Kaswende ni ugonjwa gani,
Kaswende ni maambukizi yanayosababishwa na bakteria. Mara nyingi, huenea kupitia mawasiliano ya kingono au kwa kujamiiana. Huu ni ugonjwa wa Zinaa.#Soma hapa Orodha mpya ya magonjwa ya Zonaa
Ugonjwa huu huanza kama kidonda ambacho mara nyingi hakina maumivu na kawaida huonekana kwenye sehemu za siri, puru au mdomo. Kaswende huenea kutoka kwa mtu hadi mtu kwa kugusana moja kwa moja na vidonda hivi. Pia inaweza kupitishwa kwa mtoto wakati wa ujauzito na kujifungua na wakati mwingine kwa njia ya kunyonyesha.
Baada ya maambukizo kutokea, bakteria wa kaswende wanaweza kukaa kwenye mwili kwa miaka mingi bila kusababisha dalili. Lakini maambukizi yanaweza kuwa hai tena. Bila matibabu, kaswende inaweza kuharibu moyo, ubongo au viungo vingine. Inaweza kuhatarisha maisha pia.
Ugonjwa wa Kaswende ukiwa kwenye hatua za mwanzo unaweza kuponywa, wakati mwingine kwa Sindano moja tu ya dawa inayoitwa penicillin.
Ndiyo maana ni muhimu kupata uchunguzi wa afya mara tu unapoona dalili zozote za kaswende. Wajawazito wote wanapaswa kupimwa kaswende katika uchunguzi wao wa kwanza wa ujauzito pia.
Dalili Za Ugonjwa wa Kaswende
Kaswende hukua kwa hatua, Na Dalili zake hutofautiana kwa kila hatua(Stages). Lakini hatua hizi zinaweza kuingiliana,na dalili zake zikawa hazina mpangilio uliosawa. Unaweza kuambukizwa na bakteria wa kaswende bila kugundua dalili zozote kwa miaka.
Soma Zaidi hapa kuhusu Dalili za Ugonjwa wa Kaswende kwenye Kila hatua(Stages);
Ugonjwa huu wa Kaswende huweza kusababisha Uharibufu wa;
- Ubongo
- Nerves
- Macho
- Moyo
- Mishipa ya Damu(Blood vessels).
- Ini
- Mifupa na joints.
Matatizo haya yanaweza kutokea miaka mingi baada ya maambukizi ya awali, ambayo hayajatibiwa.
Kaswende inayoenea
Katika hatua yoyote ile, na ambayo haijatibiwa inaweza kuathiri ubongo, uti wa mgongo, macho na sehemu nyingine za mwili. Hii inaweza kusababisha matatizo makubwa ya afya au hata kutishia maisha.
Kaswende ya kuzaliwa nayo(Congenital Syphilis)
Wajawazito walio na kaswende wanaweza kupitisha ugonjwa huo kwa watoto wao. Watoto ambao hawajazaliwa wanaweza kuambukizwa kupitia kiungo ambacho hutoa virutubisho na oksijeni ndani ya tumbo, kinachoitwa placenta. Maambukizi pia yanaweza kutokea wakati wa kuzaliwa.
Watoto wachanga walio na kaswende ya kuzaliwa wanaweza wasiwe na dalili. Lakini bila matibabu ya haraka, watoto wengine wanaweza kupata:
– Vidonda na upele kwenye ngozi.
– Homa.
– Ngozi na macho kubadilika rangi na kuwa manjano, hali inayoitwa kwa kitaalam jaundice
– Seli nyekundu za damu kuwa pungufu, kuwa na tatizo la upungufu wa damu au hali inayoitwa anemia.
– Kuvimba kwa wengu na ini.
– Kupiga chafya au kuwa na shida inayoitwa rhinitis.
– Mabadiliko ya mifupa.n.k
Dalili za baadaye zinaweza kujumuisha kuwa na shida ya ukiziwi, matatizo ya meno na pua, hali ambayo daraja la pua huanguka.n.k
Watoto walio na kaswende pia wanaweza kuzaliwa mapema sana. Wanaweza kufa wakiwa tumboni kabla ya kuzaliwa. Au wanaweza kufa baada ya kuzaliwa.
Chanzo cha Ugonjwa wa Kaswende
Chanzo cha kaswende ni bakteria aitwaye Treponema pallidum. Njia ya kawaida ya kaswende kuenea ni kwa kugusa kidonda cha mtu aliyeambukizwa wakati wa kujamiiana kwa uke, mdomo au Njia ya haja kubwa.
Bakteria huingia mwilini kupitia mikato,michubuko au mikwaruzo kwenye ngozi au kwenye utando wa ndani wenye unyevu wa baadhi ya sehemu za mwili.
Hatari ya kupata Kaswende
Hatari ya kupata kaswende ni kubwa ikiwa:
– Unafanya ngono bila kinga.
– Kufanya ngono na zaidi ya mpenzi mmoja.
– UnaIshi na VVU, virusi vinavyosababisha UKIMWI na haupo kwenye Tiba
– Uwezekano wa kupata kaswende pia ni mkubwa kwa wanaume wanaofanya mapenzi na wanaume.n.k
Matatizo/Madhara;
Bila matibabu, kaswende inaweza kusababisha uharibifu katika mwili wote. Kaswende pia huongeza hatari ya kuambukizwa VVU na inaweza kusababisha matatizo wakati wa ujauzito. Matibabu yanaweza kusaidia kuzuia uharibifu huu. Lakini hayawezi kurekebisha au kubadilisha uharibifu ambao tayari umetokea.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!