Connect with us

EVENTS

Siku ya hali ya hewa duniani, tarehe 23 Machi

Doctor Ombeni

Published

on

Siku ya hali ya hewa duniani, tarehe 23 Machi

Jana tarehe 23 Machi ilikuwa siku ya hali ya hewa duniani, Tafiti mbali mbali Zinaonyesha kila mwaka kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita kumerikodiwa hali ya joto kali zaidi katika historia ya Dunia,

Pia kuna mifano ya namna mataifa mbali mbali yalivyoathirika kwa majanga kama vile moto wa msituni, mafuriko, vimbunga vikali na dhoruba zisizotarajiwa.

“Katika zama hizi za maafa yasababishwayo na tabianchi, kila mtu duniani anapaswa kulindwa na mfumo wa tahadhari ya mapema kama haki ya msingi. Pamoja, lazima tuchukue hatua sasa.”

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameeleza “bado karibu nusu ya nchi duniani hazina mifumo ya kutabiri majanga na kuwaonya wananchi mapema. Ni jambo la aibu kwamba katika enzi hii ya kidijitali, watu bado wanapoteza maisha na riziki kwa sababu hawana mifumo madhubuti ya tahadhari ya mapema.”

Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Tahadhari za Mapema kwa Wote unalenga kuhakikisha kuwa kila mtu, kila mahali, analindwa na mfumo wa onyo ifikapo mwaka 2027. Na ili kuhakikisha hili linafikiwa Guterres amependekeza mambo kadhaa yafanyike.

Tunahitaji msaada wa kisiasa wa kiwango cha juu kwa mpango huu ndani ya nchi, msaada wa kiteknolojia, ushirikiano mkubwa kati ya serikali, wafanyabiashara, na jamii, pamoja na juhudi kubwa za kuongeza fedha.

Kuimarisha uwezo wa kukopesha wa Benki za Maendeleo ya Kimataifa ni hatua muhimu. Mkataba wa Baadaye (Pact for the Future) uliokubaliwa mwaka 2024 ulifanya maendeleo makubwa, lakini lazima utekelezwe kikamilifu. Vivyo hivyo, matokeo ya fedha ya COP29 lazima yahakikishwe.

Na mwisho ameeleza juhudi za kukabiliana na mgogoro wa tabianchi lazima ziongezwe kwa haraka. Inahitajika kupunguza kwa kina na haraka utoaji wa gesi chafuzi ili kuzuia hali kuwa mbaya zaidi. Mwaka huu, nchi zote zinapaswa kutimiza ahadi zao za kuwasilisha mipango mipya ya kitaifa ya kukabiliana na tabianchi, mipango ambayo inazingatia lengo la kuzuia ongezeko la joto la dunia lisizidi nyuzi joto 1.5°C.

WEWE UNAFIKIRI NINI KIFANYIKE ILI KUKABILIANA NA MABADILIKO HAYA MAKUBWA YA HALI YA HEWA?

✚

Ushauri,Elimu,Tiba

Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)

🏆Certified| Doctor from Afyaclass. Maudhui haya ni kwa ajili ya elimu ya jumla ya afya. