Ticker

6/recent/ticker-posts

Hizi ni tabia 11 zinazouharibu ubongo wako



Hizi ni tabia 11 zinazouharibu ubongo wako

Kuna watu wengi ambao hawapendi kutoka nje, Wengine hupenda kutumia wakati wao wakiwa wamelala kwenye chumba chenye giza au kusikiliza muziki kwa sauti kubwa kwenye vipokea sauti vya masikioni.

Lakini utafiti umebaini kwamba tabia hii ina athari mbaya kwenye ubongo.

Katika makala haya, tutajadili tabia 11 kama hizo, ambazo zinaharibu ubongo wako. Pamoja na hayo, tutajua pia jinsi ya kuyashinda mazoea hayo.

Taarifa katika makala haya imekusanywa kutoka kwenye ripoti mbalimbali za utafiti, zikiwemo zile za Shule ya Kitabibu ya Harvard na Taasisi ya Kitaifa ya Marekani ya Magonjwa ya Neurological and Stroke.

1) Kutokupata Usingizi wa kutosha

Kwa mujibu wa kituo cha Sayansi ya mfumo wa neva (Neurology) cha Marekani, uharibifu mkubwa zaidi kwa ubongo wetu unasababishwa na kutokupata usingizi wa kutosha.

Kwa watu wazima unatakiwa upate muda wa kulala kuanzia saa 7 hadi 8 za usingizi kati ya saa 24 kwa siku. Wataalamu wanasema kuwa kulala mfululizo usiku ni bora zaidi.

Soma Zaidi masaa yanayohitajika kulala kwa kila Mtu

Ubongo hupumzika baada ya kulala. Pia, ubongo huunda seli mpya wakati wa kulala. Lakini ikiwa unalala chini ya saa 7, seli mpya haziundwi.

Hatimaye, unaanza kupata matatizo kama vile;

  • Kupoteza kumbukumbu
  • Unapata ugumu wa kuzingatia.
  • Ugumu wa kufanya maamuzi.

Ukosefu wa usingizi pia huongeza hatari ya kupata tatizo la akili.

Ikiwa unataka kulinda ubongo wako, kuna suluhisho moja tu. Pata angalau saa saba za kulala kila usiku,Saa nane za kulala ni bora zaidi.

Soma zaidi hapa mbinu za kukusaidia upate Usingizi bora

2. Kuepuka kifungua kinywa

Baada ya kutokula usiku kucha, kifungua kinywa hutoa nishati ya kufanya kazi siku nzima. Lakini wengi wetu hukimbia asubuhi na kuruka kitu muhimu kama kifungua kinywa.

Kufanya hivyo kunapunguza viwango vya sukari kwenye damu, jambo ambalo huathiri ubongo.

Kutopata kifungua kinywa siku baada ya siku husababisha uharibifu wa ubongo, hupunguza ufanisi wa seli.

Ukosefu wa virutubisho hufanya iwe vigumu kwa ubongo kufanya kazi kwa kawaida.

3. Kutokunywa maji ya kutosha

Fahamu asilimia 75% ya ubongo wetu ni maji.

Kwa hivyo kuweka ubongo katika hali ya unyevu ni muhimu sana kwa utendaji kazi wake bora.

Ukosefu wa maji husababisha tishu za ubongo kupungua na seli kupoteza kazi.

Jambo hili linaweza kupunguza uwezo wa kufikiri kimantiki au kufanya maamuzi.

Kwa mujibu wa wataalamu, mtu mzima anapaswa kunywa angalau lita mbili za maji kwa siku ili kudumisha afya ya ubongo.

Katika unywaji huu wa maji unaweza kuongezeka kulingana na uzito wako, afya, umri, mtindo wa maisha na hali ya hewa.

Soma Zaidi faida za kunywa maji ya kutosha mwilini

4. Kuwa na msongo wa mawazo wa hali ya juu

Msongo wa mawazo wa muda mrefu husababisha seli za ubongo kufa na sehemu ya mbele ya ubongo kusinyaa. Inaathiri kumbukumbu na uwezo wetu wa kufikiria.

Kulingana na watafiti, Msongo wa mawazo ni mojawapo ya Sababu kubwa zinazoathiri uwezo wa ubongo kufanya kazi, hivo ni muhimu sana kudhibiti tatizo hili.

Soma Zaidi hapa; Tatizo la Msongo wa mawazo na jinsi ya kulidhibiti

5. Matumizi ya Vifaa saidizi kupita kiasi

Matumizi ya vitu kama vikokotoo kwa muda mrefu, kila kitu kuuliza mtandaoni bila kufikiri hata kidogo n.k

Tabia hizi huathiri uwezo wa ubongo kufanya kazi, ambapo pia huweka kuathiri uwezo wa kufikiri na kutunza kumbukumbu kwa muda mrefu.

6. Kutumia vipokea sauti kila wakati, kusikiliza muziki kwa sauti kubwa

Vipokea sauti vinavyobanwa kichwani au AirPods unazotumia zinaweza kukudhuru kwa chini ya dakika 30.

