Connect with us
KIPYA • AFYACLASS EYE Page Yote →

Madai Mengi ya Afya Si Sahihi — Tunachunguza & Kutoa Ukweli

AfyaClass Eye inachambua madai potofu ya jamii kuhusu afya na kutoa majibu sahihi ya kitaalamu.

MAKALA YA KWANZA • Afyaclass Eye Mtu akianza kutumia dawa za presha, hawezi kuziacha hata kama presha imeshuka
Soma ›
Jifunze ukweli kuhusu madai mengine ya afya: Fungua AfyaClass Eye →

magonjwa

Tatizo La Bandama Kuvimba Au Kujaa Maji,chanzo,Dalili Na Tiba

Doctor Ombeni

Published

on

🩺
Medically reviewed by Afyaclass Teams, Writen by Dr.Ombeni
1440 Views
0 Comments

TATIZO LA BANDAMA KUVIMBA AU KUJAA MAJI,CHANZO,DALILI NA TIBA

Bandama ni kiungo muhimu katika mfumo wa limfu na kinga ya mwili. Kazi zake ni pamoja na kuchuja damu, kuondoa chembe nyekundu za damu zilizozeeka au kuharibika, kusaidia kupambana na maambukizi na kuhifadhi baadhi ya chembe za damu.

Kuvimba kwa bandama, kitaalamu kunakoitwa splenomegaly, ni hali ambayo bandama huwa kubwa kuliko ukubwa wake wa kawaida.

Hali hii si ugonjwa unaojitegemea, bali ni dalili inayoweza kusababishwa na magonjwa mbalimbali, yakiwemo malaria, maambukizi mengine, magonjwa ya ini, saratani za damu na magonjwa ya damu yanayoharibu chembe nyekundu za damu.

Baadhi ya watu wenye bandama zilizovimba hawapati dalili zozote, lakini wengine wanaweza kupata madhara makubwa kutegemea ukubwa wa bandama na chanzo cha uvimbe huo (Giovanni & Giovanni, 2023).

Watu wengi kwa hivi sasa hupatwa na tatizo hili la bandama kuvimba huku wengine wakiambiwa bandama zimejaa maji baada ya kufanyiwa vipimo mbali mbali, tatizo la bandama kuvimba kwa kitaalam hujulikana kama Splenomegaly, je chanzo cha matatizo ya bandama kuvimba au kujaa maji ni nini?

Chanzo cha Kuvimba Bandama

CHANZO CHA TATIZO LA BANDAMA KUVIMBA NI PAMOJA NA;

– Maambukizi mbali mbali ya vimelea vya magonjwa kama vile;

1. Maambukizi ya bacteria mfano bacteria wanaosababisha ugonjwa wa kaswende au syphilis,maambukizi ya bacteria kwenye kuta za ndani ya moyo na kusababisha matatizo kama endocarditis n.k

2. Maambukizi ya virusi kama vile mononucleosis n.k

3. Maambukizi ya Parasites kama vile kwenye ugonjwa wa Malaria

4. Magonjwa ya ini kama Cirrhosis pamoja na magonjwa mengine yanayoshambulia Ini

5. Aina mbali mbali za anemia(upungufu wa damu mwilini), hasa anemia inayohusu uvunjaji wa seli nyekundu za damu yaani RED BLOOD CELLS(RBCs) kwenye hatua ya mwanzo kabsa kabla ya kukomaa

6. Uwepo wa tatizo la kansa kwenye damu kama vile: shida ya Leukemia,Lmyphomas,myeloproliferative neoplasms n.k

7. Magonjwa au matatizo mbali mbali kwenye mfumo wa uvunjaji chakula kwenye seli yaani metabolic disorders kama vile tatizo la Gaucher,Niemann n.k

8. Tatizo la presha kwenye mishipa ya Veins ndani ya Bandama au Ini au mtu kupatwa na shida ya damu kuganda au kutengeneza clots kwenye mishipa hii ya veins

9. Magonjwa kwenye mfumo wa kinga ya mwili yaani autoimmune conditions kama vile shida ya Lupus,Sarcoidosis n.k

Dalili za Kuvimba bandama

DALILI ZA MTU MWENYE MATATIZO HAYA YA BANDAMA NI PAMOJA NA;

– Mtu kupata maumivu makali upande wa kushoto karibu na mbavu

– Mtu kuhisi uzito kwenye eneo la karibu na mbavu kushoto juu kidogo ya kitovu

– Hali ya mtu kuhisi kushiba hata kama umekula kidogo sana au hujala kitu,hii ni kwasababu bandama hugandamiza tumbo la chakula hivo kufanya chakula kiingie kidogo sana au mtu kuhisi kushiba muda wote

