Stars Health
Picha Mpya kutoka kwa Céline Dion, hali yake ya Kiafya kwa Sasa
Picha Mpya kutoka kwa Céline Dion, hali yake ya Kiafya kwa Sasa
Kwa taarifa za leo, 11 Agosti 2026, Céline Dion bado anaendelea kuishi na Stiff-Person Syndrome (SPS), ugonjwa adimu wa mfumo wa fahamu unaoweza kusababisha kukakamaa kwa misuli na spasms.
Habari kubwa zaidi kwa sasa ni kwamba hali Céline Dion imeimarika kiasi cha kumwezesha kujiandaa kurejea jukwaani. Mnamo Machi 2026, alitangaza mfululizo wa Show mjini Paris, zinazotarajiwa kuanza Septemba 2026.
Hali yake kwa sasa;
Bado ana SPS; ugonjwa huo ni wa muda mrefu na unaweza kusababisha kukakamaa na mikazo isiyodhibitika ya misuli.
Ameendelea na matibabu na mazoezi/rehabilitation ili kurejesha uwezo wake wa kuimba na kufanya Shows.
Jambo la kutia moyo ni kwamba amerudi kwenye shughuli za muziki. Mwaka 2026 alitoa wimbo mpya wa Kifaransa, “Dansons”, na ametangaza kurejea kwenye maonyesho ya moja kwa moja.
Kwa sasa hakuna ushahidi wa kuaminika kwamba amepona kabisa. Kurudi kwake jukwaani hakumaanishi SPS imekwisha, bali inaonyesha ameweza kudhibiti hali yake kwa kiwango kinachomruhusu kufanya shughuli hizo.
Chat Nasi Whatsapp
"Ungana na Wasomaji zaidi ya 12,000 wanaopata huduma ndani ya afyaclass,Kama unachangamoto yoyote ya kiafya;Kwa Ushauri&Tiba tuwasiliane hapa kupitia WhatSapp,Kama huna Whatsapp tuma SMS au Piga +255758286584."
Chat WhatSapp HapaKwa hiyo, Céline Dion Hali yake inazidi kuimarika na anaendelea na maisha na kazi zake huku akiishi na Stiff-Person Syndrome; hali yake inaonekana kuwa bora kuliko kipindi ambacho ugonjwa ulimlazimisha kusitisha ziara zake.
Hizi ni baadhi ya Picha Zake Mpya Alizozipandisha Kwenye Mtandao wake wa Instagram.
Photos Credits: Celine Dion



Medical Disclaimer
Medical Disclaimer: Taarifa kwenye makala hii ni kwa ajili ya Updates au elimu ya jumla tu na haichukui nafasi ya uchunguzi,Tiba au ushauri wa kitaalamu wa daktari kwa mtu mmoja mmoja. Kama una dharura au tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa.
Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?
💬 Wasiliana na Daktari Hapa