Kusikiliza kwa sauti kubwa au kwa muda mrefu  nakwa kelele kubwa kunaweza kusababisha upotevu mkubwa wa kusikia.

Pia inahofiwa kwamba kusikia kwako kunapoharibika, hakuwezi kurekebishwa.

Kupoteza uwezo wa kusikia huathiri moja kwa moja ubongo.

Kulingana na watafiti wa Marekani, watu wenye upotevu wa kusikia wanakabiliwa na uharibifu wa tishu za ubongo. Hii huongeza hatari kwao ya kupata shida ya kupoteza kumbukumbu.

Ikiwa unasikiliza nyimbo kwa kutumia vipokea sauti vya masikioni kwa muda mrefu, usiongeze sauti zaidi ya asilimia 60. Pumzika kwa saa moja bila kutumia vipokea sauti vya masikioni mfululizo.

7. Kuwa peke yako kila wakati, na kutochangamana na watu

Kuzungumza na watu ni muhimu sana kwa afya ya ubongo wako.

Kutumia muda mwingi peke yako ni mbaya kwa ubongo wako kama vile kutopata usingizi wa kutosha.

Kuwa na marafiki na familia huweka akili zetu safi.

Badala yake, upweke huongeza hatari ya unyogovu, wasiwasi na shida ya akili.

Ikiwa unataka kuweka ubongo wako ukiwa na afya, tumia wakati na marafiki wa karibu na familia mara kwa mara. Lakini,wanapaswa kuwa ‘watu wenye mawazo chanya’.

8. Mawazo na watu hasi

Ikiwa una tabia ya kuwaza hasi kila wakati, mawazo hasi kama hakuna kitu kinachoweza kutokea kwako, hali ya ulimwengu ni mbaya sana, siku zijazo ni giza, huna bahati, ni hatari kwa ubongo.

Kwa sababu mawazo mabaya huunda msongo wa mawazo, unyogovu na wasiwasi kwa upande mwingine.

Vile vile, Amyloid na Tau hujilimbikiza kwenye ubongo. Ambayo ni sababu kuu ya shida ya akili na kumbukumbu.

Kwa hiyo, jaribu kuacha mawazo mabaya mara moja. Kufanya hivi mara kwa mara itakuwa tabia.

Ikiwa huwezi kufanya hivyo peke yako, tafuta msaada wa daktari wa akili.

Kuepuka urafiki mbaya pia ni muhimu sana. Jaribu kujizuia kutazama habari mbaya sana.

9. Kutumia muda mwingi gizani

Utafiti nchini Marekani umeonesha kuwa watu ambao hutumia muda mwingi gizani au kutumia muda mrefu katika maeneo yaliyofungwa ambapo hakuna mwanga mwingi na mzunguko wa hewa, mazingira huweka shinikizo sana kwenye ubongo.

Ili kuweka ubongo wako katika hali ya afya njema, unapaswa kwenda juani kila siku. Nenda nje. Ikiwa uko nyumbani, fungua milango na madirisha.

10. Tabia ya kula kupita kiasi

Haijalishi jinsi chakula ni ‘cha afya’ kiasi gani, kula kupita kiasi kunaweza kuharibu ubongo.

Utafiti umeonesha kuwa ulaji kupita kiasi pia huziba mishipa ya ubongo na kupunguza mtiririko wa damu.

Hii inasababisha kupoteza kumbukumbu na uwezo wa kufikiri. Ambayo inaweza kusababisha shida ya akili.

Kula vyakula visivyofaa, vyakula vya kukaanga, vyakula vyenye sukari nyingi, vinywaji baridi, n.k. huongeza hatari ya matatizo kwenye ubongo.

11. Muda wa kutumia skrini

Muda mwingi wa kutumia kifaa kama computer,Simu,TV,n.k una athari kubwa kwenye ukuaji wa ubongo. Utumiaji mwingi wa simu za mkononi kwa watoto husababisha uharibifu zaidi kwenye gamba la mbele, ambalo hutofautiana kutoka ujana hadi miaka 25.

Utafiti umeonesha kuwa watoto wanaotumia zaidi ya saa saba kwa siku mbele ya skrini wanakuwa na gamba jembamba la ubongo.

Kwa sababu kukaa muda mrefu kwenye simu za mkononi kunaweza kusababisha shida kama vile maumivu ya kichwa, kuchanganyikiwa na uvimbe wa ubongo.

Kwa sababu hii, muda wa kukaa kwenye skrini kwa watoto unapaswa kupunguzwa kabisa. Pia, usilale na simu yako karibu na mwili wako.

Weka simu kwenye begi badala ya mfukoni. Ikiwa unataka kuzungumza kwa muda mrefu, unaweza kuzungumza kupitia spika bila kushikilia simu kwenye sikio lako. Kutuma ujumbe wa maandishi ni bora kuliko kuzungumza.



Post a Comment

0 Comments