Ticker

6/recent/ticker-posts

Ndoa za utotoni zaongezeka SUDAN:Wataalam UN



Ndoa za utotoni zaongezeka  SUDAN:Wataalam UN

wasichana wakimbizi wa ndani katika kituo kinachosaidiwa na UNICEF cha Al Salam Sudan.Picha

Wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa leo wameelezea wasiwasi wao kuhusu kuongezeka kwa ripoti za ulanguzi wa binadamu hasa wanawake na wasichana, kwa madhumuni ya unyanyasaji wa kingono na utumwa wa kingono, ndoa za utotoni na za kulazimishwa, na kuajiri wavulana kushiriki katika mapigano nchini Sudan, kutokana na kuendelea kuzorota kwa mgogoro wa kibinadamu nchini humo ambao umesababisha watu zaidi ya milioni 9 kufungasha virago na kuyahama makazi yao.

Kwa mujibu wa wattalm hao upatikanaji wa msaada kwa waathirika na manusura wa vita umeripotiwa kuzorota tangu Desemba 2023, miezi minane baada ya kuzuka kwa vita kati ya Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) na Vikosi vya jeshi la Sudan (SAF) mwezi Aprili 2023.

Katika tarifa yao iliyotolewa mjini Geneva Uswis hii leo wamesema Vijana wa kike na wwanawake, wakiwemo wakimbizi wa ndani wanaripotiwa kusafirishwa kwa ajili ya utumwa wa ngono na aina nyingine za unyanyasaji wa kingono.

Wataalam wamesema “Tunashangazwa ma kusikitishwa na ripoti za wanawake na wasichana kuuzwa katika masoko ya watumwa katika maeneo yanayodhibitiwa na vikosi vya RSF na makundi mengine yenye silaha, ikiwa ni pamoja na Darfur Kaskazini.”

Ndoa za utotoni zaongezeka pia

Wataalamu hao pia wameelezea wasiwasi wao kuhusu ongezeko la ndoa za utotoni na za shuruti, zinazoripotiwa kuwa ni matokeo ya kutengana kwa familia na ukatili wa kijinsia, ikiwa ni pamoja na ubakaji na mimba zisizotarajiwa.

 Wameongeza kuwa “Licha ya thadhari ya mapema kwa mamlaka zote za Sudan na wawakilishi wa RSF, tunaendelea kupokea ripoti za kuajiriwa kwa watoto kushiriki kikamilifu katika mapigano, ikiwa ni pamoja na kutoka nchi jirani.”

Wameendelea kusema kuwa “Kuajiriwa kwa watoto na makundi yenye silaha kwa aina yoyote ya unyonyaji ikiwa ni pamoja na katika majukumu ya vita ni ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, uhalifu mkubwa na ukiukaji wa sheria za kimataifa za binadamu”.

Wataalamu hao pia wameelezea wasiwasi wao kwa kuendelea kwa uporaji na mashambulizi dhidi ya mashirika ya Umoja wa Mataifa ambayo ni muhimu katika kufikisha misaada ya kibinadamu kwa watu wanaohitaji sana.

Wameonya kuwa “Uwezo wa mashirika ya kibinadamu kutoa msaada umekuwa mdogo baada ya kulazimishwa kufunga programu katika ofisi zilizoporwa au kuharibiwa na katika madeneo yenye mapigano, ikiwa ni pamoja na vituo vya hatua vya usalama vya wanawake na wasichana (WGSS), maeneo ya faragha, na hospitali”.

Changamoto kwa wahudumu wa misaada

Wataalam wameongeza kuwa “Tuna wasiwasi kwamba mashirika ya kibinadamu, mashirika ya kiraia na mashirika ya misaada yanapata ugumu kufanya kazi na kufikia maeneo yaliyoathiriwa na migogoro kutokana na kuingiliwa mara kwa mara. Tumepokea ripoti zinazoonyesha udhibiti wa makundi yenye silaha juu ya uhuru wa kutembea, ikiwa ni pamoja na mashirika ya misaada kusafiri na kufikia jamii zilizoathirika na vita”. 

Wameongeza kuwa “Tuna wasiwasi mkubwa juu ya kulenga watu walio katika hatari, hasa wanawake, watoto, wakimbizi na watu waliokimbia makazi yao, na kuongezeka kwa hatari za usafirishaji harabu wa binadamu kutokana na uhasama unaoendelea nchini Sudan. “

Wataalam hao wametaka hatua zichukuliwe “Tunatoa wito wa uwajibikaji na uchunguzi madhubuti wa ukiukaji wa haki za binadamu za kimataifa na sheria za kibinadamu, kama inavyotakiwa na sheria za kimataifa.”

Wataalamu hao pia wameelezea wasiwasi wao kuhusu athari za kufungwa kwa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan, dhidi ya hali ya kuendelea kwa ghasia na ukosefu wa usalama.

 Pia wamekuwa wakiwasiliana na mamlaka ya RSF na Sudan.



Post a Comment

0 Comments