Afyaclass Eye
Je ni kweli majivu huzuia mimba?
Je ni kweli majivu yanaweza kuzuia mimba?
Afyaclass Eye tumefanya uchambuzi kuhusu dhana hii ya kutumia majivu kuzuia mimba, na haya ndiyo matokeo ya uchambuzi wetu, karibu kufuatilia;
Tafiti zinasemaje kuhusu matumizi ya majivu kuzuia mimba?
(1) Uchambuzi kutoka UNFPA
United Nations Population Fund (UNFPA), ni shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi na haki za kijinsia, linafanya kazi katika zaidi ya nchi 150 kusaidia haki za wanawake na wasichana.
UNFPA imezungumzia tabia ya baadhi ya watu kutumia njia zisizosalama kuzuia mimba, na katika chapisho lake la 09, july 2018 kuna maelezo hapa;
Unsafe, unreliable: Dangerous pregnancy-prevention methods (09 Jul 2018)
Around the world, people are resorting to dangerous, ineffective methods to prevent pregnancy – an indication of the enormous need for family planning access and education.
Hapa wanazungumzia matumizi ya Njia hatari za kuzuia mimba, njia zisizo salama na zisizoaminika:
Duniani kote, watu wanatumia njia hatari na zisizofaa kuzuia mimba – jambo linaloashiria uhitaji mkubwa wa upatikanaji wa huduma za uzazi wa mpango pamoja na elimu kuhusiana na suala hilo.
UNFPA imekusanya mifano kadhaa ya matumizi yasiyofaa – na hata yenye madhara – ambayo watu hutumia wanapojaribu kuzuia mimba,
Chat Nasi Whatsapp
"Ungana na Wasomaji zaidi ya 12,000 wanaopata huduma ndani ya afyaclass, Kama unachangamoto yoyote ya kiafya; Kwa Ushauri&Tiba tuwasiliane hapa kupitia WhatsApp, Kama huna Whatsapp tuma SMS au Piga +255758286584."
Chat WhatSapp HapaNjia hizi, ambazo mara nyingi hutegemea uvumi, imani na hadithi potofu, zinaanzia kwenye matumizi ya kemikali zinazoharibu kama vile dawa za kuua vijidudu hadi matumizi ya vifaa vya nyumbani kama vile sifongo za jikoni(kitchen sponges) n.k
Njia kama vile kuruka juu, chini baada ya kufanya tendo, eti ili kuzuia mbegu za mwanaume zisiingie, vitu ambavyo huweza kupelekea kupata mimba zisizotarajiwa.
Ingawa pia kwenye uchambuzi huu hawakutaja moja kwa moja majivu, lakini walieleza matumizi ya vitu vya asili vinavyoendana na hivo.
(2) Utafiti uliochapishwa na Tanzania Journal of Health Research
Jicho la kiuchambuzi la Afyaclass Eye lilipita na kukagua tafiti mbali mbali za nchini Tanzania mpaka kupata utafiti huu ambao ulichapishwa mwaka 2010, kwenye jarida la Tanzania journal of Health Research,
Title ya mada hiyo ilikuwa; ”
Seek any means, and keep it your secret”: Young women’s attempts to control their reproduction through contraceptive and fertility practices in rural Tanzania
Waandishi: Plummer ML, Wamoyi J, Shigongo ZS, Mshana G, Obasi AIN, Ross DA, na Wight D.
Jarida: Tanzania Journal of Health Research, 2010;12(3):160–171.
DOI: 10.4314/thrb.v12i3.51099
Utafiti huu ulichunguza majaribio ya wanawake vijana kudhibiti uzazi kupitia uzazi wa mpango na ulinzi wa uzazi au uendelezaji katika vijiji vya Tanzania.
Na utafiti huu ulitokana na uchunguzi wa washiriki katika vijiji tisa, majadiliano ya vikundi na mahojiano katika vituo vingine vitatu, na ziara 16 za wagonjwa wa kuigiza(health facility simulated patient visits) kutoka 1999-2002.
Utafiti huu ulieleza kwamba, Uzazi ulithaminiwa sana, lakini mimba za nje ya ndoa zilinyanyapaliwa. Wasichana wengi walitumia uzazi wa mpango wa kitamaduni, kama vile kuvaa hirizi au kunywa majivu yaliyochanganywa na maji(Ash solution). Akina mama wasio na waume maarufu kama Single mothers wakati mwingine walitumia uzazi wa mpango wa kisasa, ikiwa ni pamoja na matumizi ya sindano za Depo Provera, kwa sababu sindano zilikuwa zinapatikana kwa urahisi na ni za faragha zaidi.
Utafiti ulisema nini?
