Ticker

6/recent/ticker-posts

Gangrene ni ugonjwa gani,au gangrene ni nini?



Gangrene ni ugonjwa gani,au gangrene ni nini?

Gangrene ni tatizo linalohusisha  kufa kwa tissu za mwili kutokana na kupungua kwa mtiririko wa damu au maambukizi makali.

Mara nyingi tatizo la gangrene huathiri mikono na miguu, ikiwa ni pamoja na vidole vya mikono na vidole vya miguu. Inaweza pia kutokea katika misuli na viungo vya ndani ya mwili, kama vile kwenye kifuko cha nyongo(gallbladder).

Hali yoyote inasababisha uharibifu wa mishipa ya damu, na kuathiri mtiririko wa damu(Blood flow),mfano ugonjwa wa kisukari, tatizo la mishipa ya arteries kuwa migumu”hardened arteries (atherosclerosis),n.k, vyote hivi huongeza hatari ya mtu kupata tatizo la gangrene.

gangrene ni tatizo ambalo linawapata Sana wagonjwa wa kisukari, husababisha sehemu ya mwili kubadilika rangi na tissues za sehemu hiyo kufa kutokana na mzunguko wa damu kutokufika sehemu hiyo,

Tatizo hili husambaa kwa haraka kwenye viungo vya mwili na lisipo tibiwa kwa haraka hupelekea mgonjwa kukatwa viungo na muda mwingine kusababisha kifo,

Tatizo hili linatibika katika hatua za awali hivyo ukimuona mgonjwa wa kisukari kaanza kuonesha dalili hizi wahi mapema hospital ili umsaidie kupata suluhisho.

Matibabu ya gangrene yanaweza kujumuisha dawa jamii ya antibiotics, tiba ya oksijeni, na upasuaji wa kurejesha mtiririko wa damu na kuondoa tishu zilizokufa. Gangrene ikitambuliwa mapema na kutibiwa, ndivyo uwezekano wa kupona huongezeka.

Dalili za tatizo la Gangrene

Ikiwa gangrene imeathiri ngozi,dalili zake ni pamoja na:

  1. Ngozi kubadilika rangi-kuanzia kijivu iliyokolea hadi bluu, zambarau, nyeusi, shaba au nyekundu
  2. Kuvimba eneo husika
  3. Kuwa na kama malengelenge
  4. Ghafla, kuanza kupata maumivu makali ikifuatiwa na kuhisi kufa ganzi
  5. Kutokwa na Uchafu wenye harufu mbaya kwenye kidonda
  6. Ngozi kuwa nyembamba, inayong’aa, au ngozi isiyo na nywele
  7. Kuhisi baridi kwenye Ngozi au baridi kwa kugusa
  8. Iwapo gangrene itaathiri tishu zilizopo chini ya ngozi yako, unaweza pia kuwa na homa ya kiwango cha chini na kwa ujumla kujisikia vibaya.

Gangrene kutokana na maambukizi makali, Ikiwa vijidudu vilivyosababisha gangrene vitaenea kupitia mwili, hali inayoitwa septic shock inaweza kutokea. Ishara na dalili za septic shock zinazoweza kutokea ni pamoja na:

– Kushuka kwa shinikizo la Damu(Low blood pressure)

– Kupata homa

– Mapigo ya moyo kwenda mbio

– Hali ya kukosa pumzi au kupumua kwa shida n.k

Chanzo cha tatizo la Gangrene

Sababu za kutokea kwa Gangrene ni pamoja na;

– Ukosefu wa usambazaji wa damu(Lack of blood supply)

Damu hubeba oksijeni na virutubisho kwenye mwili. Pia hutoa mfumo wa kinga na antibodies kupambana na maambukizi. Bila ugavi sahihi wa damu, seli haziwezi kuishi, na tishu hufa.

– Maambukizi ya magonjwa

Maambukizi ya vimelea kama bacteria ikiwa hayajatibiwa huweza kupelekea kupata tatizo la gangrene.

– Kuumia au kupata majeraha(Traumatic injury).

Majeraha ya risasi au majeraha ya kusagwa kutokana na ajali za gari n.k yanaweza kusababisha majeraha wazi ambayo huruhusu bakteria kuingia kwenye mwili. Ikiwa bakteria huambukiza tishu na kubaki bila kutibiwa, gangrene inaweza kutokea.

Vitu ambavyo huongeza hatari ya kupata Gangrene

  • Ugonjwa wa kisukari; Viwango vya juu vya sukari kwenye damu vinaweza hatimaye kuharibu mishipa ya damu. Uharibifu wa mishipa ya damu unaweza kupunguza au kuzuia mtiririko wa damu kwenye sehemu ya mwili ikiwemo kwenye tishu, na hii huweza kupelekea kutokea kwa gangrene.
  • Ugonjwa kwenye mishipa ya damu kama vile;(atherosclerosis),damu kuganda n.k
  • Kuumia sana au kupata majeraha
  • Upasuaji
  • Uvutaji wa Sigara
  • Unene kupita kiasi au Uzito mkubwa kupita kiasi
  • Kuwa na hali yoyote inayoshusha kinga ya mwili(Immunosuppression) kama vile;, huduma ya Chemotherapy, mionzi,baadhi ya maambukizi kama vile ya UKIMWI n.k

Madhara ya Gangrene:

Tatizo la gangrene linaweza kusababisha matatizo makubwa ikiwa hautatibiwa mara moja. Bakteria wanaweza kuenea haraka kwenye tishu na viungo vingine. Huenda ukahitaji kuondolewa sehemu ya mwili (kukatwa) ili kuokoa maisha yako.

Kuondolewa kwa tishu zilizoambukizwa kunaweza kusababisha kovu au hitaji la upasuaji wa kurekebisha.

Jinsi ya kuzuia au kujikinga na tatizo la Gangrene

Hapa kuna njia chache za kusaidia kupunguza hatari ya kupata tatizo la gangrene:

✓ Hakikisha unadhibiti Sukari yako

✓ Kama una maambukizi yoyote, hakikisha unapata tiba

✓ Kama una Jeraha au kidonda, hakikisha unapata matibabu na kupona haraka

✓ Dhibiti Uzito wako wa Mwili

✓ Epuka kuvuta Sigara au kutumia tumbaku n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



Post a Comment

0 Comments