Magonjwa
Sababu za Kutokubeba Ujauzito(Sababu za kutokushika Mimba)
Sababu za Kutokubeba Ujauzito(Sababu za kutokushika Mimba)
Hizi ni baadhi ya Sababu ambazo hupelekea mwanamke kutokushika Mimba au kutokubeba Ujauzito,
1. Kutokujaribu kwa Muda mrefu au Muda wa Kutosha, Watu wengi hujaribu kwa Muda mfupi tu kisha kuanza kukata tamaa,
Na hii huanza kuleta migogoro hasa kwa Wenye ndoa ambao wana muda mfupi tu toka waoane,
Unachotakiwa kufahamu ni kwamba;Takribani Asilimia 80% ya watu wanaoshiriki mapenzi kwa Lengo la Kubeba Mimba wanafanikiwa baada ya miezi sita ya kujaribu,
Takribani asilimia 90% watakuwa wajawazito baada ya miezi 12 ya kujaribu kupata mimba,
Na Viwango hivi ni pale tu ambapo tunatarajia umejaribu kufanya mapenzi wakati unaofaa kila mwezi.
Hata kama huoni Dalili zozote za kuwa na tatizo kiafya, Lakini endapo mmejaribu kutafuta mtoto kulingana na mazingira haya hapa chini lakini hamjafanikiwa ni lazima muonane na wataalam wa afya;
– Una umri wa miaka 35 au zaidi na umejaribu kwa angalau miezi sita bila mafanikio
– Una umri wa chini ya miaka 35 na umejaribu kwa angalau mwaka mmoja bila mafanikio yoyote
2. Kutokufanya Mapenzi wakati Sahihi, hapa tunamaanisha wakati ambao mwanamke anaweza kubeba Mimba,
Kwa Lugha nyingine lazima mfanye mapenzi kwenye “siku za hatari” Siku ambazo mwanamke anaweza kubeba Mimba,
Kama hamfanyi mapenzi kwenye siku ambazo mwanamke anaweza kubeba mimba hakuna matokeo yoyote mnaweza kupata, hivo kutokutambua ni wakati gani sahihi wa kufanya mapenzi huweza kupelekea mwanamke asibebe ujauzito hata kama hana tatizo lolote.
3. Mwanamke kushindwa kupevusha Mayai,
Tatizo la Anovulation ambapo shida hutokea kwenye mayai pamoja na vifuko vya mayai(ovaries),
Shida ya mayai kushindwa kupevushwa huchangiwa na sababu mbali mbali ikiwemo;
– Tatizo la Polycystic ovary syndrome (PCOS)
– Shida ya Mwanamke kuwa na Uzito Mkubwa au Uzito mdogo sana(overweight or underweight),
– Tatizo la primary ovarian insufficiency,
– shida kwenye tezi la Thyroid yaani thyroid dysfunction, hyperprolactinemia.
– Kufanya mazoezi kupita kiasi(excessive exercise) n.k
Wanawake wengi wenye shida ya Ovulation, pia hupata shida ya kuwa na Hedhi isiyoeleweka yaani irregular periods,
Ingawa pia kuwa na hedhi inayoeleweka(regular menstrual cycles) haimaanishi kwamba huna shida yoyote kwenye ovulation.
4. Shida kwa Mwanaume,
Asilimia kubwa kwenye Jamii zetu endapo tatizo la Mwanamke kutokubeba Mimba limetokea,Lawama zote huwa juu yake, bila kujua hata Mwanaume huweza kuwa chanzo kikubwa cha Tatizo hili,
Matatizo kama vile; Mwanaume kuzalisha mbegu ambazo hazina ubora wowote na chache yaani Low sperm counts huweza kupelekea mwanamke kutokubeba mimba,
Mwanaume kutokuzalisha kabsa mbegu za Kiume, hili tatizo ni chanzo kikubwa cha Mwanamke kutokubeba mimba,
HIVO,Linapokuja swala la Kubeba Mimba, Mwanaume na Mwanamke huweza kuwa chanzo.
5. Umri kuwa Mkubwa, kadri Umri wako unavyokuwa Mkubwa ndivo uwezo wa kubeba Mimba au kutungisha Mimba hupungua zaidi,
Tafiti zinaonyesha kwa Wanawake baada ya miaka 35, huweza kuchukua muda mrefu zaidi kushika Mimba,
Na anapofikia ukomo wa hedhi,ndivo na Swala la kubeba mimba huwa historia.
Vivo hivyo kwa Wanaume, Wanaume wenye umri wa baada ya Miaka 40 baadhi yao hupata changamoto ya kutungisha Mimba Kwa Mwanamke.
6. Tatizo la kuziba kwa Mirija ya Uzazi kwa Wanawake yaani blocked fallopian tubes.
7. Mwanamke kuwa na tatizo la endometriosis,
Baadhi ya tafiti zinaonyesha kwamba,Takribani asilimia 50% ya wanawake wenye tatizo la endometriosis huwa vigumu pia kwao kubeba Ujauzito.
8. Matatizo mengine ni kama vile;
– thyroid imbalance
– Shida ya kisukari(undiagnosed diabetes)
– Baadhi ya autoimmune diseases, kama vile lupus,
– Magonjwa ya Zinaa(sexually transmitted infection (STI))
– Maambukizi ya magonjwa kama vile UTI sugu,Fangasi,PID n.k haya huweza kuchangia pia hasa endapo yamekuwa matatizo Sugu au ambayo hayajapata Tiba kwa Muda mrefu
– Shida ya wasiwasi na Msongo mkubwa wa Mawazo n.k
9. Matumizi ya baadhi ya Dawa, baadhi ya Dawa huweza kuathiri pia uwezo wa Mwanamke Kubeba Mimba,
10. Mtindo mbaya wa Maisha ikiwemo;
– Matumizi ya dawa za Kulevyia,Cocaine,Marijuana, n.k
– Uvutaji wa Sigara,Tumbaku,Kutumia Ugoro
– Unywaji wa Pombe kupita kiasi n.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.