Mjamzito kuumwa tumbo,chanzo chake hiki hapa

Mjamzito kuumwa tumbo,chanzo chake hiki hapa

Chanzo cha Mjamzito kuumwa tumbo

Mjamzito kuumwa tumbo ni tatizo ambalo huwapata wanawake wengi pindi wakiwa wajawazito, tatizo hili hujulikana kama Stomach (abdominal) pains or cramps na ni kawaida kutokea hivi.

Sio tatizo ambalo ni la kukupa wasiwasi sana,Ingawa wakati mwingine hii ni Ishara mbaya, hivo huhitaji uchunguzi Zaidi.(Soma hapa Dalili za hatari kwa mama mjamzito)

Sio kitu cha kuwa na wasiwasi ikiwa maumivu ni kidogo na yanaondoka unapobadilisha mkao, kupumzika, kujisaidia au kupitisha upepo. Lakini ikiwa una maumivu ya tumbo na una wasiwasi, hakikisha unaongea na Wataalam wa afya kwanza, au tuwasiliane hapa ndani ya @afyaclass

Mjamzito kuumwa tumbo ambako sio kwa kutilia Mashaka hutokana na;

  • Maumivu yanayojulikana kama ligament pain au “growing pains” haya ni maumivu unayoyapata wakati ligaments zinapojivuta ili kusupport ujauzito unaokua, Hii huweza kusababisha ujisikie maumivu(sharp cramp) hasa upande mmoja wa chini ya tumbo
  • Maumivu ya tumbo kwa Sababu ya shida ya kukosa choo au kupata choo kigumu(Constipation)– ambako hii ni kawaida kutokea kwa mjamzito. Soma hapa jinsi ya kudhibiti hali hii
  • Pamoja na Sababu zingine…!!!!

Dalili za hatari kwa mjamzito

Hakikisha Unapata Msaada wa Haraka ikiwa ni Mjamzito halafu unapata Maumivu ya Tumbo yanayoambatana na vitu hivi;

– Kuvuja Damu Ukeni

– Kupata maumivu ya tumbo yanayoambatana na tumbo kukaza sana mara kwa mara(regular cramping or tightenings)

– Kutokwa na Uchafu Ukeni ambao siokawaida(wenye harufu mbaya, rangi ya njano n.k)

– Kupata maumivu makali chini ya mgongo(lower back pain)

– Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa au kuhisi hali ya kuungua wakati wa kukojoa

– Kupata maumivu makali ya tumbo na ambayo hayaishi hata baada ya kupumzika kwa zaidi ya dakika  30 mpaka 60 n.k

Yoyote kati ya hizi inaweza kuwa dalili za kitu ambacho kinahitaji kuchunguzwa au kutibiwa haraka(dalili ya hatari).

Chanzo cha Maumivu ya Tumbo ambayo ni Hatari

Baadhi ya  hali hizi huweza kuwa chanzo cha Maumivu makali ya tumbo ambayo yanahitaji msaada wa haraka;

1. Tatizo la Mimba kutunga nje ya Kizazi(Ectopic pregnancy)

Huu ndio wakati yai lililorutubishwa hupandikizwa nje ya tumbo la uzazi, kwa mfano kwenye mrija wa fallopian. Mimba haiwezi kuishi na inahitaji kuondolewa kwa dawa au upasuaji.

Dalili kawaida huonekana kati ya wiki 4 na 12 za ujauzito na zinaweza kujumuisha:

  • maumivu ya tumbo na kutokwa na damu
  • maumivu katika ncha ya bega lako
  • usumbufu wakati wa kukojoa au kujisaidia haja kubwa n.k

Pata maelezo zaidi kuhusu mimba kutunga nje ya kizazi ectopic pregnancy hapa.

2. Tatizo la Mimba kutoka(Miscarriage)

Kupata maumivu makali ya tumbo yanayoambatana na hali ya tumbo kuvuta(Cramping pains) pamoja na kuvuja damu ukeni kabla ujauzito haujafika wiki 24 au 28,

Hii ni dalili kubwa ya mimba kutoka au kutishia kutoka(Sign of miscarriage or threatened miscarriage).

3. Tatizo la Kifafa cha Mimba(Pre-eclampsia)

Maumivu chini ya mbavu ni ya kawaida katika ujauzito wa baadaye kutokana na mtoto anayekua na uterasi kusukuma chini ya mbavu.

Lakini ikiwa maumivu haya ni mabaya/makali au ya kudumu, hasa upande wa kulia, inaweza kuwa ishara ya pre-eclampsia (shinikizo la damu wakati wa ujauzito au kifafa cha mimba) ambayo huwapata baadhi ya wajawazito. Kawaida huanza baada ya wiki 20 au tu baada ya mtoto kuzaliwa.

Dalili zingine za preeclampsia ni pamoja na:

  • maumivu ya kichwa kali
  • matatizo ya kuona marue rue au kutokuona vizuri
  • kuvimba sana miguu, mikono na uso n.k

Pata maelezo zaidi kuhusu pre-eclampsia

4. Uchungu wa mapema(Premature labour)

Iwapo una mimba ya chini ya wiki 37 na unakuwa na mikazo ya mara kwa mara ya tumbo au kubanwa pamoja na tumbo kuuma sana, wasaliana na wataalam wa afya mapema.

Hii inaweza kuwa ishara ya leba ya mapema, na utahitaji kufuatiliwa hospitalini.

5. Kupata tatizo la Placental abruption

Huu ndio wakati placenta inapoanza kutoka kwenye ukuta wa tumbo la uzazi, kwa kawaida husababisha kutokwa na damu na maumivu makali ya mara kwa mara ambayo hayaji na kuondoka kama maumivu ya kubana kwa tumbo.

Wakati mwingine ni dharura kwa sababu ina maana kwamba kondo la nyuma linaweza kukosa kumudu mtoto wako ipasavyo.

Unapaswa kwenda hospitali ili wewe na mtoto wako mchunguzwe.

Pata maelezo zaidi kuhusu tatizo la Placental abruption

6. UTI (maambukizi ya njia ya mkojo)

UTI ni ya kawaida wakati wa ujauzito na inaweza kutibiwa kwa urahisi.

Maambukizi haya ya njia ya Mkojo yanaweza kusababisha maumivu ya tumbo wakati mwingine, lakini si mara zote, unaweza kupata maumivu wakati wa kukojoa n.k

Pata maelezo zaidi kuhusu tatizo la UTI.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!