Ticker

6/recent/ticker-posts

jinsi ya kupunguza cholesterol mwilini



jinsi ya kupunguza cholesterol mwilini, jinsi ya kuondoa cholesterol mwilini 

Kama una kiwango kikubwa cha cholestrol mwilini,basi upo kwenye hatari ya kupata magonjwa mbali mbali ikiwemo magonjwa ya Moyo. Katika makala hii tumechambua baadhi ya Njia za kukusaidia kama una kiwango kikubwa cha cholestrol mwilini,

fahamu hapa jinsi ya kupunguza cholesterol mwilini au jinsi ya kuondoa cholesterol mwilini.

jinsi ya kupunguza cholesterol mwilini

Punguza kiwango cha Cholestrol kwa haraka Zaidi kwa kutumia njia hizi hapa;

1. Punguza Uzito au dhibiti tatizo la Uzito mkubwa,

Kama una tatizo la Cholestrol kuzidi mwilini halafu una Uzito mkubwa(overweight), hakikisha unapungua.

Tafiti zinaonyesha ikiwa una Uzito mkubwa halafu ukapunguza kiwango cha paundi 10 tu, hii inaweza kusaidia kupunguza kiwango cha cholestrol(LDL) mwilini mpaka kwa asilimia 8%.

2. Choma mafuta mwilini(Ban Trans Fats)

Kuwa na Mafuta mengi mwilini(Trans fats) huongeza kiwango cha cholestrol(LDL), na pia huongeza hatari ya wewe kupata magonjwa ya Moyo pamoja na kiharusi au Stroke.

Hivo punguza mafuta haya kwa njia mbali mbali ikiwemo kuzingatia aina ya vyakula unavyokula, kufanya mazoezi n.k

3. Fanya Mazoezi,

Hata ukifanya Mazoezi angalau tu masaa mawili na Nusu kwa wiki huweza kusaidia kudhibiti kiwango cha cholestrol mwilini(LDL pamoja na triglycerides)

Hivo hakikisha unafanya mazoezi, ikiwa kazi zako ni za kukaa kwa muda mrefu hakikisha unafanya mazoezi angalau kwa dakika 30 kilasiku.

4. Kula vyakula bora vyenye afya ikiwa ni pamoja na vyakula vyenye kiwango kikubwa cha nyuzinyuzi(Fiber)

Epuka kabsa ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi sana au chumvi nyingi,

Badala yake kula mboga za majani,matunda pamoja na vyakula vingine vyenye kiwango kikubwa cha nyuzinyuzi(fiber).

nyuzinyuzi(fiber), hupunguza kiwango cha ufyonzwaji wa cholesterol mwilini, hivo kusaidia kupunguza kiwango cha cholestrol mwilini.

5. Punguza nyama badala yake kula Samaki Zaidi

Kula Samaki mara mbili mpaka Nne kwa wiki; sio tu omega-3 fats kutoka kwa samaki itakusaidia kuboresha afya ya Moyo, lakini itachukua nafasi ya nyama nyekundu na kupunguza kiwango cha cholestrol mwilini.

6. Tumia mafuta ya mzeituni(Olive Oil),

Tafiti zinaonyesha kubadilisha mafuta ya Mzeituni kwa Siagi husaidia kupunguza kiwango cha cholestrol mwilini(LDL cholesterol) kwa asilimia 15%,

Aina ya Fat nzuri ndani ya mafuta ya mzeituni husaidia afya ya Moyo, Chagua mafuta asilimia yaliyofanyiwa processing kwa kiwango kidogo na kuwa na kiwango kikubwa cha antioxidants, ambapo husaidia kuzuia magonjwa.

7. Tumia Karanga,

Karanga huweza kusaidia kupunguza kiwango cha Cholestrol mwilini, hii ni kwa Sababu;

Karanga Zina sterols, ambazo kama vile nyuzinyuzi(fiber), hupunguza kiwango cha ufyonzwaji wa cholesterol mwilini.

8. Zingatia baadhi ya Viungo,

Mfano; vitunguu saumu, tangawizi, pilipili nyeusi, pamoja na mdalasini hufanya zaidi ya kuongeza ladha ya chakula chako, vitu hivi vinaweza pia kuboresha kiwango cha cholesterol mwilini.

Utafiti unaonyesha kuwa kula kitunguu saumu nusu hadi kimoja kila siku kunaweza kupunguza kiwango cha cholesterol mwilini hadi kwa asilimia 9%.

9. Epuka au Acha kabsa Uvutaji wa Sigara,

Tafiti zinaonyesha kuwa,; Uvutaji wa Sigara ni mojawapo ya Sababu za kuongeza kiwango cha cholestrol mwilini,

Sio tu kwa Wavutaji wa Sigara, hata wale ambao hupatwa na moshi wa sigara kutoka kwa wanaovuta(secondhand smokers).

Hitimisho:

Hizo ni baadhi ya Njia za Jinsi ya kupunguza cholesterol mwilini au jinsi ya kuondoa cholestrol Mwilini. Zingatia kwa ajili ya Afya yako….!!!!



Post a Comment

0 Comments