Connect with us

magonjwa

Dalili za Fangasi Mdomoni: Zifahamu Ishara, Sababu na Tiba

Doctor Ombeni

Published

on

Dalili za Fangasi Mdomoni: Zifahamu Ishara, Sababu na Tiba

Fangasi mdomoni ni maambukizi yanayosababishwa na kuongezeka kwa fangasi aina ya Candida albicans. Kwa kawaida, fangasi huyu huishi kwenye mdomo bila kusababisha matatizo. Hata hivyo, kinga ya mwili inapopungua au mazingira ya mdomo yanapobadilika, fangasi huongezeka na kusababisha maambukizi yanayojulikana kama oral thrush.

Haya ni maeneo makubwa ambayo Fangasi jamii ya Candida Albicans unaweza kuwapata; kwenye njia ya utumbo, mdomoni,ukeni, na pia kwenye ngozi.

Watoto wachanga, wazee, watu wenye kisukari, wanaotumia dawa za antibiotiki kwa muda mrefu, corticosteroids za kuvuta (inhalers), au wenye kinga dhaifu kama wagonjwa wa VVU wako kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata maambukizi haya.

Dalili za fangasi mdomoni

1. Mabaka meupe ndani ya mdomo

Hii ndiyo dalili ya kwanza ambayo hutokea zaidi kwa wagonjwa Wengi. Mabaka meupe yanaweza kuonekana:

  • Kwenye ulimi
  • Mashavuni kwa ndani
  • Kwenye Fizi
  • Kwenye Lips pembeni au kwenye mdomo
  • Eneo la Kooni n.k

Mabaka haya yanaweza kufutika, lakini mara nyingi huacha sehemu nyekundu inayoweza kuvuja damu kidogo.

2. Kuhisi hali ya Muwasho,Maumivu au kuungua mdomoni

Baadhi ya wagonjwa huhisi maumivu, kuwashwa au hisia za kuungua, hasa wanapokula vyakula vya moto au vyenye pilipili, au wakati wapo tu bila kula chochote,hali hii huweza kujitokeza.

3. Kupoteza ladha

Watu wengine hupata mabadiliko ya ladha au kushindwa kuhisi ladha ya chakula vizuri.

4. Maumivu wakati wa kumeza kitu

Maambukizi yakisambaa kuelekea kooni au kwenye umio, yanaweza kusababisha hali ya maumivu wakati wa kumeza kitu.

5. Hali ya kupasuka kwenye pembe za mdomo

Pembe za mdomo zinaweza kupasuka, kuwa nyekundu na kuuma kwa watu wenye maambukizi ya Fangasi Mdomoni. Hali hii huitwa angular cheilitis.

6. Hisia ya pamba mdomoni

Baadhi ya wagonjwa hueleza kuhisi kana kwamba kuna pamba au kitu laini kilichokwama mdomoni.

7. Mdomo kuwa mkavu

Fangasi wanaweza kuambatana na ukavu wa mdomo unaofanya kuzungumza au kula kuwa kugumu.

Kwahyo maambukizi haya ya Fangasi Mdomoni huweza kuambatana na hali nyingine ya Mdomo kuwa Mkavu Zaidi.

8. Hali ya Mdomo au Lips kubadilika rangi, Kuwa na Utando mweupe Mdomoni n.k

Hali hii pia huweza kutokea kwa Wagonjwa wenye Fangasi mdomoni, ambapo mdomo huweza kubadilika rangi kuwa mwekundu zaidi,kuwa na mabaka meupe, Pamoja na Dalili ya Utando mweupe mdomoni.

Bonus Points: Dalili nyingine kwa watoto wachanga

Kwa watoto wachanga, fangasi mdomoni Wanaweza kusababisha:

  • Mabaka meupe kwenye ulimi na mashavu ya ndani mdomoni.
  • Mtoto kukataa kunyonya kutokana na maumivu.
  • Kulia wakati wa kunyonya.
  • Wakati mwingine mama anayenyonyesha hupata maumivu au kuwashwa kwenye chuchu kutokana na maambukizi kwenda kwake.

