Story
Idara ya Uhamiaji ya Gambia (GID) imezindua rasmi sare mpya kwa wajawazito
Idara ya Uhamiaji ya Gambia (GID) imezindua rasmi sare mpya zilizobuniwa mahsusi kwa Maafisa wajawazito, hatua inayolenga kuboresha ustawi wao na kuwawezesha kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa faraja na heshima katika kipindi chote cha ujauzito.
Kwa mujibu wa ripoti za Vyombo vya Habari Nchini huko, Uongozi wa Idara hiyo umeeleza kuwa sare hizo zimeundwa kwa kuzingatia mahitaji ya Maafisa wajawazito ili kuwawezesha kufanya kazi kwa ufanisi bila kulazimika kuvaa sare zisizowatosha kadri ujauzito unavyoendelea.
Inaelezwa kwamba, hatua hiyo pia inaonyesha dhamira ya taasisi hiyo ya kujenga mazingira jumuishi na rafiki kwa Maafisa Wanawake.
Kwa mujibu wa GID, uzinduzi wa sare hizo ni sehemu ya maboresho ya sera za Ustawi wa Watumishi, ukilenga kuimarisha usawa mahali pa kazi na kuthibitisha kuwa ujauzito haupaswi kuwa kikwazo kwa Mwanamke kutekeleza majukumu yake ya kikazi kwa hadhi na kujiamini.
#MillardAyoUPDATES
Medical Disclaimer
Medical Disclaimer: Taarifa kwenye makala hii ni kwa ajili ya Updates au elimu ya jumla tu na haichukui nafasi ya uchunguzi,Tiba au ushauri wa kitaalamu wa daktari kwa mtu mmoja mmoja. Kama una dharura au tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa.
Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?
💬 Wasiliana na Daktari Hapa