Ticker

6/recent/ticker-posts

Ujue Ugonjwa Wa PID (Pelvic Inflammatory Disease)



Ujue Ugonjwa Wa PID (Pelvic Inflammatory Disease)

Pid ni ugonjwa gani?

PID ni Maambukizi ya bacteria Kwenye Via vya Uzazi vya Mwanamke, yaani pelvic inflammatory disease,

Infection kwenye kizazi ni moja ya matatizo ambayo huwaathiri sana wanawake. Kwa kawaida maambukizi haya huusisha shingo ya uzazi (cervix) hali ambayo hujulikana kama cervicitis, nyama ya mfuko wa uzazi (endometrium) ambayo kitaalamu huitwa endometritis, na mirija ya uzazi (fallopian tubes) hali ijulikanayo kitabibu kama salpingitis.

Chanzo cha ugonjwa wa PID

PID husababishwa na nini?chanzo kikuu cha Pid

Pamoja na aina kadhaa za vimelea kuhusishwa na PID, vimelea vya jamii ya Neisseria Gonorrhoeae pamoja na Chlamydia trachomatis ndivyo vinavyoongoza zaidi kuwa chanzo cha Pid kwa wanawake.

Je mwanamke hupataje PID?

Kwa Njia hizi hapa chini ni rahsi sana kwa mwanamke kupata maambukizi katika via vyake vya Uzazi.

(1) Kufanya mapenzi au ngono isiyo salama

(2) Kupata maambukizi katika via vya uzazi mara baada ya mama tu Kujifungua ambapo kitaalam huitwa “POSTPARTUM INFECTION”

(3) Maambukizi ambayo mwanamke huweza kuyapata mara tu baada kutoa mimba kwa Njia zisizo salama kitaalam huitwa Post abortion infection au baada ya mimba kutoka yenyewe ambapo kitaalam huitwa post miscarrage infection

(4) Matumizi ya baadhi ya Njia za Uzazi wa mpango kama lupu au(IUCD)  ambapo mwanamke kuweza kupata PID wakati wa uwekaji n.k

(5) Maambukizi kwa Njia ya damu kutoka kwa Mtu mwenye maambukizi katika via vya Uzazi

Dalili za Ugonjwa wa PID ni zipi?

Zipo dalili kadhaa za ugonjwa huu wa PID. Miongoni mwa dalili hizi ni;

  • Mwanamke kuhisi maumivu ya tumbo hasa maeneo ya chini ya kitovu
  • Kupata maumivu ya mgongo
  • Mwanamke kutokwa na uchafu sehemu za siri wenye rangi kama njano n.k. Utoko huu huambatana na harufu mbaya.
  • Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa
  • Kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa
  • Kutoka damu bila mpangilio wakati wa hedhi
  • Kupata homa
  • Wakati fulani kuhisi kichefuchefu na Pia kutapika

MADHARA YA Ugonjwa wa PID(MAAMBUKIZI KATIKA VIA VYA UZAZI VYA MWANAMKE)

1- Mwanamke kushindwa kabsa kubeba Mimba au Ujauzito,

Mtu mwenye PID anaweza kupata mimba?

Moja ya madhara ya PID ni kuathiri uwezo wa mwanamke kupata Ujauzito

2- Ujauzito kutoka hasa katika miezi 3 ya mwanzoni

3- Kutokwa na uchafu unaombatana na harafu kali hata kukukosesha raha,hasa hasa kama Upo kwenye mahusiano ya kimapenzi

4- Kupata maumivu makali chini ya Kitovu wakati wa Tendo la Ndoa

5- Kupata maumivu wakati wa period huku ikiambatana na damu nyeusi,yenye mabonge mabonge  na wakati mwingine kutoka nyama kama Vipande vya maini.

6-Hali ya kichefuchefu na kutapika kutokea

7-Uke kuwa Mkavu hata kuleta maumivu wakati wa Tendo la Ndoa.