– Mtu kuanza kuonyesha dalili mbali mbali za upungufu wa damu yaani anemia kwenye mwili wake

– Mtu kupata shida ya kuvuja damu kwa urahisi zaidi,kushambuliwa na magonjwa mbali mbali mara kwa mara n.k

Vipimo vya Tatizo la kuvimba bandama

VIPIMO MBALI MBALI KUFANYIKA KAMA VILE

• Vipimo vya kuchukua Sample ya damu yaani blood tests

• Kufanya physical examination

• Kufanya ultrasound,Ct Scan au MRI n.k

MATIBABU YA TATIZO HILI LA BANDAMA

Tiba ya matatizo ya bandama kama vile bandama kuvimba au bandama kujaa maji hutegemea na chanzo chake,hivo kama chanzo ni maambukizi ya bacteria basi mgonjwa atapewa antibiotics mbali mbali kutibu shida hii n.k

Kama matibabu ya dawa yameshindikana huduma ya upasuaji huweza kufanyika kwa mgonjwa

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO HILI TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Madhara ya kuvimba kwa bandama (Splenomegaly)

1. Kupungua kwa chembechembe au seli za damu (Cytopenia)

Bandama zinapovimba kupita kiasi, zinaweza kuanza kuhifadhi na kuondoa chembechembe au seli za damu kwa kiwango kikubwa kuliko kawaida.

Hali hii inajulikana kama hypersplenism.

Inaweza kusababisha:

  • Upungufu wa damu(Anemia): Kupungua kwa chembechembe nyekundu za damu, hali inayoweza kusababisha uchovu, kizunguzungu, mapigo ya moyo kwenda kasi na kupumua kwa shida.
  • Thrombocytopenia: Kupungua kwa chembe sahani zinazosaidia damu kuganda, hali inayoweza kuongeza uwezekano wa kutokwa na damu bila kuganda au kupata michubuko kirahisi.
  • Leukopenia: Kupungua kwa chembechembe au seli nyeupe za damu, hali inayoweza kuongeza uwezekano wa kupata maambukizi.

Madhara haya yanaweza kutokea kwa wakati mmoja au kwa kutofautiana kulingana na chanzo cha ugonjwa.

2. Kupasuka kwa bandama (Splenic rupture)

Hii ni mojawapo ya madhara hatari zaidi ya kuvimba kwa bandama.

Bandama iliyovimba inaweza kuwa rahisi kuumia au kupasuka, hasa baada ya ajali, kuanguka au kupata kipigo kwenye tumbo.

Hata hivyo, katika baadhi ya magonjwa, bandama inaweza kupasuka bila kupata jeraha kubwa.

Kupasuka kwa bandama kunaweza kusababisha:

  • Kutokwa na damu nyingi ndani ya tumbo.
  • Kushuka kwa shinikizo la damu.
  • Mapigo ya moyo kwenda kasi.
  • Kizunguzungu au kupoteza fahamu.
  • Mshtuko kwenye mzunguko wa damu (hemorrhagic shock).
  • Kifo ikiwa damu nyingi itapotea bila matibabu ya haraka.

Mtu mwenye bandama iliyovimba anapaswa kutafuta huduma ya dharura ikiwa anapata maumivu makali ghafla upande wa juu kushoto wa tumbo, hasa ikiwa maumivu yanaenea hadi kwenye bega la kushoto.

3. Maumivu ya tumbo na kuhisi kushiba haraka

Bandama inapokuwa kubwa, inaweza kubana viungo vilivyo karibu nayo, hasa tumbo.

Hali hii inaweza kusababisha:

  • Maumivu au hali ya kutokuwa na raha upande wa juu kushoto wa tumbo.
  • Kuhisi tumbo limejaa hata baada ya kula chakula kidogo.
  • Kupungua kwa hamu ya kula.
  • Kushiba haraka kuliko kawaida.

Ikiwa hali hii itaendelea kwa muda mrefu, inaweza kusababisha mtu kula chakula kidogo na kupata upungufu wa virutubisho au kupungua uzito kwa kasi.

4. Kuongezeka kwa hatari ya maambukizi

Bandama ni sehemu muhimu ya mfumo wa kinga ya mwili. Husaidia kuondoa vijidudu kutoka kwenye damu na kutengeneza mwitikio wa kinga dhidi ya maambukizi.

