Connect with us
Author 1 Author 2 Author 3 Author 4
Authors

magonjwa

Tatizo la Kuota Vinyama Sehemu za Siri,genital warts,Chanzo,Dalili na Tiba

Doctor Ombeni

Published

on

1440 Views
0 Comments

Tatizo la Kuota Vinyama Sehemu za Siri,genital warts,Chanzo,Dalili na Tiba

Genital warts ni ugonjwa gani,Soma Zaidi hapa kufahamu

Genital warts ni moja ya aina ya magonjwa ya zinaa,Takribani watu wote wanaofanya ngono bila kinga wanaweza kuambukizwa angalau aina moja ya virusi vya human papilloma (HPV),

virusi vinavyosababisha vidonda sehemu za siri au masundosundo, wakati fulani wa maisha yao.

Genital warts huathiri zaidi tishu zenye unyevu unyevu za eneo la sehemu za siri, zinaweza kuonekana kama matuta madogo,

yenye rangi kama nyama au kuwa na mwonekano wa cauliflower(tazama kwenye picha). Katika hali nyingine, warts ni ndogo sana kuonekana.

Lakini pia warts huweza kujitokeza kwenye maeneo mengine ya mwili kama vile kwenye vidole vya mikono,viganja vya mikono,

Genital warts pia inaweza kutokea mdomoni au kooni mwa mtu ambaye amefanya ngono kwa njia ya mdomo na mtu aliyeambukizwa.

Kwa Wanawake, genital warts zinaweza kutokea kwenye;

  • mashavu ya uke au vulva,
  • kuta za uke
  • eneo katikati ya uke na njia ya haja kubwa
  • Eneo kuzunguka njia ya haja kubwa
  • Ndani ya uke, pamoja na mlango wa kizazi au cervix.

Kwa Wanaume, genital warts huweza kutokea kwenye;

  • Ncha au shimo la uume,
  • Kwenye ngozi ya korodani au scrotum,
  • Kwenye eneo la haja kubwa(anus).n.k

Dalili za genital warts

Dalili za genital warts ni pamoja na;

– Kuota Vinyama Sehemu Za Siri kama kwenye Picha hapo,

-Kuwa na Uvimbe mdogo, wa rangi kama nyama au kahawia kwenye sehemu zako za siri

– Wakati mwingine Kuwashwa sehemu za siri

– Kutokwa na damu wakati wa kujamiiana

– Vidonda vya sehemu za siri,

Hata hivyo, mara chache sana, warts za sehemu za siri zinaweza kuzidi katika makundi makubwa kwa mtu aliye na mfumo wa kinga uliodhaifu.

Chanzo cha Genital warts

Human papillomavirus (HPV) ndyo virusi ambavyo husababisha tatizo la warts,

Kuna zaidi ya aina 40 za HPV zinazoathiri sehemu za siri.

Genital warts karibu kila mara huenea kwa njia ya kujamiiana, na sio lazima genital warts zionekane ili ueneze maambukizi kwa mwenzi wako ambaye unashiriki naye tendo.

Sababu hatarishi za kupata Genital Warts

Watu wengi wanaofanya ngono huambukizwa virusi vya human papilloma(HPV) sehemu za siri wakati fulani.

Mambo ambayo yanaweza kuongeza hatari ya kuambukizwa ni pamoja na:

✓ Kufanya ngono bila kinga au kondomu

✓ Kuwa na wapenzi wengi

✓ Baada ya kupata maambukizi mengine ya magonjwa ya zinaa

✓ Kufanya mapenzi na mpenzi ambaye hujui historia yake kwenye ngono

✓ Kuanza kufanya ngono katika umri mdogo

✓ Kuwa na mfumo  dhaifu wa kinga mwilini mfano kwa wagonjwa wenye virusi vya UKIMWI (VVU)

Matatizo yanayotokana na genital warts au virusi vya human papilloma (HPV)

Matatizo yanayotokana na genital warts au virusi vya human papilloma (HPV) ni pamoja  na:

1. kupata Saratani.

Saratani ya shingo ya kizazi(cervical cancer) imehusishwa kwa karibu na maambukizi ya HPV  sehemu za siri,

Aina fulani za HPV pia huhusishwa na;

  • saratani za uke,
  • njia ya haja kubwa,
  • kwenye uume,
  • mdomoni na kooni.

Maambukizi ya HPV sio mara zote husababisha saratani, lakini ni muhimu kwa wanawake kufanya kipimo cha “Pap” mara kwa mara, hasa wale ambao wameambukizwa na aina hatari zaidi za HPV.