Vipimo vya Ugonjwa wa pid:

Baadhi ya vipimo kwa Mtu mwenye dalili za Ugonjwa wa PID ni kama ifuatavyo;

➖Kuchunguza mkojo kwenye darubini ili kutambua aina za vimelea vinavyomletea mgonjwa maambukizi. Lakini pia Mkojo huweza kutumiwa kwa kuoteshwa katika maabara kwa ajili ya kutambua aina nyingine za vimelea viletavyo maambukizi hayo.

➖Kipimo cha Damu kwa ajili ya kuchunguza vimelea mbali mbali vya Magonjwa ikiwemo PID,ambapo kitaalam kipimo hichi huitwa Full Blood Picture.

➖Uchanguzi wa utando unaozunguka shingo ya uzazi ambapo huweza kutumika vifaaa kama SPECULUM

➖Mwanamke mwenye dalili hizi kufanya kipimo cha ULTRASOUND

TIBA YA UGONJWA WA PID

Kama una tatizo la PId waone wataalamu wa afya au nenda Hospital kwa Ajili ya vipimo na matibabu kamili,Kumbuka ukifika hospital unaweza kufanyiwa vipimo kama ULTRASOUND na kupata matibabu sahihi kwako.

Baada ya Ugonjwa wa PID kugundulika,mgonjwa atapewa  dawa za kutibu ugonjwa huu. Shirika la Afya Duniani (WHO)  limeonyesha baadhi ya miongozo na maelekezo ya kutibu Ugonjwa wa PID.

Baadhi ya dawa zilizoorodheshwa kwa ajili ya matibabu ya maambukizi katika via vya uzazi vya mwanamke(PID) ni pamoja na Cefotetan na Doxycycline; Clindamycin pamoja na Gentamycin; Ampicillin na Sulbactam kwa pamoja na Doxycycline; na Ceftriaxone au Cefoxitin pamoja na Doxycycline.

KINGA DHIDI YA UGONJWA WA PID

✓Kutokufanya ngono zembe kwani hiki ni mojawapo ya Chanzo cha Kupata ugonjwa wa PID

✓Kutokufanya tendo la ndoa mara tu baada Ya kujifungua kwani mlango wa uzazi utakuwa bado haujafunga vizuri na ni rahis kupata maambukizi pia

✓Fanya vipimo vya mara kwa mara hasa ukiwa na dalili kama nilizozitaja hapo juu

✓Muone mtaalam wa afya pale tu unapojihisi tofauti

NB: KAMA UNA TATIZO HILI NA MENGINE TUWASILIANE KUPITIA Namba 0758286584.

 BONUS TIPS:MAUMIVU WAKATI WA TENDO LA NDOA

Wanawake wengi wamekuwa wakilalamika Juu ya Tatizo hili siku hizi.

Wengine Hata kushindwa kabsa Kushiriki Tendo la Ndoa,kwa kuogopa Maumivu ambayo wamekuwa wakiyapata Wakati wa Tendo la Ndoa.

VISABABISHI VYA MAUMIVU MAKALI WAKATI WA TENDO LA NDOA

(1)Kuvimba kwa Kuta za Uke- Na hii huweza kuusababishwa na FANGASI aina ya CANDIDA ALBICANS au BACTERIA

(2)Uvimbe wa Kizazi au Shingo ya Kizazi Huweza kuleta hali hii ya Maumivu makali wakati wa Tendo la Ndoa

(3)Mirija ya kizazi kuziba-Hali hii inaweza kukuletea maumivu makali wakati wa Tendo la Ndoa

(4)Saratani ya Shingo ya Kizazi-Mojawapo ya dalili za kansa ya shingo ya kizazi ni mwanamke kupata maumivu makali wakati wa Tendo la Ndoa

(5)Ukavu wa sehemu za siri-Hali hii huweza kupelekea maumivu makali pamoja na michubuko sehem za Siri wakati wa Tendo la Ndoa

KUMBUKA; JUKUMU LANGU KWAKO,NI KUKUSHAURI,KUKUELIMISHA NA KUKUPA MSAADA WA KIAFYA PALE INAPOHITAJIKA

kwa ushauri/Elimu/Tiba mawasiliano ni +255758286584.



Post a Comment

0 Comments