Ugonjwa Madhara yanayoweza kutokea
Malaria Anemia, kupungua kwa chembe sahani na katika hali kali kupasuka kwa bandama.
Cirrhosis ya ini Portal hypertension, kutokwa na damu na matatizo ya ini.
Leukemia Kupungua kwa chembe za damu, maambukizi na kutokwa na damu.
Hemolytic anemia Kuharibika kwa chembe nyekundu za damu na anemia.
Infectious mononucleosis Bandama kuvimba na kuongezeka kwa hatari ya kupasuka.

Ni muhimu kutambua kwamba si kila mtu mwenye bandama iliyovimba atapata madhara haya. Madhara hutegemea chanzo cha uvimbe, ukubwa wa bandama na hali ya afya ya mgonjwa.

References:

  • Di Sabatino, A., Carsetti, R., & Corazza, G. R. (2011). Post-splenectomy and hyposplenic states. The Lancet, 378(9785), 86–97. https://doi.org/10.1016/S0140-6736(10)61493-6
  • Giovanni, J. E., & Giovanni, J. E. (2023). Splenomegaly. In StatPearls. StatPearls Publishing. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK430907/
  • McKenzie, C. V., Colonne, C. K., Yeo, J. H., & Fraser, S. T. (2018). Splenomegaly: Pathophysiology and clinical manifestations. Hematology/Oncology Clinics of North America, 32(4), 635–647.
1440 Views
0 Comments
✚

Ushauri,Elimu,Tiba

Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)

🏆Certified| Doctor from Afyaclass. Maudhui haya ni kwa ajili ya elimu ya jumla ya afya. Unapohitaji ushauri wa kina, uchunguzi, au matibabu binafsi, wasiliana na daktari kupitia namba:+255758286584.Pia tufwatilie kupitia: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Guest Avatar

LATEST POSTS

magonjwa2 years ago

Tatizo La Bandama Kuvimba Au Kujaa Maji,chanzo,Dalili Na Tiba

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams, Writen by Dr.Ombeni TATIZO LA BANDAMA KUVIMBA AU KUJAA MAJI,CHANZO,DALILI NA TIBA Bandama ni kiungo...

magonjwa ya wanawake3 days ago

Kutokwa na damu ya hedhi kwa muda mrefu

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams, Writen by Dr.Ombeni Kutokwa na damu ya hedhi kwa muda mrefu Kwa kawaida mwanamke anatakiwa...

Story1 hour ago

Mungu amenifanya nicheke baada ya miaka 7 ya dhihaka – Mwanamume wa Nigeria afurahia kuwa baba

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams, Writen by Dr.Ombeni Mungu amenifanya nicheke baada ya miaka 7 ya dhihaka – Mwanamume wa...

Stars Health3 hours ago

Princess Kate Afunguka Jinsi Saratani Ilivyobadilisha Mwili na Akili Yake

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams, Writen by Dr.Ombeni Princess Kate Afunguka Jinsi Saratani Ilivyobadilisha Mwili na Akili Yake Catherine, Princess...

Afyaclass Eye18 hours ago

Mtu akianza kutumia dawa za presha, hawezi kuziacha hata kama presha imeshuka

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams, Writen by Dr.Ombeni Dai:Mtu akianza kutumia dawa za presha, hawezi kuziacha hata kama presha imeshuka...

Story23 hours ago

Mwandishi wa habari wa Kike asambaa sana mtandaoni baada ya kuonyesha misuli kwenye mikono

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams, Writen by Dr.Ombeni Mwandishi wa habari wa televisheni kutoka Australia asambaa sana mtandaoni baada ya...

Afyaclass Eye1 day ago

Kunywa maji ya moto kunayeyusha mafuta tumboni

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams, Writen by Dr.Ombeni Dai: Kunywa maji ya moto kunayeyusha mafuta tumboni. Je, kuna ukweli juu...

magonjwa ya wanaume1 day ago

Korodani kupotea,korodani moja kupotea au kupanda juu kwa mtu mzima

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams, Writen by Dr.Ombeni Korodani kupotea,korodani moja kupotea au kupanda juu kwa mtu mzima Kwa mtu...

magonjwa5 years ago

Tatizo La Masikio Kupiga Kelele,chanzo na tiba yake(Tinnitus)

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams, Writen by Dr.Ombeni Tatizo La Masikio Kupiga Kelele,chanzo na tiba yake(Tinnitus) Tinnitus, Tatizo hili huhusisha...

Afyaclass Eye2 days ago

Kitunguu Saumu kinatibu kila aina ya Maambukizi

🩺Medically reviewed by Afyaclass Teams, Writen by Dr.Ombeni Kitunguu Saumu kinatibu kila aina ya Maambukizi Madai haya yanaenea kwenye jamii...

1441
0