Ugonjwa wa zinaa pangusa,chanzo,dalili na Tiba
Pangusa ni miongoni mwa magonjwa ya Zinaa ambayo hutokea kwa jinsia zote mbili(mwanaume na mwanamke),
Ugonjwa huu husababishwa na bacteria wanaojulikana kama Haemophilus ducreyi(H.ducreyi).Na hutibiwa kwa dawa jamii ya antibiotics.
Dalili za Pangusa
Kwenye hatua za mwanzo,Maambukizi haya huweza kusababisha dalili chache, na unaweza hata kuzipuuzia maana sio kali, ndyo mana kuna umuhimu wa kufanya Screening mara kwa mara.
UGONJWA WA PANGUSA(,chanzo,dalili tiba)
Ugonjwa wa pangusa ni ugonjwa wa zinaa au ugonjwa unaoambukizwa kwa njia ya kufanya ngono, na ugonjwa huu kwa kitaam hujulikana kama chancroid.
CHANZO CHA UGONJWA WA PANGUSA
Ugonjwa wa pangusa husababishwa na vimelea mbali mbali vya magonjwa ikiwa ni pamoja na Backteria jamii ya Haemophilus ducreyi.
Bacteria hawa husambazwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya kujamiiana.
DALILI ZA UGONJWA WA PANGUSA NI PAMOJA NA;
– Mgonjwa huanza kuwa na viupele sehemu za siri ambavyo baadae huchubuka na kuwa vidonda
– Mgonjwa kupata maumivu makali kwenye vidonda hivi
– Mgonjwa kuhisi muwasho kwenye vidonda
– Vidonda hivi hutoa damu pale vinapoguswa au kubinywa
– Joto la mwili la mgonjwa kuwa juu au mgonjwa kuwa na homa
– Mgonjwa kukosa hamu ya kula chakula
– Na wakati mwingine mgonjwa kupata shida wakati wa kutembea
– kupata maumivu wakati wa kukojoa
– Kutokwa na uchafu(discharge) kwenye uume au Ukeni
– Kupata maumivu wakati wa tendo kwa wanawake
– Kutoa damu(blid) katikati ya period na baada ya tendo la ndoa
– Kupata maumivu kwenye korodani
– Kupata maumivu sehemu ya haja kubwa n.k
MAMBO YA KUEPUKA ILI KUJIKINGA NA UGONJWA HUU WA PANGUSA
– Epuka kufanya ngono zembe(mapenzi bila kinga au condom)
– Epuka tabia ya kuwa na wapenzi wengi
– Epuka tabia ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile
– Kamuone mtaalam wa afya baada ya kuhisi haupo sawa
MATIBABU YA UGONJWA WA PANGUSA
✓ Matibabu sahihi ya ugonjwa wa pangusa huhusisha matumizi ya dawa mbali mbali baada ya kuongea na wataalam wa afya na kujua chanzo halisi cha tatizo lako.
“KUMBUKA; Hakikisha unapata maelekezo kutokwa kwa Mtaalam wa afya kabla ya matumizi ya dawa yoyote,ili kuona ni tiba gani sahihi kulingana na hali yako
Je,chancroid inaweza kupona yenyewe?
Ikiwa una Pangusa au chancroid na hujatibiwa ukapona, vidonda au sores vinaweza kuisha vyenyewe ndani ya mwezi mmoja au miwili, Ingawa utakuwa kwenye hatari ya kupata tatizo lingine la suppurative lymphadenitis, Maambukizi kwenye Soft Tissues.”
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
Ugonjwa wa CHLAMYDIA,chanzo,dalili na Tiba yake
Chlamydia ni ugonjwa unaowapata watu wengi na unaenezwa kwa ngono,Hivo chlamydia ni miongoni mwa magonjwa ya Zinaa. Ni ugonjwa unaoshambulia jinsia zote na mara nyingi hauonyeshi dalili zozote. Dalili zikionekana, ni baada ya wiki kadhaa kutoka siku ya mambukizi.
#SOMA hapa Lists Mpya ya Magonjwa ya Zinaa kwa Sasa
Chanzo cha Ugonjwa wa Chlamydia
Chlamydia husababishwa na kuenezwa na bakteria aitwaye Chlamydia trachomatis. Bakteria huyu hupatikana kwenye shingo ya kizazi (cervix), mrija wa mkojo, uke na/au sehem ya haja kubwa.. Bakteria pia huishi ndani ya koo. Namna yo yote ya kujamiiana inaweza kumweneza bakteria huyu.
Bakteria wa Chlamydia trachomatis mara nyingi huenezwa kupitia kufanya mapenzi kwa njia ya uke, mdomo na haja kubwa(vaginal, oral and anal sex),
Pia inawezekana, kwa bakteria hawa kuenea kipindi cha ujauzito, wakati wa kuzaa mtoto n.k. Ugonjwa wa chlamydia unaweza kusababisha nimonia au maambukizi makubwa ya macho kwa mtoto mchanga.
