Stars Health
Hali ya Papa Leo XIV imeendelea kuimarika baada ya upasuaji wa mapafu
Papa Leo XIV anaendelea kuimarika baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye pafu. Vatican yasema alikuwa na usiku mtulivu huku waumini na viongozi duniani wakituma salamu za kumpa moyo.
Baada ya kugundulika na saratani ya mapafu, Papa Leo XIV amefanyiwa upasuaji uliofanikiwa mjini Roma. Sasa macho yanaelekezwa kwenye hatua za matibabu na ratiba yake ya miezi ijayo.
Papa Leo XIV, ameendelea kuimarika baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye pafu lake la kulia katika Hospitali ya Gemelli mjini Roma. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Habari ya Vatican, Papa alikuwa na “usiku mtulivu” baada ya upasuaji huo na hali yake inaendelea vizuri.
Vatican imesema taarifa zaidi kuhusu mwenendo wa afya ya Papa zitatolewa baadaye, huku akiendelea kupatiwa matibabu na uangalizi wa karibu hospitalini.
Saratani ya Mapafu Yagundulika
Madaktari waligundua kwamba Papa Leo XIV alikuwa na saratani ya mapafu aina ya adenocarcinoma baada ya kuondoa sehemu ya chini ya pafu lake la kulia wakati wa upasuaji huo. Hata hivyo, Vatican haijaeleza ukubwa wa uvimbe huo wala hatua ya ugonjwa huo.
Daktari Stefano Margaritora, aliyeongoza upasuaji huo, pamoja na daktari binafsi wa Papa, Luigi Carbone, walieleza kuwa Papa alibaki katika chumba cha upasuaji kwa takriban saa tatu. Upasuaji wenyewe ulidumu dakika 90 na ulifanikiwa bila matatizo yaliyoripotiwa.
Chat Nasi Whatsapp
"Ungana na Wasomaji zaidi ya 12,000 wanaopata huduma ndani ya afyaclass, Kama unachangamoto yoyote ya kiafya; Kwa Ushauri&Tiba tuwasiliane hapa kupitia WhatsApp, Kama huna Whatsapp tuma SMS au Piga +255758286584."
Chat WhatSapp HapaSalamu za uponyaji zamiminika kwa Papa Leo XIV duniani kote.Salamu za uponyaji zamiminika kwa Papa Leo XIV duniani kote.
Salamu za uponyaji zamiminika kwa Papa Leo XIV duniani kote.Picha: Guglielmo Mangiapane/REUTERS
Waumini Waendelea Kuombea Afya Yake
Nje ya Hospitali ya Gemelli, waumini mbalimbali wameendelea kukusanyika kwa ajili ya maombi na kutoa salamu za kumtakia Papa nafuu ya haraka.
Miongoni mwao ni Sonia Coppola kutoka Italia ambaye alieleza matumaini yake kwamba Papa atapona na kurejea kuongoza shughuli zake za kidini haraka iwezekanavyo.
“Tunamtakia Papa nafuu ya haraka na uponyaji wenye mafanikio. Na tuna matumaini atarejea kuongoza Sala ya Malaika wa Bwana katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, ambako nasi tutakuwepo,” alisema Sonia.
Ziara na Mikutano Yaathirika
Mwishoni mwa juma lililopita, Papa Leo XIV mwenye umri wa miaka 71 alitangaza kuwa uchunguzi wa kawaida wa afya ulikuwa umebaini uvimbe mdogo katika moja ya mapafu yake, na kwamba alikuwa akijiandaa kufanyiwa upasuaji.
Papa huyo anatarajiwa kubaki hospitalini kwa takriban wiki moja. Vatican pia imetangaza kufutwa kwa mikutano yote kati ya Papa na waumini hadi Oktoba 20 ili kumpa nafasi ya kuendelea na matibabu na kupona.
Chanzo:DW
Ushauri,Elimu,Tiba
Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.
Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?
💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)