Connect with us

Afya News

Mtoto asipopata chanjo hatarini kupata maambukizi ya magonjwa -Mhagama

Doctor Ombeni

Published

on

Mtoto asipopata chanjo hatarini kupata maambukizi ya magonjwa -Mhagama

Na. WAF, Tabora

Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama ameiasa jamii kuwa mstari wa mbele kuhakikisha watoto wote wanaostahili kupata chanjo wanapata ili kujikinga na magonjwa kwakuwa mtoto asipopata chanjo anakuwa hatarini kupata maambukizi ya magonjwa. 

Waziri Mhagama ameyasema hayo Aprili 28, 2025 Mkoani Tabora wakati akizindua Maadhimisho ya Wiki ya Chanjo Kitaifa yanayoenda sambamba na kauli mbiu isemayo “Chanjo ni Kinga; Tuungane kuwezesha Walengwa wote watape Chanjo.”

Amesisitiza jamii kuendelea kutumia wiki ya chanjo kama fursa ya kuhakikisha walengwa na watoto wote wanapata chanjo kulingana na ratiba na kuvielekeza vituo vya kutolea huduma za chanjo kuendelee kuwahudumia wananchi wote wanaohitaji huduma za Afya hususan huduma za chanjo. 

“Maadhimisho haya yatafanyika sambamba na utoaji wa chanjo zote ikiwemo chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi kwa mabinti wenye umri wa miaka tisa (9) ambayo itamsaidia kumkinga dhidi ya ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi hivyo kwa wale mabinti ambao hawakupatiwa chanjo ni vema wapatiwe ili kuwakinga,” amesema Waziri Mhagama.

Aidha, Waziri Mhagama ameeleza kuwa takwimu za hivi karibuni zinaonesha kwa miaka mitano (5) mfululizo kiwango cha uchanjaji kitaifa ni zaidi ya asilimia 90 na hivyo kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri katika utoaji wa huduma za chanjo. 

“Kiwango hiki cha uchanjaji hapa nchini, pamoja na afua nyingine, imewezesha nchi kufikia malengo ya Milenia (SDG 4) kwa kupunguza vifo vya watoto chini ya umri miaka mitano,” amesema Waziri Mhagama.

Waziri Mhagama amewahakikishia Watanzania kuwa Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kushirikiana na Shirika  la utoaji wa  Chanjo Duniani (GAVI) ina mikakati mingi ya kuhakikisha huduma za afya hususani chanjo zinaendelea kuboreshwa ambapo imeweza kuimarisha mnyororo baridi wa utunzaji wa chanjo katika vituo vya kutolea huduma za afya hapa nchini. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa huduma za uuguzi na Ukunga Wizara ya Afya Bi. Ziada Sellah akimuwakilisha Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe amesema dhima ya maadhimisho hayo ni kuwaleta wadau pamoja na wataalam ili kujadili namna bora ya  kuendelea kutoa huduma bora za chanjo katika mkoa wa Tabora na nchi nzima kwa ujumla. 

“Madhumuni mengine ya maadhimisho haya ni kuhamasisha na kuelimisha jamii umuhimu wa huduma za chanjo katika kukinga magonjwa ambayo yanaweza kuzuilika kwa chanjo ikiwemo, Surua Rubella, Nimonia pamoja na chanjo ya kuzuia kuhara,” amesema Bi. Ziada

Mwakilishi Mkazi Shirika la Afya Duniani Tanzania (WHO) Dkt. Charles Sagoe-Moses amesema uchaguzi wa mkoa wa Tabora kuwa mkoa wa uzinduzi wa kitaifa kwa mwaka huu ni wa kupongezwa kutokana na baadhi ya watoto walio wengi ambao ni walengwa wa chanjo kutofikiwa.

“WHO imeendelea kuunga mkono katika kushughulikia pengo hilo kwa kutoa msaada wa  chanjo ambayo ililenga wilaya tatu (3) za Kaliua, Sikonge na Uyui, zilizotajwa kuwa na idadi kubwa ya dozi sifuri, kampeni ililenga kufikia vijiji vyote na  ilikuwa na mafanikio makubwa ” amesema Dkt. Charles.

✚

Ushauri,Elimu,Tiba

Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)

🏆Certified| Doctor from Afyaclass. Maudhui haya ni kwa ajili ya elimu ya jumla ya afya. Unapohitaji ushauri wa kina, uchunguzi, au matibabu binafsi, wasiliana na daktari kupitia namba:+255758286584.Pia tufwatilie kupitia: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Guest Avatar

LATEST POSTS

Utafiti8 hours ago

Wanaume Wahimizwa Kupima Saratani ya Tezi Dume Kuanzia Miaka 50

Wanaume Wahimizwa Kupima Saratani ya Tezi Dume Kuanzia Miaka 50 Chanzo: CNN Health Mwandishi: Jacqueline Howard Tarehe: Novemba 12, 2026...

magonjwa ya watoto11 hours ago

Changamoto ya Ngozi Kwa Watoto,fahamu hapa

Changamoto ya Ngozi Kwa Watoto: Sababu, Dalili, Magonjwa Yanayoonekana Mara kwa Mara na Njia za Kuzuia Ngozi ni kiungo kikubwa...

Utafiti15 hours ago

Asilimia 63 ya Wauzaji wa Matunda Wanatumia Kemikali Kuchelewesha au Kuharakisha Kuiva kwa Ndizi na Nyanya

Wataalamu waonya kuhusu matumizi yasiyo sahihi ya kemikali katika kuiva kwa matunda, wakisema baadhi ya kemikali zinaweza kuwa na madhara...

WHO1 day ago

WHO yatoa Miongozo ya Kwanza ya Utambuzi na Udhibiti wa Kisukari cha Aina ya Kwanza kwa Watu Wazima

Shirika la Afya Duniani (World Health Organization – WHO) limetoa kwa mara ya kwanza miongozo ya kimataifa kuhusu utambuzi na...

magonjwa ya wanaume2 years ago

Madhara ya punyeto,Soma Hapa Kufahamu ukweli wa Mambo

Madhara ya punyeto,Soma Hapa Kufahamu ukweli wa Mambo Tabia hii imekuwa ikiwaathiri Wanaume Wengi kwa hivi Sasa,Je unazifahamu athari au...

magonjwa1 day ago

HPV ni Ugonjwa gani?,Fahamu hapa

Human Papilloma Virus (HPV): Maana Yake, Magonjwa Inayosababisha Na Athari Zake Kwa Afya Human Papilloma Virus (HPV) ni nini? Human...

Hospital1 day ago

Waziri wa Afya,amewapongeza watumishi wanne kwa kuokoa maisha ya mama na mtoto

Waziri wa Afya,amewapongeza watumishi wanne kwa kuokoa maisha ya mama na mtoto Waziri wa Afya, Mohamed Omary Mchengerwa, amewapongeza watumishi...

Ebola2 days ago

Ugonjwa wa Ebola ulivyoleta Athari kwa watoto DRC

Ugonjwa wa Ebola ulivyoleta Athari kwa watoto DRC Kufikia tarehe 4 Novemba, watoto 2,959 wenye umri chini ya miaka 18...

magonjwa ya wanawake3 days ago

Madhara ya kuvurugika kwa homoni za kike (Hormonal Imbalance in women)

Kuvurugika kwa hormone au vichocheo ni nini? Kuvurugika kwa hormone au vichocheo hutokea pale mwili unapozalisha homoni kwa kiwango kikubwa...

Hospital4 days ago

Muhimbili kufanya upasuaji wa kurejesha nguvu za kiume (Penile Implant Surgery)

Muhimbili kufanya upasuaji wa kurejesha nguvu za kiume (Penile Implant Surgery) Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imeendelea kuboresha huduma za kibingwa...