Kujisaidia Choo chenye Makamasi,chanzo,dalili na Tiba
Je,unashangaa wakati wa kujisaidia unaona choo chako kimechanganyika na vitu kama Makamasi?, Sababu ya hili ni nini?
Sehemu nyingi za mwili wako hutengeneza kamasi au Mucus, ikiwemo kwenye Utumbo. Hii Inaweka njia yako ya utumbo katika hali nzuri, na kuunda safu ya kinga dhidi ya bakteria. Pia husaidia taka kupita vizuri kwenye Utumbo mpana. Baadhi ya Kamasi huweza kushikamana na kinyesi wakati kinatoka kwenye mwili wako, Je hili ni tatizo au kawaida? Soma Zaidi hapa….
Chanzo cha Kujisaidia Choo chenye Makamasi
Matatizo tofauti ya usagaji chakula yanaweza kufanya kamasi zaidi kuonekana kwenye kinyesi chako. Wakati mwingine ni dalili mbaya na ambayo huweza kudumu kwa muda mrefu. Ila kuna wakati Makamasi haya huweza kujisafisha haraka. Matatizo ambayo yanaweza kusababisha kamasi kwenye Kinyesi chako ni pamoja na;
Ugonjwa wa Amoebiasis au wengi husema amoeba,#Soma Zaidi hapa dalili Zake
Moja ya Dalili kubwa ya Ugonjwa huu ni Mtu kujisaidia kinyesi chenye Vitu kama Kamasi au Makamasi.
Tatizo La Irritable Bowel Syndrome (Ibs)
Takriban nusu ya watu ambao wana tatizo la IBS hupata shida ya kuharisha na Pia huripoti kwamba wana kamasi kwenye kinyesi chao. Ute huo unaweza kuwa mweupe. Baadhi ya tafiti zinasema kwamba unaweza kuwa na uwezekano mkubwa wa kuwa na kamasi kwenye kinyesi kama una tatizo la IBS ikiwa pia una huzuni au una wasiwasi.
Crohn’s disease
Ugonjwa huu wa uvimbe wa tumbo (IBD) husababisha njia yako ya usagaji chakula kuvimba na kuwashwa. Kuharisha na kutokwa na damu kwenye njia ya haja kubwa au rectum ni dalili za kawaida. Wakati ugonjwa unapoanza, unaweza kuona damu au kamasi kwenye kinyesi chako. Kuharisha damu, mara nyingi hufuatana na kamasi au usaha;
Ulcerative colitis (UC)
Tatizo hili pia huhusisha hali ya Vidonda kwenye Utumbo pamoja na kuvimba, Hii huweza kusababisha kuvuja damu na kutengeneza Usaha au Makasi ambayo huweza kutoka kwa njia ya haja Kubwa.
Tatizo la kuvimba kwa Rectum au Proctitis
Hili ni tatizo ambalo huhusisha kuvimba kwa sehemu ya chini ya Utumbo Mkubwa inayojulikana kama rectum, Matokeo yake ni kupata maumivu makali ya Rectum, au njia ya haja kubwa,kutokwa na damu au Makamasi kwenye kinyesi n.k
Magonjwa ya Zinaa kama vile Kisonono au chlamydia, Magonjwa ya chakula au foodborne illnesses kama salmonella, huduma ya mionzi au radiation therapy, huweza kuchangia tatizo hili la proctitis.
Maambukizi ya bacteria,C. difficile (C. diff )
Pia maambukizi ya bacteria hawa huweza kusababisha Mtu kuharisha sana, na hata wakati mwingine kujisaidia kinyesi chenye Makamasi.
Bacteria wengine ambao huweza kusababisha shida hii ni pamoja na campylobacter.
Sumu kwenye Vyakula au Food poisoning
Aina fulani za viini huwa kama sumu kwenye chakula, mfano ni kama vile salmonella na shigella, ambapo huweza kusababisha kupata tatizo la kuharisha choo chenye kamasi au damu, pamoja na dalili zingine kama vile tumbo kuuma, homa, na kutapika.n.k
Maambukizi ya Parasite,Parasitic infections
Vimelea, ambavyo ni viumbe vidogo jamii ya Parasites, wakati mwingine kama minyoo, vinaweza kusababisha maambukizi katika njia yako ya utumbo. Aina kuu mbili za vimelea vinavyoweza kuambukiza mfumo wako wa usagaji chakula huitwa protozoa na helminths.
Vimelea hivi vinaweza kusababisha tatizo la kuharisha damu, ambapo huweza kuambatana na kamasi, pamoja na kichefuchefu, kutapika, homa, tumbo kuuma, na kupoteza uzito.
Saratani ya Utumbo Mpana,Colorectal cancer
Asilimia kubwa,Saratani ya utumbo mpana(colorectal cancer),ambayo hujulikana kama adenocarcinoma, huanzia kwenye mucosa, ambapo hapa ndyo penye Seli hai zinazotengeneza Kamasi.
Kuwa na Fistula aina ya Anal fistulas au Vidonda njia ya haja kubwa, rectal ulcers
Fistula ya Njia ya haja kubwa(Anal fistula) hutengeneza tundu lenye maambukizi kati ya ngozi na njia ya haja kubwa. Tatizo hili huweza kuundwa baada ya kuwa na jipu. Ni matatizo yanayoweza kusababishwa na IBD, na pia yanaweza kusababishwa na magonjwa ya zinaa sehemu ya haja kubwa, jeraha, ugonjwa wa kifua kikuu, na tiba ya mionzi kuzunguka pelvisi yako.
Tatizo hili la Fistula Wakati mwingine huweza kusababisha kamasi, pamoja na Usaha na damu, kutoka Sehemu ya haja kubwa.
Vidonda kwenye Puru au Rectum, vinavyosababishwa na jeraha kwenye ukuta wa puru yako, ni vidonda vilivyo wazi ndani ya puru yako ambavyo vinaweza pia kusababisha kamasi au damu kuonekana kwenye kinyesi chako. N.k….!!!!
Hizi ni Baadhi Ya Sababu za Wewe Kujiaidia Kinyesi chenye Makamasi
IKIWA UNA SHIDA HII,KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!