Chanzo cha mdudu kwenye kidole
UGONJWA WA MDUDU KWENYE KIDOLE(paronychia)
Mdudu kwenye kidole ndilo jina lilizozoeleka sana kwetu ila kwa kitaalam hujulikana kama Paronychia,
Ugonjwa huu wa Mdudu kwenye kidole huhusisha maambukizi ya vimelea kama vile bacteria na fangasi.
Na vimelea hawa huweza kupenya kwa njia mbali mbali ikiwemo michubuko,vidonda au mpasuko wa ngozi karibu na kucha.
Kulingana na Tafiti mbali mbali; Zinaonyesha Ugonjwa huu wa Mdudu kwenye kidole huwapata sana watu wanaofanya kazi kwenye mazingira ya kushika maji sana mara kwa mara au watu ambao ni rahisi kuwa katika mazingira yenye kemikali za vitu mbali mbali kama madawa ya shambani,viwandani n.k
Chanzo cha mdudu kwenye kidole
Ugonjwa wa Mdudu kwenye kidole unaweza kutokea wakati vimelea vya magonjwa kama vile bakteria au Fangasi vinapoingia kwenye ngozi kuzunguka kucha, inaweza kuwa ngozi iliyopasuka karibu na cuticle pamoja na eneo la mkunjo wa kucha au nail fold, na kusababisha maambukizi,
Jamii ya Bacteria ambao husababisha tatizo hili kwa kiasi kikubwa hujulikana kama Staphylococcus aureus na wengine ni Streptococcus pyogenes bacteria.
Lakini pia tabia kama vile; Mtu kung'ata kucha mara kwa mara huongeza uwezekano wa kutokea kwa tatizo hili, hii ni kwa sababu kung'ata kucha huweza kusababisha ngozi ya kwenye kucha au karibu sana na kucha kutengeneza uwazi,mchubuko au vitundu ambavyo itakuwa rahisi sana kwa vimelea vya magonjwa kama vile Bacteria au fangasi kupenya kwa urahisi zaidi,Tatizo hili huweza kumpata mtu wa umri wowote na linatibika kabsa.
Pia hali hii huweza kujitokeza kwa watu wenye tatizo la;
- kucha kuingia ndani ya kidole yaani Ingrown nails
- Irritation kutoka kwenye maji au chemicals
- Kuumia eneo la nailbed or cuticle area
- Pia tafiti zinaonyesha Matumizi ya baadhi ya Dawa huongeza hatari ya tatizo hili,dawa hizo ni pamoja na retinoids, baadhi ya anti-cancer medications, baadhi ya antibiotics.n.k
Watu ambao wapo kwenye hatari ya kupata Ugonjwa wa Mdudu kwenye kidole
Ingawa kila Mtu anaweza kupata,tafiti zinaonyesha makundi haya ya watu wapo kwenye hatari zaidi ya Kupata Ugonjwa wa Mdudu kwenye Kidole;
- Watu wanaofanya kazi Viwandani, au kazi za kushika makemikali mara kwa mara
- Wenye Tabia ya kung'ata kucha kwa meno au kutoa ngozi ya pembeni ya kucha kwa meno
- Wajenzi
- Wakulima
- Wenye baadhi ya magonjwa ya ngozi
- Wanaofanya kazi za kushika maji mara kwa mara,Mfano housegirl,houseboy n.k
Dalili za Ugonjwa wa Mdudu kwenye Kidole
Dalili za Mdudu kwenye kidole kawaida hutokea kwa masaa au siku kadhaa. Wakati mwingine huchukua muda mrefu kujitokeza. Dalili huonekana mahali ambapo kucha hukutana na ngozi, na Dalili hizo ni pamoja na;
1. Kupata maumivu kuzunguka eneo la kucha
2. Kuvimba eneo la kuzunguka kucha au kuvimba kidole
3. Ngozi ya eneo lilioathiriwa kubadilika rangi na kuwa nyekundu
4. Kuonekana kwa Usaha kujaa ndani ya ngozi karibu na kucha
5. Kucha kuwa ngumu kuliko kawaida
6. Kucha kuanza kutoka(kwa baadhi ya watu)
7. Kucha kuanza kujitenga kutoka kwenye sehemu yake yaani nailbed n.k
Jinsi ya Kuutambua Ugonjwa wa Mdudu kwenye kidole(paronychia)
Kwanza kabsa ni kupitia Dalili na Ishara zitakazojionyesha kwa Mgonjwa, kama tulivyokwisha kueleza,
Mtoa huduma wako atakuuliza kuhusu dalili ulizonazo na kukufanyia uchunguzi Zaidi, Kwa kawaida Wahudumu wa afya hawahitaji kuagiza vipimo ili kugundua maambukizi haya ya kucha. Ingawa watoa huduma wanaweza kuchukua sampuli ya tishu na kuituma kwenye maabara ili kupima sababu mahususi za Maambukizi haya, kama ni bakteria au fangasi.
Mara chache, ikiwa maambukizi ni makali, kipimo kama X-ray kinaweza kuagizwa ili kuangalia ikiwa mfupa wa chini umehusishwa pia.
Matibabu Ya Ugonjwa Wa Mdudu Kwenye Kidole
Matibabu ya tatizo hili hutegemea na ukubwa wa tatizo, je ni la muda mrefu au muda mfupi n.k, Yaani ni acute or chronic,
Je,Unasumbuliwa na tatizo hili na bado hujapata Tiba?
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.