kutokwa na uchafu kwenye uume,chanzo na Tiba yake
kutokwa na uchafu kwenye uume ambapo wengine husema kutokwa na uchafu mweupe kwenye uume, wengine husema kutokwa na usaha kwenye uume n.k, je hali hii hutokana na nini?
Kwa Mwanaume, mara nyingi kutokwa na uchafu kwenye uume ni dalili ya maambukizi ya magonjwa,
na wakati mwingine huambatana na dalili zingine kama vile; Kupata maumivu wakati wa kukojoa, kupata Maumivu wakati wa tendo n.k
Magonjwa ya Zinaa kama vile; Ugonjwa wa Chlamydia, Kisonono(Gonorrhoea), Trichomoniasis,Mycoplasma genitalium n.k, huweza kusababisha Mwanaume kutokwa na uchafu kwenye Uume.
Kumbuka; Uchafu huu tunaozungumzia hapa ni tofauti na maji maji ambayo huweza kutangulia kutoka kabla ya tendo,mwanaume anapokuwa amesisimka kihisia na kuhitaji kufanya mapenzi.
Ikiwa unatokwa na uchafu kwenye Uume ambao una rangi isiyoyakawaida, unatoa harufu, upo kama usaha n.k, hizi ni dalili za maambukizi ya magonjwa.
UWEPO WA TATIZO LA KUTOKA USAHA KWENYE UUME WAKATI WA KUKOJOA
kutoa usaha kwenye uume
Tatizo la Kuwepo kwa chembechembe za usaha au usaha kwenye mkojo hujulikana kama pyuria ambapo linaweza kuonekana kwa kutumia hadubini (microscope) au kama tatizo ni kubwa linaweza kuonekana kwa macho.
•Soma: Ugonjwa wa Tezi Dume, chanzo,Dalili zake pamoja na Matibabu yake
VISABABISHI VYA TATIZO HILI LA KUTOKWA NA USAHA KWENYE UUME
Zipo sababu mbalimbali ambazo huchangia sana kutokea kwa hali ya kutokwa na usaha kwenye uume wakati wa kukojoa,ambapo ni pamoja na;
- Ugonjwa au maambukizi katika mfumo wa mkojo yaani UTI ambapo huhusisha Maambukizi kwenye figo, kwenye mrija wa mkojo na kwenye kibofu cha mkojo (cystitis- amabayo huonekana sana)
- Magonjwa ya Zinaa-Kama ugonjwa wa kisonono au ‘’gono’’ kama wengi wanavyoita, ugonjwa wa Chlamydia na Trichomoniasis
- Sumu inayotokana na kemikali (Chemical poisoning) kama 4-Aminodiphenyl inayotumika kwenye maabara kwa ajili ya tafiti mbalimbali
- Tatizo linajulikana kama Reiter’s syndrome
- Pyelonephritis-Maambukizi ya bakteria kwenye sehemu za figo zinazojulikana kama calyces, renal pelvis na tishu za figo .Madhara ya pyelonephritis ambayo husabababisha ugonjwa unaojulikana kama renal abscessMl
- Maambukizi kwenye tezi dume-Prostatitis (Kwa wanaume)
- Upungufu wa kinga mwilini
- Uvimbe kutokana na kuwepo kwa mawe kwenye kibofu cha mkojo au kwenye figo
- Mzio (Allergy) au kuota uvimbe sehemu yoyote ya mfumo wa mkojo
DALILI ZA UWEPO WA TATIZO HILI
Viashiria vya tatizo hili pamoja na dalili zake ni Pamoja na;
-Maumivu makali ya kuchoma (Painful burning sensation) wakati wa kukojoa
-Maumivu chini ya kitovu
-Homa
-Kutapika
– Usaha kutoka wakati wa kukojoa
-Tatizo hii likidumu kwa muda mrefu husababisha kupungua uzito kwa mgonjwa
•Soma: Ugonjwa wa Tezi Dume, chanzo,Dalili zake pamoja na Matibabu yake
MATIBABU Ya Tatizo Hili
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
WEKA COMMENT HAPA..!!!
image quote pre code