magonjwa
Kukojoa mara kwa mara husababishwa na nini
Kukojoa Mara kwa Mara Husababishwa na Nini?
Kukojoa mara kwa mara tunakozungumzia hapa ni hali ya mtu kuhisi kwenda haja ndogo mara nyingi kuliko kawaida. Kwa baadhi ya watu inaweza kuwa kutokana na kunywa maji mengi, lakini wakati mwingine inaweza kuwa dalili ya ugonjwa unaohitaji uchunguzi.
Sababu kuu za kukojoa mara kwa mara
1. Maambukizi ya njia ya mkojo (UTI)
UTI ni moja ya sababu kubwa ya kukojoa mara kwa mara. Mtu anaweza pia kupata:
- Maumivu au hali ya kuhisi kuwaka moto wakati wa kukojoa
- Haja ya kukojoa kwa haraka
- Kukojoa na Mkojo kama hauishi au hubaki kidogo
- Maumivu chini ya tumbo hasa upande wa kushoto mwa tumbo
- Kukojoa Mkojo wenye harufu kali n.k
2. Ugonjwa wa Kisukari (Diabetes mellitus)
Sukari ikiwa nyingi kwenye damu inapofika kwenye mkojo, figo huongeza utoaji wa maji pamoja na sukari hiyo. Hii inaweza kusababisha mtu kukojoa mara nyingi zaidi na kuwa na kiu kubwa pia ya maji.
3. Kunywa maji mengi
Mtu anayekunywa kiasi kikubwa cha maji, hasa kwa muda mfupi, anaweza pia kupata hali hii ya kukojoa mara kwa mara au mara nyingi bila kuwa na ugonjwa wowote.
4. Vinywaji vyenye caffeine
Matumizi ya Kahawa,chai,energy drinks na vinywaji vingine vyenye caffeine vinaweza kuongeza uzalishaji wa mkojo na pia kuchochea kibofu,hivo kusababisha hali ya kukojoa mara kwa mara.
5. Kibofu cha mkojo kuwa na msisimko kupita kiasi (Overactive bladder)
Hali hii husababisha kibofu kujikaza(Contracts) bila kutakiwa hata kama hakijajaa vizuri. Hali hii huweza kusababisha Mtu:
Chat Nasi Whatsapp
"Ungana na Wasomaji zaidi ya 12,000 wanaopata huduma ndani ya afyaclass,Kama unachangamoto yoyote ya kiafya;Kwa Ushauri&Tiba tuwasiliane hapa kupitia WhatSapp,Kama huna Whatsapp tuma SMS au Piga +255758286584."
Chat WhatSapp Hapa- Kuhisi haja kali ya kukojoa kwa ghafla
- Kukojoa mara nyingi mchana
- Kuamka mara nyingi usiku
- Wakati mwingine kushindwa kuzuia mkojo.
6. Ujauzito
Mjamzito anaweza kukojoa mara kwa mara, hasa mwanzoni mwa ujauzito na katika kipindi cha mwisho. Kadiri ujauzito unavyokua, mfuko wa uzazi unaweza kuweka shinikizo(Pressure) zaidi kwenye kibofu,Eneo au Room ya Kibofu kupungua au kukandamizwa zaidi kwa kibofu. Hali hii huweza kusababisha mjamzito kukojoa mara kwa mara.
7. Kuongezeka kwa tezi dume kwa mwanaume (BPH)
Kwa wanaume, hasa kadiri umri unavyoongezeka, tezi dume inaweza kuongezeka na kuzuia mtiririko mzuri wa mkojo. Hii inaweza kusababisha kukojoa mara kwa mara, hasa usiku, mkojo kutoka kwa shida au kuhisi kibofu hakijaisha mkojo.
8. Mawe kwenye njia ya mkojo
Mawe kwenye figo au njia ya mkojo yanaweza kusababisha muwasho na kuongeza pia haja ya kukojoa. Mara nyingi yanaweza kuambatana na maumivu makali ya mgongo, ubavu au tumbo na wakati mwingine damu kwenye mkojo.
9. Dawa zinazoongeza mkojo (Diuretics)
Baadhi ya dawa, hasa dawa zinazotumika kusaidia kupunguza maji mwilini au kutibu shinikizo la damu, zinaweza kufanya mtu akojoe mara nyingi zaidi.
10. Matatizo ya mfumo wa fahamu
Magonjwa au uharibifu wa mishipa inayodhibiti kibofu unaweza kuvuruga namna kibofu kinavyohifadhi na kutoa mkojo. Kisukari pia kinaweza kuathiri mishipa hiyo.
Ni wakati gani mtu anapaswa kumuona mtaalamu wa afya?
Kukojoa mara kwa mara kunahitaji uchunguzi hasa ikiwa kuna:
- Hali ya Kuwaka moto au kuhisi kuungua au maumivu wakati wa kukojoa
- Damu kwenye mkojo
- Homa au kutetemeka
- Maumivu ya mgongo/ubavu
- Kiu kubwa ya maji
- Kupungua uzito bila sababu
- Mkojo kutoka kwa shida
- Kushindwa kabisa kutoa mkojo
- Kuamka mara nyingi sana usiku kwa ajili ya kukojoa.
Homa, kutetemeka, kichefuchefu/kutapika pamoja na maumivu ya mgongo au ubavu vinaweza kuashiria maambukizi yaliyofika kwenye figo na vinahitaji huduma ya haraka.
Vipimo vinavyoweza kufanyika
Chanzo hakipaswi kubashiriwa kwa dalili pekee. Mtaalamu wa afya anaweza kufanya kipimo cha mkojo, kipimo cha sukari kwenye damu, vipimo vya kazi ya figo au vipimo vingine kulingana na dalili.
Je,Unatatizo hili? Kwa Ushauri zaidi,Elimu na Tiba tuwasiliane +255758286584.
References;
- National Institute of Diabetes and Digestive and Kidney Diseases (NIDDK). Bladder Infection (Urinary Tract Infection—UTI) in Adults.
- NIDDK. Diabetes, Sexual, & Bladder Problems.
- NIDDK. Symptoms & Causes of Bladder Control Problems.
- Mayo Clinic. Overactive bladder—Symptoms and causes.
- Mayo Clinic. Diabetes symptoms: When diabetes symptoms are a concern.
- NHS. Common health problems in pregnancy—Peeing a lot in pregnancy.
Ushauri,Elimu,Tiba
Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.
Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?
💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)

