Connect with us
Author 1 Author 2 Author 3 Author 4
Authors

Afya News

Vipimo vya Vinasaba kutumika kutambua waliofariki kwa Ajali Morogoro

Avatar

Published

on

299 Views
0 Comments

Vipimo vya Vinasaba kutumika kutambua waliofariki kwa Ajali Morogoro

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dk. Fidelice Mafumiko, amewataka ndugu wa watu waliofariki katika ajali ya Mkambalani, mkoani Morogoro, kufika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kusaidia zoezi la utambuzi wa miili ya marehemu kwa kutumia vipimo vya vinasaba.

Ajali hiyo imesababisha vifo vya watu 32 na wengine 30 kujeruhiwa, huku mamlaka husika zikiendelea na hatua za kubaini utambulisho wa waliofariki kwa kutumia vipimo vya vinasaba.

Dk. Mafumiko amesema zoezi la utambuzi linahusisha hatua mbili kuu, ambazo ni uchunguzi wa miili iliyopatikana na uchukuaji wa sampuli kutoka kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya kulinganisha vinasaba na kuthibitisha utambulisho wa miili hiyo.

Amesema Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali itaendelea kushirikiana na uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro pamoja na Mganga Mkuu wa Mkoa kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa.

Naye, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Dkt. Best Magoma, amesema hospitali hiyo inaendelea kutoa huduma za matibabu kwa majeruhi wa ajali hiyo waliolazwa katika kituo hicho.

Ajali hiyo ilitokea eneo la Mkambalani katika barabara kuu ya Morogoro–Dar es Salaam, ikihusisha lori aina ya Scania lililokuwa limebeba miti na basi la abiria mali ya kampuni ya Green Line.

Vyombo hivyo vya usafiri viligongana uso kwa uso, na kusababisha moto mkubwa ulioteketeza basi hilo. Moto huo ulisababisha baadhi ya miili ya waliofariki kuharibika vibaya, hali inayofanya utambuzi wa marehemu kwa kutumia vinasaba kuwa muhimu. Credits:ITV.

299 Views
0 Comments
✚

Ushauri,Elimu,Tiba

Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)

Karibu Afyaclass Jukwaa linaloongoza kwa utoaji wa elimu sahihi ya Afya. Hapa utapata Elimu na Updates mbali mbali za Afya Duniani. Pia Pata dondoo za afya kila siku kwa kufuatilia kupitia Mitandao hii hapa: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Guest Avatar

LATEST POSTS

WHO9 hours ago

Kifo cha mfanyakazi wa maabara NCHINI URUSI chazua maswali kuhusu NIMONIA isiyojulikana chanzo chake

Kifo cha mfanyakazi wa maabara NCHINI URUSI chazua maswali kuhusu NIMONIA isiyojulikana chanzo chake Tarehe ya kuchapishwa: 13 Oktoba 2026...

EVENTS10 hours ago

Mwanaume Afariki Baada ya Kuanguka Kutoka Kwenye Mchezo wa Roller Coaster wa Urefu wa Takribani Mita 61 Nchini Marekani

Mwanaume Afariki Baada ya Kuanguka Kutoka Kwenye Mchezo wa Roller Coaster wa Urefu wa Takribani Mita 61 Nchini Marekani Tarehe...

afyatips17 hours ago

Jinsi ya kuongeza damu kwa haraka

Jinsi ya kuongeza damu kwa haraka Chembe hai nyekundu za damu maarufu kama Haemoglobin(hb) ndizo hutumika katika kuangalia kiwango cha...

magonjwa ya Zinaa5 days ago

Ugonjwa wa Genital herpes,chanzo,dalili na Tiba

HERPES SEHEMU ZA SIRI: DALILI, NAMNA INAVYOAMBUKIZWA, KINGA NA MATIBABU Herpes sehemu za siri (Genital herpes) ni maambukizi ya zinaa...

Afya News2 days ago

Vipimo vya Vinasaba kutumika kutambua waliofariki kwa Ajali Morogoro

Vipimo vya Vinasaba kutumika kutambua waliofariki kwa Ajali Morogoro Mkemia Mkuu wa Serikali, Dk. Fidelice Mafumiko, amewataka ndugu wa watu...

Stars Health2 days ago

Papa Leo XIV Kufanyiwa Upasuaji wa Kuondoa Uvimbe Mdogo kwenye Pafu

Papa Leo XIV Kufanyiwa Upasuaji wa Kuondoa Uvimbe Mdogo kwenye Pafu Roma, Italia — Oktoba 11, 2026 Papa Leo XIV...

magonjwa ya wanaume4 days ago

Madhara ya UTI kwa mwanaume,Athari 8 zinazoweza kutokea

Madhara Ya Uti Kwa Mwanaume: Athari 8 zinazoweza kutokea na namna ya kuziepuka Maambukizi ya njia ya mkojo, yanayojulikana kama...

EVENTS4 days ago

Watu 32 wamefariki dunia na wengine 37 kujeruhiwa katika Ajali ya barabarani Morogoro

Watu 32 wamefariki dunia na wengine 37 kujeruhiwa katika ajali mbili za barabarani zilizotokea usiku wa kuamkia leo Oktoba 9,...

WHO5 days ago

WHO yazindua Mpango wa Kimataifa wa Kukabiliana na Shinikizo la Damu Wakati wa Ujauzito

Shirika la Afya Duniani (WHO), kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, limezindua mpango mpya wa kimataifa wa kukabiliana na matatizo ya...

Stars Health5 days ago

Mwigizaji mkongwe wa India, Nana Patekar, amefariki dunia leo

Mwigizaji mkongwe wa India, Nana Patekar, amefariki dunia leo Oktoba 8, 2026, akiwa na umri wa miaka 75, baada ya...

300
0