Afya News
Vifo vya Wajawazito barani Afrika mada hii imeibuka tena
Tatizo la wajawazito kupoteza maisha kwa kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua, limetajwa katika mkutano wa kanda wa kuimarisha mbinu za kuzuia na kudhibiti tatizo hilo, unaoendelea jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo ulioanza leo, unashirikisha wadau wa afya ya mama na mtoto kutoka zaidi ya nchi 20 za Afrika ikiwakmo mwenyeji Tanzania, Kenya, Uganda. Rwanda, Burundi. Afrika Kusini, Malawi, Madagascar na nyingine nyingi.
Katika mkutano huo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Makazi (UNFPA) Tanzania, limesema kutokwa damu nyingi baada ya kujifungua kunachangia vifo vya uzazi kwa asilimia kati ya 30 hadi 40 Afrika, hasa katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Mwakilishi Mkazi wa shirika hilo, Mark Bryan Schreiner, amesema ipo haja ya kuimarisha huduma za dharura za uzazi, mifumo ya rufaa na upatikanaji wa dawa ili kuzuia vifo vya wanawake vinavyotokana na kutokwa damu nyingi baada ya kujifungua, na kwamba ingawa miongozo iliyoboreshwa ya kukabiliana na kutokwa damu nyingi baada ya kujifungua ni msingi muhimu wa kuimarisha huduma, uwepo wa miongozo pekee hautoshi kuokoa maisha bila utekelezaji wake wa vitendo.
“Utekelezaji huo unahitaji wahudumu wa afya wenye ujuzi na wanaopata msaada wa kitaalamu, upatikanaji wa uhakika wa dawa na vifaa tiba muhimu, mifumo inayofanya kazi ya rufaa za wagonjwa, upatikanaji wa damu inapohitajika, takwimu sahihi na maandalizi madhubuti ya kukabiliana na dharura. UNFPA inaungana na wadau wote wa afya ya uzazi kujadili na kuweka mikakati ya kuhakikisha vinapungua kama siyo kuisha kabisa, na imeipongeza serikali kwa kuendelea kujitolea kuboresha huduma za afya ya uzazi, mama na mtoto mchanga,” amesema Schreiner.
Amewataka wadau hao kutoka na mapendekezo na vipaumbele vitakavyomaliza au kupunguza tatizo hili, na kwamba UNFPA itaendelea kushirikiana na serikali, taasisi za kikanda, vyama vya kitaaluma, mashirika ya Umoja wa Mataifa, washirika wa maendeleo na wahudumu wa afya ili kutimiza lengo hilo.
Chat Nasi Whatsapp
"Ungana na Wasomaji zaidi ya 12,000 wanaopata huduma ndani ya afyaclass, Kama unachangamoto yoyote ya kiafya; Kwa Ushauri&Tiba tuwasiliane hapa kupitia WhatsApp, Kama huna Whatsapp tuma SMS au Piga +255758286584."
Chat WhatSapp HapaSerikali imeomba msaada katika maeneo matatu kwa wadau wa afya wa kimataifa ili iweze kuimarisha huduma za afya kwa jamii, ikiwamo ujuzi na utaalamu kwa ajili ya kupanua mafunzo ya awali na ya kazini pamoja ufuatiliaji kwa wakunga na wataalamu wa afya ili waweze kutoa huduma za kuokoa maisha ya jamii, hasa wanawake na watoto.
Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Bruno Sunguya ndiye aliyetoa ombi hilo katika ufunguzi wa mkutano huo na kutaja eneo la pili kuwa ni uoanishaji wa miongozo Ili kusaidia wizara za kimataifa kuharakisha urekebishaji na ujumuishaji wa miongozo mipya ya kimataifa ya PPH katika miongozo ya matibabu ya kitaifa, orodha ya dawa muhimu na taratibu za kawaida za matibabu.
“Eneo la tatu ni kuwa teknolojia na usalama wa bihaa za afya, ili kusaidia upanuzi wa teknolojia na bidhaa za kiubunifu, ikiwemo alioitaja kwa jina la heat-stable carbetocin, tranexamic acid na vitambaa Maalum vya kupimia damu Kwa ajili ya kusaidia mifumo ya Kanda ya ununuzi wa pamoja ili kujenga mnyororo imara wa ugavi usioingiliwa,” alisema Profesa Sunguya.
“Kwa kuwa mkutano huu unaleta pamoja zaidi ya nchi 20 kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Shirika la Afya la Afrika Magharibu (WAHO), tuutumie kuleta mafanikio kwenye sekta ya afya,” amesema.
Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Afya Africa ya Umma Barani Afrika (CDC), Dk. Hassan Mataka, amezitaka nchi za Afrika kujifunza mfumo wa huduma za dharura za uzazi wa Tanzania, EMaMA, ili kuimarisha huduma za afya ya mama na mtoto.
Amesema mfumo huo unaweza kuwa mfano kwa mataifa mengine katika kuboresha rufaa na usafirishaji wa wajawazito wanaohitaji huduma za dharura.
Ushauri,Elimu,Tiba
Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.
Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?
💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)