Ticker

6/recent/ticker-posts

kupoteza nywele, Pia kutokwa na damu kwenye fizi baada ya kunyanyua vitu VIZITO



kupoteza nywele, Pia kutokwa na damu kwenye fizi baada ya kunyanyua vitu VIZITO

Adele Johnston alikuwa akila vizuri na kufanya mazoezi ya kujenga mwili.

Adele, ambaye alishinda medali ya dhahabu katika mashindano ya kuinua vyuma, alianza kupoteza nywele zake. Pia kutokwa na damu kwenye fizi, mapigo ya moyo kuongezeka, kuwashwa na ngozi na kuvimba sehemu za siri.

Baada ya miaka mingi ya vipimo na matibabu mbalimbali, aligunduliwa kuwa na dalili zinazompata mwanamke anapokaribia kukatika kwa hedhi.

Kawaida dalili huanza baada ya umri wa miaka 45. Lakini Adele, mama wa watoto wawili, alikuwa na umri wa miaka thelathini.

“Kwa miaka mingi nilikuwa nikiusukuma mwili wangu kupita uwezo wake. Kujenga mwili ni mchezo mgumu sana na sikuwa imara vya kutosha,” aliiambia BBC.

“Unaweza kuona mbavu zangu na muundo wa mifupa. Nilikuwa nimedhoofika sana, mwili wangu haukuwa mzuri wala haukuwa na afya jinsi nilivyoonekana. Ndipo nilipoamua kubadilisha mtindo wa maisha.”

Adele, ana urefu wa futi 5 na inchi 8, alikuwa na uzito wa kilo 53 tu alipoanza kujenga mwili. Sasa uzito wake umepungua zaidi.

“Nilianza kuhoji kwa nini napata dalili za kukata hedhi mapema. Nilimuuliza daktari, ikiwa ni kwa sababu ya kujenga mwili wangu. Daktari alisema inaweza kuwa, lakini hatukuwa na utafiti wowote,” alisema.

Daktari wa magonjwa ya wanawake, Dkt. Heather Currie, anasema kujenga mwili kupita kiasi kunaweza kuwa sababu ya tatizo la Adele.

Dkt. Currie pia ni mshauri wa Serikali ya Scotland kuhusu kukoma hedhi na afya ya wanawake. Anasema, baada ya Adele kuacha kujenga mwili, ovari zake zinaweza kurudi kawaida.

“Labda ujenzi wa mwili umeathiri, lakini hatuwezi kujua,” anasema.

Adele sasa ameacha kujenga mwili. Lakini wakati huo huo, anafanyiwa tiba ya uingizwaji wa homoni ili kupunguza dalili za kukoma kwa hedhi.

Adele, ana umri wa miaka 40 sasa, afya yake imeimarika.

“Zilikuwa dalili za kutisha za kukoma kwa hedhi. Moyo wangu ulienda mbio. Nilidhani nitapata mshtuko wa moyo. Sikuweza kulala usiku. Nilikuwa nikichoka sana. Nitokwa na jasho na kuwashwa kila mahali.

“Nilikuwa naumwa sana ukeni hadi nisimame nikiwa kazini, tumbo lilikuwa limevimba na fizi zinavuja damu, nywele zilikuwa zikinitoka, yote yalinishangaza sana.”

Wanawake wengine

Kukoma hedhi ni wakati ambapo mzunguko wa hedhi wa mwanamke hukata. Kikawaida hutokea mwanamke anapokaribia umri wa miaka hamsini.

Wakati hedhi inapokaribia kukata, wanawake wengi hupata mzunguko wao wa hedhi usio wa kawaida. Wanakumbana na matatizo ya kihisi au ya kimwili ambayo hawajawahi kuyapata.

Vicky McCann, mwenyekiti wa Shirikisho la Kujenga Mwili, Uingereza, anasema uhusiano kati ya kujenga mwili na dalili za mapema za kukoma hedhi ni mada ya kuvutia.

Vicky ana umri wa miaka 54. Anasema, “nimekuwa nikishiriki mashindano kwa miaka 30. Lakini nilianza kupata dalili za kukoma hedhi miaka mitatu iliyopita.

Nimekula na kufanya mazoezi sana maisha yangu yote. Bado sikukumbana na tatizo lolote. Ninaweza pia kusema, kuna watu wengine watatu wa umri wangu ambao nawajua na hawajapata matatizo yoyote.

“Lakini, kila mtu yuko tofauti.”

Jessica Watson, mwanzilishi mwenza wa shirika la elimu ya wanawake waliomaliza kuzaa, Gloria, anasema anajua kesi nyingi kama za Adele.

“Kuna hitaji la haraka la utafiti kuhusu sababu au mambo mengine yanayohusiana na kukoma kwa hedhi mapema. Ndiyo maana tunajenga ufahamu kila mara,” anasema.

Via bbc:Mada



Post a Comment

0 Comments