Dalili za bacteria kwenye damu

Dalili za bacteria kwenye damu

Maambukizi ya bacteria kwenye damu husababisha kinga ya mwili kujibu mashambulizi na kutoa matokeo mbali mbali mwilini,

endapo mwili wako una mwitikio mkali sana kwa maambukizi haya, hii kwa kitaalam hujulikana kama Sepsis.

Ingawa Sepsis sio lazima iwe bacteria pekee, mwili huweza kuonyesha mwitikio mkali dhidi ya maambukizi ya vimelea mbali mbali kwenye damu ikiwemo; Virusi, Fangasi n.k

Dalili za bacteria kwenye damu

Dalili za maambukizi ya bacteria kwenye damu ni pamoja na;

– Mtu kuwa na homa

– Mwili kutetemeka au kuhisi baridi(chills)

– Kuhisi kichefuchefu na kutapika

– Mwili kuchoka kuliko kawaida

– Mwili kukosa nguvu au kuwa dhaifu

– Wengine kuharisha

– Kutoa Sana jasho mwilini

– Kupata maumivu mbali mbali kama vile ya;

  • Kichwa
  • Viungo
  • Joints
  • Misuli n.k

– Kupata Vipele kwenye Ngozi

– Kuhisi kizunguzungu

– Kupumua haraka haraka au kupata shida ya kupumua

– Kuwa na dalili kama za kuchanganyikiwa

– Kukojoa kidogo kuliko kawaida au kutokojoa kabisa

– Mapigo ya moyo kwenda mbio

– Kupata shida ya kusimama

– Kuhisi usingizi sana na kuwa na ugumu wa kuamka

– Kuwa na machafuko makubwa au matatizo mengine ya kufikiri n.k

Watu ambao wapo kwenye hatari ya kupata maambukizi ya bacteria kwenye damu

1. Wenye Kinga ya Mwili dhaifu

2. Wenye matatizo mbali mbali ya kiafya kama vile;

3. Wajawazito, kwa Sababu ya kinga yao ya mwili kuwa dhaifu katika kipindi hiki

4. Waliowahi kuwa na tatizo la Sepsis huko nyuma

5. Wenye umri wa Zaidi ya miaka 65, hasa hasa wakiwa na matatizo mengine ya kiafya

6. Waliokuwa wamelazwa hospital kwa kuugua sana au kufanyiwa Upasuaji

7. Wanaotumia mpira wa Mkojo(catheters) au wakupumulia(breathing tubes)

8. Wenye Vidonda mbali mbali n.k

Vipimo

Unaweza kufanya Vipimo hivi kwa ajili ya kuangalia afya yako kwa Ujumla;

  • Kipimo cha damu(Blood test)
  • X-ray
  • CT scan
  • MRI

Matibabu ya bacteria kwenye damu

Baada ya kugundulika kwamba una maambukizi ya bacteria kwenye damu zipo tiba mbali mbali unaweza kuanza kupata ikiwemo;

✓ Dawa za Vidonge Jamii ya Antibiotics

✓ Sindano n.k

Kumbuka; Maambukizi ya bacteria yanaweza kuwa makali hadi kusababisha tatizo la Sepsis, ambalo huweza hata kuhatarisha maisha yako, Hivo hakikisha unapata tiba ili kujikinga na Madhara Zaidi.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!