Vitu ambavyo huongeza hatari ya kupata Ugonjwa wa Chlamydia
Tafiti zinaonyesha:Watu ambao huanza kufanya mapenzi kabla ya umri wa miaka 25 wapo kwenye hatari kubwa Zaidi ya kupata ugonjwa wa chlamydia kuliko wenye umri mkubwa Zaidi.
Vitu hivi huongeza hatari Zaidi ya kupata Ugonjwa wa Chlamydia;
– Kutokutumia kinga kama Condomu wakati wa tendo
– Matumizi yasio sahihi ya Condomu wakati wa Tendo,
#Soma hapa Matumizi Sahihi ya Condomu
– Kuwa na mpenzi mpya ambaye hujui hali yake au kuwa na wapenzi wengi
– Kutokufanya vipimo mara kwa mara
– Kutokujikinga na magonjwa ya Zinaa au kutokutibu magonjwa ya Zinaa n.k
Dalili za Chlamydia;
Katika hatua za awali maambukizi ya Chlamydia trachomatis huweza kusababisha dalili chache Zaidi na ambazo sio kali, hali ambayo hufanya baadhi ya watu kutokugundua mapema kwamba tayari wana maambukizi haya.
Hii ndyo maana,kufanya screening mara kwa mara ni muhimu Zaidi ili kukuweka Salama mapema Zaidi.
Dalili za maambukizi ya Chlamydia trachomatis ni pamoja na:
- Kupata maumivu wakati wa kukojoa
- Kutokwa na Uchafu ukeni
- Kutokwa na Uchafu kwenye Uume
- Kupata maumivu ukeni wakati wa tendo
- Kuvuja damu ukeni katikati ya mzunguko wa hedhi
- Kuvuja damu ukeni baada ya tendo
- Kupata maumivu ya Korodani n.k
DALILI ZA CHLAMYDIA
Dalili za chlamydia zinaweza kuwa:
. Maumivu ya sehemu ya chini ya tumbo
. Maumivu wakati wa kukojoa
. Maumivu wakati wa tendo la ndoa
. Maumivu ya nyonga
. Usaha au uchafu kutoka kwenye uume
. Kutoka damu kwenye mkundu
. Uchafu kutoka kwenye mkundu
. Maumivu kwenye mkundu
. Maumivu kwenye korodani
. Kukojoa mara kwa mara
. Uchafu kutoka ukeni
. Maumivu ukeni
. Kutokwa damu katikati ya hedhi na baada ya tendo la ndoa kwa wanawake
Madhara ya Ugonjwa wa Chlamydia(Complications)
Maambukizi ya Chlamydia trachomatis huweza kuhusishwa na:
• Kupata tatizo la maambukizi ya bacteria kwenye via vya uzazi vya Mwanamke yaani Pelvic inflammatory disease(PID).
• Kupata maambukizi karibu na Korodani.
Maambukizi ya klamidia yanaweza kuleta athari kwenye mirija iliyojikunja iliyo karibu na kila korodani, inayoitwa epididymis. Maambukizi haya yanaweza kusababisha homa, maumivu ya scrotal na uvimbe.
• Maambukizi kwenye Tezi Dume(Prostate gland infection).
Mara chache, bakteria wa chlamydia wanaweza kuenea kwenye tezi ya prostate na kusababisha tatizo la kuvimba kwa tezi hili yaani Prostatitis,Hii inaweza kusababisha maumivu wakati au baada ya kufanya Mapenzi, homa,kuhisi baridi, maumivu wakati wa kukojoa, na maumivu sehemu ya chini ya mgongo au maumivu ya kiuno.
• Maambukizi kwa Mtoto mchanga.
Maambukizi ya klamidia yanaweza kupita kutoka kwenye mfereji wa uke hadi kwa mtoto wako wakati wa kujifungua, na kusababisha nimonia au maambukizi makubwa ya macho.
• Tatizo la mimba kutunga nje ya kizazi(Ectopic pregnancy).
Hii hutokea wakati yai lililorutubishwa hupandikizwa na kukua nje ya uterasi, kwa kawaida kwenye mrija wa fallopian. Yai hili linahitaji kuondolewa ili kuzuia matatizo ya kutishia maisha, kama vile kupasuka kwa mrija wa fallopian n.k. Maambukizi ya chlamydia huongeza hatari hii.
• Tatizo la Mwanamke kushindwa kubeba mimba(Infertility).
Maambukizi ya Klamidia yanaweza kusababisha kovu na kuziba kwa mirija ya uzazi, jambo ambalo linaweza kusababisha utasa.
• Kupata tatizo la Reactive arthritis.
Watu wenye maambukizi ya Chlamydia trachomatis wapo kwenye hatari Zaidi ya kupata tatizo la reactive arthritis, au pia hujulikana kama Reiter syndrome.
Hii ni hali ambayo huathiri mifupa,macho au urethra — mrija unaosafirisha mkojo kutoka kwenye kibofu hadi nje ya mwili wako.
Hayo ndiyo baadhi ya madhara yanayotokana na Ugonjwa wa Chlamydia, Ikiwa una tatizo hili hakikisha unapata Tiba mapema au;
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!