Dalili za kukojoa mara kwa mara kwa mwanamke,chanzo na Tiba
Dalili za kukojoa kwa Mwanamke mara kwa mara huweza kuashiria matatizo mbali mbali ya kiafya ikiwemo;
– Maambukizi ya magonjwa kama vile UTI(Urinary track infection), Kuumia au kupata majeraha(Injury) eneo la kibofu au magonjwa mengine.
– Hali yoyote inayoufanya mwili wako kutengeneza Mkojo Zaidi, huweza kuleta tatizo la kukojoa mara kwa mara
– Matatizo kwenye misuli, nerves au tishu zingine zinazoathiri uwezo wa kibofu cha mkojo kufanya kazi
– Kuwa kwenye aina flani ya matibabu ya Saratani
– Vitu unavyokunywa au dawa unazotumia mfano dawa jamii ya Diuretics huweza kusababisha mwili kutengeneza mkojo zaidi. n.k
Mara nyingi kukojoa mara kwa mara huambatana na dalili zingine kwenye mfumo wa mkojo ikiwemo;
- Kuhisi maumivu au usumbufu wowote wakati wa kukojoa
- Kuhisi kukojoa kila wakati
- Kupata shida ya kukojoa
- Mkojo kubaki au kutoka wenyewe
- Kutoa mkojo wenye harufu kali n.k
Chanzo cha kukojoa kwa mwanamke mara kwa mara
Hizi hapa ni baadhi ya Sababu Za kukojoa kwa mwanamke mara kwa mara;
1. Maambukizi kwenye njia ya Mkojo(urinary tract infection-UTI)
Moja ya chanzo kikubwa cha tatizo la kukojoa kwa Mwanamke mara kwa mara ni maambukizi ya magonjwa kama vile UTI.
Hii ndio sababu ya kawaida ya kukojoa mara kwa mara. UTI hutokea wakati bakteria wanapoingia kwenye kibofu cha mkojo kupitia urethra. Wanaume pia hupata UTI, lakini hutokea mara nyingi zaidi kwa wanawake kwani wanawake wana mrija mfupi wa mkojo(urethra),
Hii ina maana kwamba bakteria husafiri umbali mdogo sana kabla ya kuambukiza njia ya mkojo na kusababisha UTI.
UTI kwa wanawake inaweza kuzuiwa kwa kupangusa vizuri baada ya kutoka chooni, au kutumia njia nyingine ambayo italinda mrija wa mkojo dhidi ya bakteria wa E.coli. Usafi sahihi pia ni muhimu, hasa baada ya kujamiiana.
2. Matatizo ya kiafya ambayo huweza kuathiri misuli, nerves au tishu za kibofu cha Mkojo, mfano;
- Kudhoofika kwa nerves kwa sababu ya tatizo la hernia kwenye eneo la chini ya mgongo
- Tatizo la upungufu wa hormones kama vile Oestrogen kutokana na mwanamke kufikia ukomo wa hedhi(menopause) inaweza kusababisha kibofu kuwa na kazi nyingi kupita kiasi na mwanamke kupata shida ya kushindwa kuzuia mkojo kwa muda mrefu.
3. Tatizo la Uzito mkubwa na Unene(Obesity),
Shida hii huweza kuongeza shinikizo kweye kibofu cha mkojo hali ambayo huweza kupelekea ukojoe mara kwa mara,
Kumbuka; kutofautisha kukojoa mara kwa mara na kuhisi hali ya kuungua wakati wa kukojoa;
Mbali na magonjwa mengine kama UTI, Kukojoa mara kwa mara hakuna uhusiano wa karibu na magonjwa ya Zinaa, Ingawa ikiwa unahisi hali ya kuungua wakati wa kukojoa hii huweza kuwa na uhusiano wa karibu na magonjwa mengine ya Zinaa kama vile;
Pia kuhisi kuungua wakati wa kukojoa huweza kuhusishwa na matatizo mengine kama vile;
- Mawe kwenye figo(Kidney stones)
- Tatizo la Urethral stricture; Hii ni hali ya mrija wa mkojo kuwa mwembamba na hali hii husababisha kuhisi kuungua na maumivu wakati wa kukojoa kwa wanawake.
- Tatizo la Urethritis(Kuvimba kwa njia au mrija wa mkojo)
- Tatizo la PID(Pelvic inflammatory disease)
- Saratani ya kibofu cha mkojo(Bladder cancer)
- Tatizo la Vulvovaginitis n.k
4. Sababu zingine za kukojoa kwa Mwanamke mara kwa mara ni pamoja na;
– Kuwa na Saratani ya kibofu(Bladder cancer)
– Mawe kwenye kibofu
– Tatizo la Interstitial cystitis
– Maambukizi kwenye Figo(pyelonephritis)
– Tatizo la kushindwa kuzuia mkojo kutoka(Urinary incontinence)
– Tatizo la Anterior vaginal prolapse (cystocele)
– Ugonjwa wa kisukari(Diabetes)
- Type 1 diabetes
- Type 2 diabetes
– Matumizi ya vitu jamii ya Diuretics (water retention relievers)
– Kunywa pombe au kutumia vitu vya Caffeine
– Kunywa Sana maji
– Kuwa mjamzito
– Tiba ya mionzi inayoathiri eneo la pelvis au lower abdomen n.k
Ukiwa na tatizo hili hakikisha unapata Tiba sahihi haraka.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!