2. Matatizo wakati wa ujauzito.

Mara chache wakati wa ujauzito, genital warts zinaweza kuongezeka, na kufanya iwe vigumu wakati wa kukojoa.

genital warts kwenye ukuta wa uke zinaweza kuzuia kuvutika kwa tishu za uke wakati wa kujifungua,  warts kubwa kwenye vulva au kwenye uke zinaweza kutoka damu wakati wa kujifungua baada ya kuvutwa zaidi.

Ni mara chache sana, mtoto anayezaliwa na mama mwenye genital warts kuwa na warts kwenye koo.  Mtoto anaweza kuhitaji upasuaji ili kuzuia njia ya hewa kuziba.

Jinsi ya Kuzuia genital warts

– Epuka ngono zembe au tumia kinga kama condomu wakati wa tendo

– Epuka kuwa na wapenzi wengi

– Epuka kufanya ngono katika umri mdogo

– Pata chanjo ya kuzuia maambukizi ya human papilloma virus(HPV),

Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) vinapendekeza chanjo ya HPV kwa wasichana na wavulana wenye umri wa miaka 11 na 12, ingawa inaweza kutolewa mapema kama umri wa miaka 9.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

1440 Views
0 Comments
✚

Ushauri,Elimu,Tiba

Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)

🏆Certified| Doctor from Afyaclass. Maudhui haya ni kwa ajili ya elimu ya jumla ya afya. Unapohitaji ushauri wa kina, uchunguzi, au matibabu binafsi, wasiliana na daktari kupitia namba:+255758286584.Pia tufwatilie kupitia: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Guest Avatar

LATEST POSTS

magonjwa ya Zinaa1 hour ago

Ugonjwa wa Genital herpes,chanzo,dalili na Tiba

HERPES SEHEMU ZA SIRI: DALILI, NAMNA INAVYOAMBUKIZWA, KINGA NA MATIBABU Herpes sehemu za siri (Genital herpes) ni maambukizi ya zinaa...

Stars Health12 hours ago

Mwigizaji mkongwe wa India, Nana Patekar, amefariki dunia leo

Mwigizaji mkongwe wa India, Nana Patekar, amefariki dunia leo Oktoba 8, 2026, akiwa na umri wa miaka 75, baada ya...

Ebola12 hours ago

Kenya yaweka Ulinzi Mkali kwa Wasafiri Kutoka Nchi 10 Baada ya Kesi ya Ebola

Kenya yaweka Ulinzi Mkali kwa Wasafiri Kutoka Nchi 10 Baada ya Kesi ya Ebola Nairobi, Kenya — 8 Oktoba 2026:...

magonjwa ya watoto1 day ago

Mtoto Kutokula Chakula: Kwa Nini Hamu ya Kula Hupotea?

Mtoto Kutokula Chakula: Kwa Nini Hamu ya Kula Hupotea? Kupungua kwa hamu ya kula kwa mtoto ni jambo linaloweza kutokea...

Ebola1 day ago

Kenya imeanza kuwaweka karantini watu waliotathminiwa kuwa na hatari ya kuambukizwa Ebola

Kenya imeanza kuwaweka karantini watu waliotathminiwa kuwa na hatari ya kuambukizwa Ebola Kenya imeanza kuwaweka katika karantini watu waliotathminiwa kuwa...

Utafiti2 days ago

Mtafiti wa Tauni Afariki Urusi: Marekani yaendelea Kufuatilia Hatari ya Tauni ya Mapafu

Mtafiti wa Tauni Afariki Urusi: Marekani yaendelea Kufuatilia Hatari ya Tauni ya Mapafu Mtafiti aliyekuwa akifanya kazi katika kituo cha...

Ukimwi2 days ago

Je kondomu inazuia Maambukizi ya Ukimwi kwa asilimia ngapi?

Je kondomu inazuia mMambukizi ya Ukimwi kwa asilimia ngapi? Kondomu hupunguza kwa kiwango kikubwa hatari ya kuambukizwa HIV, lakini si...

magonjwa1 year ago

Tatizo la Kuota Vinyama Sehemu za Siri,genital warts,Chanzo,Dalili na Tiba

Tatizo la Kuota Vinyama Sehemu za Siri,genital warts,Chanzo,Dalili na Tiba Genital warts ni ugonjwa gani,Soma Zaidi hapa kufahamu Genital warts...

Ebola3 days ago

Kisa cha Kwanza cha Ebola chathibitishwa Kenya na mgonjwa afariki dunia

Kisa cha Kwanza cha Ebola Chathibitishwa Kenya na Mgonjwa Afariki Dunia Nairobi, Kenya — Oktoba 6, 2026: Kenya imethibitisha kisa...

Others3 days ago

Nigeria yaomboleza Vifo vya Watu 32 Baada ya Ajali ya Ndege ya Kijeshi

Nigeria yaomboleza Vifo vya Watu 32 Baada ya Ajali ya Ndege ya Kijeshi Nigeria imeingia katika kipindi cha maombolezo baada...

1441
0