Utafiti huu ulifanyika katika maeneo ya vijijini Tanzania, ukichunguza namna wanawake vijana walivyojaribu kudhibiti uzazi.
Watafiti walitumia mbinu mbalimbali za kukusanya taarifa, zikiwemo:
- Uchunguzi wa moja kwa moja katika vijiji tisa.
- Majadiliano ya vikundi katika vijiji vingine vitatu.
- Mahojiano na washiriki.
- Ziara 16 za wagonjwa wa kuigiza katika vituo vya afya.
Katika matokeo yake, watafiti walibaini kuwa baadhi ya wasichana walitumia njia za jadi za kuzuia mimba, zikiwemo kuvaa hirizi na kunywa mchanganyiko wa majivu na maji (ash solutions).
Hii ina maana kwamba matumizi ya majivu kwa lengo la kuzuia mimba yaliripotiwa katika utafiti uliofanyika Tanzania.
Hata hivyo, utafiti huu haukupima kama majivu hayo yalikuwa na uwezo wa kuzuia mimba au kiwango cha ufanisi wake, au yalitumika tu kwa imani kama yanaweza kusaidia kuzuia ujauzito.(Hakuna majibu yoyote yaliyoeleza uwezo na ufanisi wa majivu katika kuzuia mimba kwenye utafiti huu)
NB: Moja ya vitu tulivyogundua ni uhaba mkubwa wa tafiti na taarifa sahihi kutoka kwa jamii kuhusu uwezo na ufanisi wa majivu katika kuzuia mimba.
Majibu ya Kisayansi yanasemaje
Hakuna ushahidi wa kutosha wa kisayansi unaothibitisha kuwa majivu yanaweza kuzuia mimba. Majivu si njia ya uzazi wa mpango inayotambuliwa na wataalamu wa afya,
Zipo njia mbali mbali za uzazi wa mpango ambazo zimetajwa na kuidhinishwa na shirika la afya duniani(WHO) ikiwemo;
- Condomu
- Njiti
- Kitanzi
- Sindano n.k
Kila moja ikiwa na faida zake na maudhi yake(side effects).
Hitimisho kutoka Afyaclass Eye
Je ni kweli majivu huweza kuzuia mimba?
Hapana, majivu hayawezi kuzuia mimba. Hakuna ushahidi wa kisayansi au msingi wa kimatibabu unaounga mkono matumizi ya majivu kama njia ya uzazi wa mpango. Tumia mbinu na njia za uzazi wa mpango zinazoaminika kama vile kondomu, vidonge vya uzazi wa mpango, njia kama kitanzi (IUD), kipandikizi, au njia zingine zilizoidhinishwa kimatibabu.
Baada ya kufanya uchambuzi wa kina kuhusu dhana hii ya kutumia majivu kuzuia mimba, hatukupata ushidi wa moja kwa moja wa kisayansi au asili unaonyesha kwamba matumizi ya majivu yanaweza kuzuia mimba.
Hivo kuepuka kupata mimba zisizotarajiwa, tunashauri utumie njia za uzazi wa mpango za uhakika na zilizothibitishwa kitaalamu.
Links Used:
- https://www.ajol.info/index.php/thrb/article/view/51099
- https://aa.unfpa.org/news/balloons-disinfectant-brandy-used-attempts-prevent-pregnancy
- https://www.unfpa.org/unsafe-unreliable-dangerous-pregnancy-prevention-methods
- https://www.who.int/news-room/fact-sheets/detail/family-planning-contraception
- https://askfilo.com/user-question-answers-smart-solutions/can-ash-prevent-someone-from-getting-pregnant-3433333331303634
References
- United Nations Population Fund. (2018, July 9). Balloons, disinfectant, brandy used in attempts to prevent pregnancy. https://aa.unfpa.org/news/balloons-disinfectant-brandy-used-attempts-prevent-pregnancy
- United Nations Population Fund. (2018, July 9). Unsafe, unreliable: Dangerous pregnancy-prevention methods. https://www.unfpa.org/unsafe-unreliable-dangerous-pregnancy-prevention-methods
- World Health Organization. (2025, July 3). Family planning/contraception methods. https://www.who.int/news-room/fact-sheets/detail/family-planning-contraception
- Jarida la Tanzania journal of Health Research,Title ya mada hiyo ilikuwa; “Seek any means, and keep it your secret”: Young women’s attempts to control their reproduction through contraceptive and fertility practices in rural TanzaniaWaandishi: Plummer ML, Wamoyi J, Shigongo ZS, Mshana G, Obasi AIN, Ross DA, na Wight D.
Jarida: Tanzania Journal of Health Research, 2010;12(3):160–171.
DOI: 10.4314/thrb.v12i3.51099
Ushauri,Elimu,Tiba
Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.
Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?
💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)