Magonjwa
VIHATARISHI VYA SARATANI YA UTUMBO MPANA
NYAMA YASABABISHA SARATANI YA UTUMBO MPANA.
Saratani ya utumbo mpana ni miongoni mwa saratani zinazosababisha vifo vya watu wengi. Na saratani hii hutokana na kugawanyika au kuongezeka kwa seli katika utumbo mpana kusikokuwa na mpangilio.
Saratani hii inaonekana kuwa juu katika nchi au jamii ambazo zinafatisha mfumo wa maisha wa nchi za mataifa ya magharibi.
VIHATARISHI VYA SARATANI YA UTUMBO MPANA
1. kuwa na shida ya uzito uliopitiliza
2. mfumo wa maisha wa kutokufanya mazoezi
3. ulaji nyama nyekundu
4. unywaji pombe kupita kiasi
5. uvutaji wa tumbaku/sigara
6. kuwepo/kuota kwa vinyama/tishu katika kuta za ndani za utumbo mpana
7. umri mkubwa
8. magonjwa yanayohusisha inflamesheni ya utumbo
9. ulaji hafifu wa matunda na mbogamboga
10. kuongezeka kwa kiwango cha wadudu wasio rafiki katika utumbo.
11. kuondolewa kwa mfuko wa nyongo
JE NI ZIPI DALILI ZA TATIZO HILI
1. kutokwa na damu katika njia ya haja kubwa.
2. uvimbe tumboni.
3. maumivu ya tumbo
4. mabadiliko katika tabia ya haja kubwa
5. kupungua uzito kusiko na sababu
6. upungufu wa damu
7. kukosa hamu ya kula
Iwapo saratani hii itagundulika mapema basi matibabu yake huwa na matokeo mazuri na iwapo itachelewa basi matokeo yako si mazuri.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.