitu visivvyofaa kwenye Jamii.

Akiongea Jijini Dar es salaam leo, Kamishna Msaidizi wa Kinga na Huduma za Jamii DCEA, Moza Makumbuli amesema bangi ni miongoni mwa vileta njozi ambapo humfanya Mtumiaji kuhisi, kuona au kusikia vitu visivyokuwepo au tofauti na uhalisia.

Makumbuli amewataka Watanzania kujiepusha na matumizi ya bangi na dawa nyingine za kulevya kwakuwa zina madhara huku akishangaa Watumiaji wa mitandao kutofurahia pale madhara ya bangi yanaposemwa au bangi ikikamatwa “Suala la bangi ni mtihani inaonekana wengi wanatumia, hata ukiangalia habari mfano ile ya biskuti za bangi mtandaoni comment za Watu ni kama vile wanaona bangi inachelewa kuhalalishwa, bangi haifai tujiepushe kutumia”



Post a Comment

0 Comments