Ticker

6/recent/ticker-posts

Tatizo la ngozi kukauka na kukakamaa,chanzo,Na tiba



Tatizo la ngozi kukauka na kukakamaa,chanzo,Na tiba

Ngozi kukauka;

Ngozi kukauka kwa jia jingine la kitaalam hufahamika kama xerosis kyutizi mara nyingi husababishwa na sababu za kawaida kama vile hali ya hewa ya umoto au baridi, kuloweka ngozi kwenye maji ya moto na kukosekana kwa unyevu kwenye ngozi.

Visababishi hivi vinavyojulikana huweza kutibika kwa njia ambazo mtu anaweza kuzifanya nyumbani. Hata hivyo baadhi ya watu hupata tatizo kubwa linaloogopesha na kufanya waende hospitali kuonana na daktari wa ngozi.

Ngozi kukauka huambatana pia na kupasuka kwa ngozi, kupata magamba, kupata ramani na miwasho haswa katika maeneo ya viganja vya mikono, mikono na miguuni

Visababishi vya Ngozi kukauka

Zipo hali na magonjwa mbalimbali yanayoweza kupelekea ngozi kukauka, katika sehemu hii utajifunza sababu zinazosababisha kwa kiasi kikubwa.

1. Kuwa na magonjwa ya ngozi kama demataitizi, kontakti demataitizi, pumu ya ngozi, soriasisi

2. Kukaa kwenye hali ya hewa yenye unyevu kidogo

3. Hali ya hewa ya ujoto, kuishi mazingira yenye joto kali

4. Kuoga maji ya moto na kwa muda mrefu au mara kwa mara

5. Matumizi ya sabuni na kemikali zinazokausha ngozi n.k

Dalili za Ngozi kukauka

Dalili hutegemea kisababishi na umri wako, unaweza kupata dalili zifuatazo;

– Kuhisi ngozi kuvuta mara baada ya kuoga au kuogelea

– Ngozi kuwa nyekundu

– Ngozi kuwa na rangi ya majivu

– Kupasuka kwa ngozi au kuwana michirizi

– Kuwasha kwa ngozi

– Kuhisi na kuona ngozi imekunjamana

– Kubabuka kwa ngozi

– Kutokwa na damu kwenye ngozi haswa kwenye michirizi ilozama zaidi

Ni wakati gani wa kumwona daktari?

Mwone daktari endapo:

• Ngozi haijirudii kwenye hali yake ya awali licha ya kufanya juhudi za kujitibu mwenyewe

• Ngozi inabadilika kuwa na rangi nyekundu

• Unakosa usingizi

• Unavidonda kwenye ngozi iliyokauka vitokanavyo na kujikuna au maambukizi

• Ngozi imekauka au kukunjamana katika eneo kubwa la mwili

Vihatarishi vya Ngozi kukauka

Mtu mwenye ngozi yenye mafuta au mwenye ngozi kavu asilia wote wanaweza kukumbwa na tatizo hili la ngozi kukauka na kupasuka. Vihatarishi vingine ni;

  • Umri mkubwa na kuzeeka. Umri zaidi ya miaka 40
  • Kutumia maji yenye chlorine kuoga mara kwa mara
  • Kufanya kazi zinazohusika kuzamisha mwili wako kwenye maji
  • Kuosha ngozi na vimiminika vya moto na mara kwa mara
  • Historia ya kuwa na magonjwa ya ngozi kama demataitizi
  • Hali ya hewa, kipindi cha baridi na joto ambapo hali ya hewa inakosa unyevu wa kutosha

Matibabu ya nyumbani kwa tatizo la Ngozi kukauka

Badili mtindo wa maisha kwa kufanya mambo yafuatayo;

✓ Kunywa maji ya kutosha

✓ Chagua kilainisha ngozi kizuri. Mafuta ya Vaseline yasiyo na pafyumu ni mazuri zaidi

✓ Usioge kwa kutumia maji ya moto

✓ Usioge kila siku

✓ Usioge zaidi ya dakika 10 kwa siku

✓ Tumia sabuni za kuongeza unyevu kwenye ngozi unapooga

✓ Paka mafuta ya kuleta unyevu wkenye ngozi mara unapomaliza kuoga

✓ Usifanye scrubu/kusababisha miwasho kwenye maeneo ngozi imekauka

✓ Endapo ni msimu wa masika au baridi, tumia mashine za kuongeza unyevu kwenye hewa kama ukiweza

Kinga ya tatizo la Ngozi kukauka

Kujikinga fanya mambo yaliyotajwa kwenye matibabu ya nyumbani pamoja na;

  • Kuvaa glavu wakati unashika majimaji endapo unahatari ya kukauka mikono
  • Jifunike jinsi uwezavyo kwenye msimu wa baridi

Madhara ya Ngozi kukauka

Madhara ya tatizo la ngozi kukauka ni pamoja na;

– Kupelekea Kuamka kwa pumu ya ngozi

– Kubanduka kwa ngozi

– Kupata maambukizi kwenye ngozi haswa kwenye maeneo ambayo yamepasuka n.k

NB: wasiliana na Wataalam wa afya kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

AU KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



Post a Comment

0 Comments