Connect with us

Uzazi/Ujauzito

Magonjwa Yanayosababisha Mwanamke Asipate Mimba

Doctor Ombeni

Published

on

Kupata mtoto ni ndoto ya wanandoa wengi, lakini si kila wanandoa hupata ujauzito kwa urahisi. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), takribani mtu 1 kati ya 6 wenye umri wa kuzaa duniani hukumbana na changamoto ya ugumba (infertility) wakati fulani wa maisha yao. Changamoto hii inaweza kutokana na matatizo ya mwanamke, mwanaume, wote wawili au wakati mwingine sababu isijulikane.

Kwa mwanamke, magonjwa mbalimbali yanaweza kuathiri utoaji wa yai, mirija ya uzazi, mfuko wa uzazi au mfumo wa homoni, hivyo kufanya iwe vigumu kushika mimba.

Ugumba ni nini?

Ugumba ni hali ya kushindwa kupata ujauzito baada ya kufanya tendo la ndoa mara kwa mara bila kutumia njia za uzazi wa mpango kwa kipindi cha miezi 12. Kwa wanawake wenye umri wa miaka 35 au zaidi, uchunguzi unapendekezwa kuanza baada ya miezi 6 ya kujaribu kupata ujauzito bila mafanikio.

1. Polycystic Ovary Syndrome (PCOS)

PCOS ni mojawapo ya sababu kuu za ugumba kwa wanawake. Ni ugonjwa wa homoni—Huu ni Ugonjwa unaohusisha homoni na unaoathiri takriban 10% hadi 13% ya wanawake walio katika umri wa kuzaa. Unahusisha viwango vya juu vya androjeni (homoni za kiume), hedhi isiyo ya kawaida, na vifuko vidogo vilivyojaa maji kwenye ovari, ingawa sio Cysts.

Dalili

  • Hedhi zisizo za kawaida au kukosa hedhi.
  • Kuongezeka kwa uzito.
  • Chunusi nyingi.
  • Nywele nyingi usoni au kifuani.
  • Ugumu wa kupata ujauzito.n.k

Kwa nini husababisha ugumba?

#Soma Zaidi hapa,kuhusu Ugonjwa unaojulikana kama PCOS

2. Endometriosis

Huu ni ugonjwa ambapo tishu zinazofanana na ukuta wa ndani wa mfuko wa uzazi hukua nje ya mfuko wa uzazi.

Dalili

Husababisha vipi ugumba?

Huleta makovu na msongamano ndani ya nyonga, unaweza kuziba mirija ya uzazi na kuathiri ubora wa mayai au upandikizaji wa mimba.

3. Pelvic Inflammatory Disease (PID)

PID ni maambukizi ya Bacteria kwenye viungo vya uzazi vya mwanamke, mara nyingi yanayotokana na magonjwa ya zinaa kama klamidia au kisonono.

Dalili

  • Maumivu chini ya tumbo.
  • Kutokwa uchafu wenye harufu mbaya.
  • Homa.
  • Maumivu wakati wa tendo la ndoa.n.k..

Husababisha vipi ugumba?

Maambukizi yanaweza kuacha makovu yanayoziba mirija ya uzazi, hivyo yai kushindwa kukutana na mbegu za mwanaume. #Soma Zaidi madhara ya PID

4. Kuziba kwa Mirija ya Uzazi

Mirija ya uzazi ndiyo njia ambayo yai hupita kuelekea kwenye mfuko wa uzazi.

Mirija inaweza kuzibwa kutokana na:

Mirija ikiziba, mbegu za mwanaume haziwezi kulifikia yai.

5. Fibroids za Mfuko wa Uzazi

Fibroids ni uvimbe usio wa saratani unaoota kwenye mfuko wa uzazi.

Ingawa si fibroids zote husababisha ugumba, baadhi yake:

  • Huzuia upandikizaji wa mimba.
  • Hubadilisha umbo la mfuko wa uzazi.
  • Huziba mirija ya uzazi.

6. Matatizo ya Tezi (Thyroid)

Tezi ikifanya kazi kupita kiasi au chini ya kiwango inaweza kuvuruga homoni zinazodhibiti hedhi na ovulesheni.

Dalili zinaweza kujumuisha:

  • Uchovu.
  • Kubadilika uzito.
  • Hedhi zisizo za kawaida.
  • Kushindwa kupata mimba.

7. Hyperprolactinemia

Hii ni hali ya kuwa na kiwango kikubwa cha homoni ya prolactin.

Dalili:

  • Kukosa hedhi.
  • Kutoka maziwa kwenye matiti bila ujauzito.
  • Kushindwa kutoa yai.

Matibabu ya dawa mara nyingi hurudisha uwezo wa kushika mimba.

8. Primary Ovarian Insufficiency

Hii hutokea pale ovari zinapoacha kufanya kazi kabla ya umri wa miaka 40.

Dalili:

  • Kukosa hedhi.
  • Joto la ghafla mwilini.
  • Ugumu wa kupata ujauzito.

Dalili zinazopaswa kukupeleka hospitalini

  • Kushindwa kupata mimba baada ya mwaka mmoja.
  • Hedhi zisizo za kawaida.
  • Kukosa hedhi.
  • Maumivu makali wakati wa hedhi.
  • Maumivu wakati wa kujamiiana.
  • Kutokwa uchafu usio wa kawaida.
  • Historia ya PID au magonjwa ya zinaa.

Vipimo vinavyoweza kufanyika

Daktari anaweza kupendekeza:

  • Kipimo cha Ultrasound.
  • Kipimo cha HSG kuangalia mirija ya uzazi.
  • Vipimo vya homoni (FSH, LH, TSH, Prolactin, AMH).
  • Vipimo vya magonjwa ya zinaa.
  • Laparoscopy ikiwa inashukiwa endometriosis.
  • Pia mwanaume hufanyiwa kipimo cha mbegu za uzazi (semen analysis), kwa kuwa tatizo linaweza kuwa kwa mwanaume, mwanamke au wote wawili.

Je, Magonjwa Haya Yanatibika?

Ndiyo. Matibabu hutegemea chanzo cha tatizo. Baadhi ya wanawake hupata ujauzito baada ya:

  • Dawa za kurekebisha homoni.
  • Dawa za kuchochea utoaji wa yai.
  • Antibiotiki kwa maambukizi.
  • Upasuaji wa kuondoa fibroids au kutibu endometriosis.
  • Teknolojia za uzazi kama IVF pale inapohitajika.

Facts Check:

Kushindwa kupata mimba si hukumu ya maisha. Sababu nyingi zinaweza kugunduliwa na kutibiwa mapema. Ikiwa umekuwa ukijaribu kupata ujauzito bila mafanikio, ni muhimu kuwasiliana na Wataalam wa Afya au kuwahi hospitalini kwa uchunguzi wa kina. Pia kumbuka kuwa ugumba si tatizo la mwanamke pekee; mwanaume naye anatakiwa kufanyiwa uchunguzi ili kubaini chanzo halisi cha tatizo.

Kwa Ushauri Zaidi,Elimu au Tiba tuwasiliane kwa namba +255758286584.

References:

  1. World Health Organization (WHO). Infertility Fact Sheet.
  2. Mayo Clinic. Female Infertility – Symptoms and Causes.
  3. Mayo Clinic. Infertility – Symptoms and Causes.

🏆Certified| Doctor from Afyaclass.Hapa utapata Ushauri & Tiba juu ya magonjwa mbali mbali. Kwa msaada Zaidi Tuwasiliane kupitia namba: +255758286584.Pata dondoo za afya kila siku kwa kufuatilia kupitia: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *