Connect with us

Afya News

Afrika Kusini kunufaika na chanjo mpya ya kupambana na VVU

Doctor Ombeni

Published

on

134 Views
0 Comments

Afrika Kusini taifa lenye idadi kubwa zaidi duniani ya watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI limeingia kwenye orodha ya nchi za kwanza kunufaika na chanjo ya kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi, iitwayo Lenacapavir.

Chanjo hii itakayoleta mapinduzi katika sekta ya afya, inawalenga watu ambao bado hawajaambukizwa, lakini wako katika hatari kubwa ya kupata maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Kupitia dawa hii, mtu atahitaji kuchoma sindano mbili tu kwa mwaka, kwani hulinda mwili dhidi ya virusi vya UKIMWI kwa kipindi cha hadi miezi sita.

Katika juhudi za kukomesha maambukizi mapya ya virusi vya  UKIMWI , serikali ya Afrika Kusini inapanga kuzindua rasmi dawa hii ya muda mrefu ambayo wataalamu wanasema inaweza kubadilisha mwelekeo wa mapambano dhidi ya virusi hivyo.

Waziri wa Afya wa Afrika Kusini Dokta Aaron Motsoaledi, amefafanua kwamba chanjo hii haibadilishi tiba za walioathirika, bali inawalenga watu walio salama, lakini wako katika hatari ya kuambukizwa virusi hivyo.

”Hii si kwa ajili ya matibabu, bali ni kwa ajili ya kinga. Wale ambao tayari wanaishi na VVU wataendelea na tiba zao za sasa. Chanjo hii ni kwa wale ambao bado hawajaambukizwa, lakini wako kwenye hatari kubwa ya kuambukizwa virusi vya UKIMWI, ” alisema Dokta Motsoaledi.

Katika majaribio ya kliniki, Lenacapavir imeonyesha matokeo ya kuvutia hasa miongoni mwa wasichana ambao ni wazazi , kundi ambalo linaongoza kwa maambukizi mapya barani Afrika.

”Katika majaribio, dawa hii ilionekana kuwa na ufanisi wa asilimia 100. Msichana yeyote anayepokea chanjo hizo mbili kwa mwaka anahakikishiwa ulinzi kamili dhidi ya kuambukizwa virusi vya UKIMWI, ” alieleza Daktari huyo.

Kauli ya WHO kuhusu chanjo hiyo

Kwa upande wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Mkurugenzi Mkuu Tedros Adhanom Ghebreyesus, anasema mafanikio haya yanaweza kuwa hatua muhimu kuelekea kukomesha kwa UKIMWI barani Afrika.

”Japo tunakabiliwa na changamoto nyingi, chanjo hii yenye nguvu ya kinga inaweza kuisaidia Afrika Kusini kufikia lengo lake la kuumaliza UKIMWI,” alisisitiza Ghebreyesus.

Kwa muda mrefu, hospitali nyingi nchini  Afrika Kusini  zimekuwa zikizidiwa na idadi kubwa ya wagonjwa wa UKIMWI, huku wengi wao wakirudi wakiwa na hali mbaya baada ya kusitisha tiba. Ujio wa Lenacapavir unatarajiwa kupunguza mzigo huo, kwa kuwa watu wengi zaidi watafanikiwa kujikinga mapema kabla ya kuambukizwa.

Joseph Nkosi, mkaazi wa Pretoria anazungumzia umuhimu wa chanjo hii, ambapo anasema itasaidia kupunguza maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

”Dawa hii itawasaidia sana vijana wa Afrika Kusini, na pia itasaidia kupunguza ongezeko la maambukizi mapya, ” alisema mkaazi mmoja wa mji wa Pretoria.

Cha kuvutia zaidi, ni kwamba chanjo hii ambayo hapo awali iligharimu dola elfu 28 za Marekani kwa mwaka, sasa itauzwa kwa dola 40 pekee, chini ya asilimia 0.1 ya bei ya awali. Hili limewezekana baada ya kampuni ya Gilead kutoa leseni za bure kwa wazalishaji wengine, kwa msaada wa mashirika kama Clinton Health Access Initiative na Taasisi ya Gates.

Chanjo inayoleta matumaini makubwa

Mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa afya Barani Afrika Limakatso Lebina anasema, kwa sasa hii ndiyo dawa ya kwanza duniani yenye nguvu kubwa dhidi ya UKIMWI:

”Hii ndiyo mara ya kwanza kuona dawa ya  kinga dhidi ya VVU  inayotoa ulinzi wa asilimia 100 kwa wanawake waliochoma sindano. Wote waliotumia hawakuambukizwa, tofauti na wale waliotumia dawa za kumeza kila siku.”