Sababu zinazoongeza hatari ya maambukizi haya ya Fangasi Mdomoni

  • Michezo michafu ya kufanya mapenzi kwa njia ya Mdomo(Oral Sex)
  • Kutokusafisha kinywa vizuri
  • Kisukari kisichodhibitiwa.
  • Matumizi ya antibiotiki kwa muda mrefu.
  • Kutumia inhaler za corticosteroids bila kusafisha mdomo baada ya matumizi.
  • Kinga ya mwili kuwa dhaifu (ikiwemo VVU, saratani au matumizi ya dawa zinazoshusha kinga).
  • Kuvuta sigara.
  • Kuvaa meno bandia yasiyosafishwa vizuri.
  • Kinywa kuwa kikavu kutokana na magonjwa au dawa.n.k.

Madaktari wanasemaje?

Madaktari wa magonjwa ya kinywa wanaeleza kuwa fangasi mdomoni mara nyingi hugunduliwa kwa kuangalia dalili za mgonjwa. Ikiwa maambukizi yanajirudia mara kwa mara au ni makali, wanaweza kupendekeza vipimo vingine kama vya kisukari, VVU au hali nyingine zinazoweza kushusha kinga ya mwili.

Uzoefu wa wagonjwa

Wagonjwa wengi hueleza kuwa dalili zilianza kwa hisia ya ukavu na ladha kubadilika. Baadaye waliona mabaka meupe kwenye ulimi na mashavu ya ndani ya mdomo au nje ya mdomo. Baada ya kutumia dawa za kuua fangasi walizoandikiwa na daktari na kuboresha usafi wa mdomo, dalili zilianza kupungua ndani ya siku chache, ingawa wengine walihitaji matibabu ya muda mrefu kutokana na chanzo cha msingi kama kisukari.

Data zinaonyesha nini?

  • Kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO), fangasi aina ya Candida ni miongoni mwa vijidudu vinavyosababisha maambukizi kwa kiasi kikubwa kwa watu wenye kinga dhaifu.
  • Tafiti zinaonyesha kuwa watoto wachanga, wazee, na watu wanaoishi na VVU wana uwezekano mkubwa wa kupata fangasi mdomoni kuliko watu wenye kinga nzuri.
  • Kwa watu wanaotumia inhaler za corticosteroids kwa pumu ambazo ni Safi, kusafisha au kusukutua mdomo baada ya kutumia dawa hupunguza hatari ya kupata fangasi mdomoni.

Matibabu

Matibabu hutegemea ukali wa maambukizi na yanaweza kujumuisha:

  • Dawa za kuua fangasi za kupaka au kusukutua mdomoni.
  • Dawa za kumeza kwa maambukizi makali au yanayojirudia.
  • Kutibu chanzo cha msingi, kama kudhibiti kisukari au kubadili matumizi ya dawa fulani chini ya ushauri wa daktari.

Usitumie dawa bila ushauri wa daktari, hasa ikiwa dalili zinajirudia mara kwa mara.

NA KWA USHAURI ZAIDI AU TIBA TUWASILIANE +255758286584.

Jinsi ya kujikinga

  • Piga mswaki mara mbili kwa siku.
  • Safisha meno bandia kila siku.
  • Sukutua mdomo baada ya kutumia inhaler za corticosteroids.
  • Dhibiti kisukari vizuri.
  • Epuka kuvuta sigara.
  • Tumia antibiotiki pale tu unaposhauriwa na mtaalamu wa afya.

Wakati wa kumwona daktari

Nenda hospitali AU ongea na Wataalam wa Afya ikiwa:

  • Mabaka meupe hayapotei baada ya siku chache.
  • Una maumivu makali au unashindwa kula na kunywa.
  • Unapata fangasi mara kwa mara.
  • Una homa au maambukizi yanaonekana kuenea hadi kooni.

FACTS check:

Fangasi mdomoni ni maambukizi yanayotibika, lakini yanaweza kuwa ishara ya tatizo jingine la kiafya kama kisukari au kinga dhaifu ya mwili. Uchunguzi na matibabu ya mapema husaidia kuondoa maambukizi na kuzuia kujirudia.

References:

🏆Certified| Doctor from Afyaclass.Hapa utapata Ushauri & Tiba juu ya magonjwa mbali mbali. Kwa msaada Zaidi Tuwasiliane kupitia namba: +255758286584.Pata dondoo za afya kila siku kwa kufuatilia kupitia: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *