Ticker

6/recent/ticker-posts

Jinsi ya Kupata Mimba haraka,Fahamu hapa Siri hii



Jinsi ya Kupata Mimba haraka,Fahamu hapa Siri hii

Swala la kupata Mimba haraka kwa muda unaotaka wewe,ni changamoto kwa watu wengi, hali ambayo hupelekea migogoro mingi katika mahusiano na hata baadhi ya ndoa kuvunjika.

Zipo Dondoo mbali mbali ambazo ukizizingatia zinaweza kukusaidia kupata Mimba haraka, katika Makala hii tumechambua baadhi ya Njia hizo.

Kupata Mimba haraka

Hizi hapa ni baadhi ya Dondoo za kukusaidia kupata Mimba haraka;

1. Kufanya Mapenzi mara kwa mara;

Fahamu kwamba, uwezekano wa kubeba Mimba huongezeka Zaidi kwa wanandoa au wapenzi ambao hupata muda mwingi wa kufanya mapenzi mara kwa mara,

Tafiti zinaonyesha kwamba; Viwango vya kubeba mimba huongezeka Zaidi kwa Wapenzi wanaofanya mapenzi kila siku au kila baada ya siku moja tofauti na wale ambao hukutana mara chache Zaidi.

2. Kufanya Mapenzi karibu na kipindi cha yai kutoka(ovulation).

Watu wengi huhangaika na swala la kupata Mimba kwa Sababu hufanya mapenzi siku ambazo huwezi kupata Mimba,

Kitu cha kwanza ambacho ni muhimu,unatakiwa kuufahamu vizuri mzunguko wako wa hedhi na kujua “SIKU ZA HATARI” ni Zipi, Maana hapa ndyo unaweza kubeba Mimba.

Ikiwa kujamiiana kila siku haiwezekani – fanya Mapenzi kila baada ya siku 2 hadi 3 kwa wiki kuanzia mara tu baada ya kumalizika kwa kipindi chako cha hedhi. Hii inaweza kusaidia kuhakikisha kwamba unafanya Mapenzi wakati una uwezekano mkubwa wa kubeba Mimba kwa haraka Zaidi.

3. Hakikisha unadhibiti Uzito wako wa Mwili(normal weight).

Watu wengi hawafahamu kwamba, kuwa na Uzito mkubwa(Overweight) au Uzito mdogo Zaidi(underweight) huongeza hatari ya kupata matatizo ya Mayai kutoka kwenye Ovari(ovulation disorders) kwa Mwanamke.

4. Fanya Checkup kwanza kabla ya kuhangaika na Ujauzito,

Wataalam pia wanashauri ufanye Kitu kinaitwa “preconception checkup”.

Kabla ya kuanza kujaribu rasmi, pata uchunguzi kwanza. Muulize daktari wako juu ya vitamini vya ujauzito ambavyo vina folic acid, ambayo husaidia kulinda dhidi ya kasoro kadhaa za kuzaliwa, kama vile spina bifida Foliki asidi hufanya kazi katika hatua za mapema za ujauzito, kwa hiyo ni muhimu kuhakikisha kuwa unapata Foliki asidi ya kutosha kabla na baada ya kupata mimba.

5. Ujue Vizuri Mzunguko wako wa Hedhi

Je! Unajua kiasi gani kuhusu mzunguko wako wa hedhi? Kuelewa kwa kweli hukusaidia kujua wakati unaweza kupata Mimba. Ovulation ndio wakati mzuri zaidi wa kupata mimba. “Huu ndio wakati wa kuzingatia kufanya Mapenzi,”

6. Mkao Sahihi wa kufanya Mapenzi na kupata Mimba,

Usiwe na wasiwasi kuhusu mkao rahisi wa kufanya Mapenzi na kupata Mimba

Kuna dhana nyingi sana kuhusu Mkao mzuri wa kupata mimba, lakini hizo ni dhana tu,

Kwa kweli hakuna ushahidi wa kisayansi unaonyesha kwamba Mkao flani wa kufanya mapenzi kama vile “missionary position” ni bora kuliko mwanamke kuwa juu linapokuja suala la kuongeza nafasi ya kupata mtoto. Na hii inathibitishwa na Majarida mbali mbali ya Wataalam wa afya kama vile WebMd.

Ingawa Mkao wa Kukaa au Kusimama wakati wa kufanya Mapenzi huweza kupunguza kiwango cha mbegu za kiume kupanda juu, kwa Sababu ya gravity inavuta chini.

7. Tulia kidogo kitandani baada ya kufanya Mapenzi

Unashauriwa kutokukimbilia kuamka mara moja baada ya kufanya Mapenzi, tulia kidogo kitandani.

Unashauriwa kutulia kitandani angalau kwa dakika 10 mpaka 15 baada ya kufanya Mapenzi,Usiwahi kwenda bafuni kunawa na maji,

Ikiwa utatulia kwa dakika 10-15, mbegu za kiume(sperm) ambazo zilikuwa zinaenda kwenye Mlango wa kizazi(Cervix) zitakuwa tayari zimeshafika eneo husika.

Hii inaongeza nafasi ya mbegu za kiume kusafiri mpaka kwenye kizazi na kukutana na yai kwa ajili ya Urutubishaji.

8. Hakikisha hufanyi tendo la ndoa ukiwa kwenye hali ya Msongo wa Mawazo(De-stress any way you can).

Jaribu kutofadhaika na kuwa na MSongo wa mawazo sana kuhusu kuanzisha familia. “Tulia tu na itafanyika,”

Fahamu Msongo wa mawazo unaweza kutatiza hata yai kutoka kwenye Ovari(ovulation) na kupunguza Zaidi uwezo wa wewe kubeba mimba kwa wakati unaohitaji.

9. Pamoja na Dondoo Zingine za kubadilisha mtindo wa Maisha zinaweza kukusaidia kupata Mimba kwa haraka,Mfano;

  • Kuacha kabsa Matumizi ya Pombe kwa mwanamke na Mwanaume
  • Kuacha kabsa Uvutaji wa Sigara au kutumia kilevyi cha aina yoyote
  • Kutokutumia dawa pasipo maelekezo kutoka kwa Wataalam wa afya n.k

Ni matumaini Yangu umejifunza Dondoo muhimu za Kukusaidia kubeba Mimba kwa haraka Zaidi…!!!!

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



Post a Comment

0 Comments