Connect with us

DAWA

Dawa ya kudhibiti pombe sasa ni rasmi kutumika

Avatar

Published

on

Dawa ya kudhibiti pombe sasa ni rasmi kutumika

Bohari ya Dawa (MSD) imefanikiwa kuingiza shehena ya kwanza ya dawa ya tiba ya uraibu wa pombe iitwayo Naltrexone. Hatua hii ni matokeo ya ushirikiano wa kimkakati kati ya MSD na Taasisi ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe katika kuimarisha matibabu ya uraibu wa pombe nchini.

Hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa makubaliano ya uimarishaji huduma kati ya MSD na Taasisi ya Taifa ya Afya ya Akili-Mirembe kuimarisha upatikanaji wa bidhaa za udhibiti wa uraibu wa pombe.

Dawa ya Naltrexone itaratibiwa upatikanaji wake na Taasisi ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe huku ikiwa ni bidhaa itakayo endelea kununuliwa na MSD kwa ajili ya taasisi hiyo.

Mapema mwezi huu, wakati wa mafunzo kuhusu matumizi ya dawa ya Naltrexone, yaliyoandaliwa na Taasisi ya Taifa ya Afya ya Akili, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe aliwaagiza MSD kuharakisha upatikanaji wa vidonge hivyo.

MSD imepokea na kuingiza shehena hii nchini ikiwa ni hatua muhimu katika kuimarisha huduma za afya ya akili na tiba ya uraibu pombe. Mafanikio haya yanaonesha juhudi za Serikali kupitia MSD na wadau wa sekta ya afya kuhakikisha bidhaa muhimu za afya na za kimkakati zinapatikana nchini kwa wakati. Via @tbc_online

✚

Ushauri,Elimu,Tiba

Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)

Karibu Afyaclass Jukwaa linaloongoza kwa utoaji wa elimu sahihi ya Afya. Hapa utapata Elimu na Updates mbali mbali za Afya Duniani. Pia Pata dondoo za afya kila siku kwa kufuatilia kupitia Mitandao hii hapa: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Guest Avatar

LATEST POSTS

Utafiti9 hours ago

Wanaume Wahimizwa Kupima Saratani ya Tezi Dume Kuanzia Miaka 50

Wanaume Wahimizwa Kupima Saratani ya Tezi Dume Kuanzia Miaka 50 Chanzo: CNN Health Mwandishi: Jacqueline Howard Tarehe: Novemba 12, 2026...

magonjwa ya watoto11 hours ago

Changamoto ya Ngozi Kwa Watoto,fahamu hapa

Changamoto ya Ngozi Kwa Watoto: Sababu, Dalili, Magonjwa Yanayoonekana Mara kwa Mara na Njia za Kuzuia Ngozi ni kiungo kikubwa...

Utafiti16 hours ago

Asilimia 63 ya Wauzaji wa Matunda Wanatumia Kemikali Kuchelewesha au Kuharakisha Kuiva kwa Ndizi na Nyanya

Wataalamu waonya kuhusu matumizi yasiyo sahihi ya kemikali katika kuiva kwa matunda, wakisema baadhi ya kemikali zinaweza kuwa na madhara...

WHO1 day ago

WHO yatoa Miongozo ya Kwanza ya Utambuzi na Udhibiti wa Kisukari cha Aina ya Kwanza kwa Watu Wazima

Shirika la Afya Duniani (World Health Organization – WHO) limetoa kwa mara ya kwanza miongozo ya kimataifa kuhusu utambuzi na...

magonjwa ya wanaume2 years ago

Madhara ya punyeto,Soma Hapa Kufahamu ukweli wa Mambo

Madhara ya punyeto,Soma Hapa Kufahamu ukweli wa Mambo Tabia hii imekuwa ikiwaathiri Wanaume Wengi kwa hivi Sasa,Je unazifahamu athari au...

magonjwa1 day ago

HPV ni Ugonjwa gani?,Fahamu hapa

Human Papilloma Virus (HPV): Maana Yake, Magonjwa Inayosababisha Na Athari Zake Kwa Afya Human Papilloma Virus (HPV) ni nini? Human...

Hospital1 day ago

Waziri wa Afya,amewapongeza watumishi wanne kwa kuokoa maisha ya mama na mtoto

Waziri wa Afya,amewapongeza watumishi wanne kwa kuokoa maisha ya mama na mtoto Waziri wa Afya, Mohamed Omary Mchengerwa, amewapongeza watumishi...

Ebola2 days ago

Ugonjwa wa Ebola ulivyoleta Athari kwa watoto DRC

Ugonjwa wa Ebola ulivyoleta Athari kwa watoto DRC Kufikia tarehe 4 Novemba, watoto 2,959 wenye umri chini ya miaka 18...

magonjwa ya wanawake3 days ago

Madhara ya kuvurugika kwa homoni za kike (Hormonal Imbalance in women)

Kuvurugika kwa hormone au vichocheo ni nini? Kuvurugika kwa hormone au vichocheo hutokea pale mwili unapozalisha homoni kwa kiwango kikubwa...

Hospital4 days ago

Muhimbili kufanya upasuaji wa kurejesha nguvu za kiume (Penile Implant Surgery)

Muhimbili kufanya upasuaji wa kurejesha nguvu za kiume (Penile Implant Surgery) Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imeendelea kuboresha huduma za kibingwa...