Ticker

6/recent/ticker-posts

Pasaka ni nini?,Nawatakia pasaka njema, happy easter 2024



Pasaka ni nini?,Nawatakia pasaka njema, happy easter 2024

Asante sana kwa kuwa Mdau muhimu ndani ya @afyaclass, tunakuthamini na tunakutakia sikukuu njema ya Pasaka.

Pasaka ni sikukuu muhimu zaidi katika kalenda ya Kikristo, na huadhimishwa na maelfu ya watu duniani kote.

Inaashiria Yesu kufufuka kutoka kwa wafu, baada ya kufa msalabani.

Pasaka ni nini?

Je, Pasaka ni nini kibiblia?

Pasaka ni neno la Kiswahili ambalo limetokana na neno la kigiriki “pascha” ambalo tafsiri yake kwa lugha ya kiingereza ni “passover” kwa Kiswahili  ni “pita juu”. Hivyo pasaka kwa Kiswahili tunaweza kusema tafsiri yake ni “pita juu au vuka upite”.

Asili ya Neno hili ni siku ile wana wa Israeli walipokuwa wanatolewa kutoka Misri, usiku ule ambao ndio walikuwa wanatoka Misri, Bwana Mungu aliwaagiza wasitoke nyumba zao kwamba mpaka watakapomchinja yule Mwanakondoo na damu yake kuipaka katika miimo miwili ya Milango…ili wakati yule malaika ambaye alitumwa kuwaangamiza wazaliwa wa kwanza wote wa wanadamu na wanyama waliokuwepo katika Misri nzima..atakapopita katika kila nyuma na kuiona damu hiyo ya mwanakondoo kwenye miimo ya mlango basi hataingia katika nyumba hiyo kumharibu mzaliwa wa kwanza wa nyumba hiyo “ATAVUKA JUU, AU ATAPITA JUU” Kuendelea na nyumba nyingine…na atakapofika katika nyumba nyingine na kukuta damu juu ya miimo ya mlango kama nyumba ya kwanza vile vile ATAPITA JUU na kuendelea mpaka atakapokuta nyumba ambazo hazina damu hiyo, ndipo ataingia na kuangamiza.

Kutoka 12:12 “Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi Bwana.

13 Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo; nami nitakapoiona ile damu, NITAPITA JUU YENU, lisiwapate pigo lo lote likawaharibu, nitakapoipiga nchi ya Misri”.

Hivyo hicho kitendo cha kuvuka na KUPITA JUU ndicho kinachoitwa Passover, kwa kigiriki Pascha, kwa Kiswahili PASAKA.

pasaka ni nini

Sasa katika Agano jipya damu ya mwanakondoo yule ndio inayofanananishwa na damu ya Bwana wetu Yesu Kristo, Sisi tuliokuwa dhambini tulipotolewa dhambini(yaani Misri yetu) na tunapoelekea nchi yetu ya ahadi mbinguni…

Damu ya Yesu ndiyo iliyotuokoa la laana ya Mungu dhidi ya watu wote walio katika dhambi..Na damu ya Yesu ni ishara ya Agano kwamba kwa kupitia damu yake tunalindwa na hukumu ya Mungu..

Hukumu ya Mungu inapoachiliwa au itakapoachiliwa tutakuwa tumefunikwa chini ya damu ya Yesu na Malaika yule wa hukumu ATAPITA JUU YETU, na tutanusurika na hukumu ya Mungu.

Mungu wa Mbinguni akubariki sana

PASAKA NJEMA KWAKO..!!!!!



Post a Comment

0 Comments