Wataalamu wanasema chanjo hii inaweza kuwa ngao muhimu ya kinga kwa makundi yenye hatari kubwa kama vile wasichana walioko kwenye balehe, vijana wa kike, na wanaotumia dawa za kulevya kwa kujidunga.

Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na UKIMWI , UNAIDS, zaidi ya watu milioni 40 duniani wanaishi na virusi vya UKIMWI. Na iwapo hata asilimia 4 tu ya watu wataanza kutumia sindano hii, inaweza kupunguza hadi asilimia 20 ya maambukizi mapya duniani.

Kwa sasa, Afrika Kusini inasubiri kibali rasmi kutoka kweny Mamlaka ya Bidhaa za Afya, SAPRA, ili kuanza kutoa dawa hii hatua kwa hatua katika hospitali za umma.

134 Views
0 Comments

Medical Disclaimer

Medical Disclaimer: Taarifa kwenye makala hii ni kwa ajili ya Updates au elimu ya jumla tu na haichukui nafasi ya uchunguzi,Tiba au ushauri wa kitaalamu wa daktari kwa mtu mmoja mmoja. Kama una dharura au tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa

🏆Certified| Doctor from Afyaclass. Maudhui haya ni kwa ajili ya elimu ya jumla ya afya. Unapohitaji ushauri wa kina, uchunguzi, au matibabu binafsi, wasiliana na daktari kupitia namba:+255758286584.Pia tufwatilie kupitia: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Guest Avatar

LATEST POSTS

Hospital7 hours ago

MNH-Mloganzila Yafanya Upasuaji wa Kurekebisha na Kurefusha Mifupa kwa Mbinu ya Ilizarov

MNH-Mloganzila Yafanya Upasuaji wa Kurekebisha na Kurefusha Mifupa kwa Mbinu ya Ilizarov Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)-Mloganzila imefanikiwa kufanya kwa...

EVENTS9 hours ago

Wavunja Record ya Dunia kwa kupanda miche 2,51,446 kwa saa moja tu

Wavunja Record ya Dunia kwa kupanda miche 2,51,446 kwa saa moja tu. Katika juhudi kubwa za kushangaza kwenye kutunza mazingira,...

magonjwa ya wanawake10 hours ago

Fangasi Ukeni: Chanzo na Dalili

Fangasi Ukeni: Chanzo na Dalili Fangasi ukeni ni maambukizi ya fangasi yanayotokea kwenye uke na mara nyingi husababishwa na fangasi...

magonjwa ya wanawake1 day ago

Hedhi yenye harufu mbaya: SABABU zinazoweza kusababisha

Kwa baadhi ya wanawake, damu ya hedhi inaweza kuwa na harufu fulani ambayo si sawa na harufu ya kawaida ya...

EVENTS1 day ago

Siku ya kuzuia kujiua duniani 2026: kubadili mtazamo na kuanza mazungumzo

SIKU YA KUZUIA KUJIUA DUNIANI 2026: KUBADILI MTAZAMO NA KUANZA MAZUNGUMZO Kaulimbiu ya 2026: “Changing the Narrative on Suicide” –...

Utafiti1 day ago

Vifo Vinavyotokana na Mimba kutunga Nje ya Kizazi

Mimba kutunga nje ya kizazi (ectopic pregnancy) ni hali ambayo mimba inajipandikiza nje ya sehemu ya kawaida ya kizazi,Mara nyingi...

Utafiti2 days ago

Ucheleweshaji wa huduma Ndani ya Hospitali Wawa Tishio Kubwa kwa Maisha ya Mama na Mtoto

Ucheleweshaji wa huduma ndani ya vituo vya afya umeonekana kuwa moja ya sababu kubwa zinazochangia vifo vya wajawazito na watoto...

Afya News2 days ago

Jinsi Dawa za Kulevya Zinavyoharibu Afya ya Kinywa na Meno

Matumizi ya dawa za kulevya yanaweza kuathiri sehemu mbalimbali za mwili, ikiwemo ubongo, moyo, ini na mfumo wa fahamu. Hata...

magonjwa3 days ago

Ugonjwa wa Selimundu,dalili,chanzo na Tiba

Katika Makala hii tunachambua Zaidi kuhusu Dalili za ugonjwa wa seli mundu,chanzo cha ugonjwa wa Seli mundu pamoja na Matibabu...

Afya News3 days ago

Wataalam wa maabara wahimizwa kuboresha huduma za afya kwa Wananchi

WATAALAM WA MAABARA WAHIMIZWA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA KWA WANANCHI Na Zakayo Mosha- WAF Morogoro Wataalam wa Maabara wamehimizwa kutumia...

135
0