Afya News
Chanjo ya kwanza ya kisonono duniani yazinduliwa wakati maambukizi yakiongezeka
Chanjo ya kwanza ya kisonono duniani yazinduliwa wakati maambukizi yakiongezeka
Uingereza itakuwa nchi ya kwanza duniani kuanza kutoa chanjo dhidi ya ugonjwa wa zinaa wa kisonono.
Haitapatikana kwa kila mtu. Lengo zaidi litakuwa kwa wanaume wenye kujihusisha na wapenzi wa jinsi moja na wapenzi wawili wenye historia ya kuwa na wapenzi wengi au waliokuwa na historia ya kupata magonjwa ya zinaa.
Chanjo hiyo ina ufanisi wa 30-40%, lakini NHS England inatumai kuwa itabadilisha idadi inayoongezeka ya maambukizi. Kulikuwa na kesi zaidi ya 85,000 mnamo 2023, ya juu zaidi tangu rekodi zilipoanza mnamo 1918.
Chat Nasi Whatsapp
"Ungana na Wasomaji zaidi ya 12,000 wanaopata huduma ndani ya afyaclass, Kama unachangamoto yoyote ya kiafya; Kwa Ushauri&Tiba tuwasiliane hapa kupitia WhatsApp, Kama huna Whatsapp tuma SMS au Piga +255758286584."
Chat WhatSapp HapaUgonjwa wa kisonono hauneshi dalili wakati wote, lakini zinaweza kujumuisha maumivu, kuvimba kwa sehemu za siri na utasa.
Ni watu wangapi watachagua kuchanjwa haijulikani. Lakini makadirio ya Chuo cha Imperial London yanaonesha kwamba ikiwa chanjo itathibitishwa kuwa maarufu basi inaweza kuzuia kesi 100,000
Max, mwanaharakati wa afya ya ngono, aliiambia BBC Newsbeat kuwa “100%” atachanja chanjo hiyo baada ya kugunduliwa na ugonjwa wa kisonono mara mbili ndani ya mwaka mmoja.
“Nadhani hii ni nzuri kwamba imetangazwa”, anasema, na kuongeza: ” ni ushindi mkubwa tu pande zote.”
Chanjo itaanza kutolewa mwezi Agosti na itatolewa kupitia huduma za afya ya ngono.
Ushauri,Elimu,Tiba
Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.
Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?
💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)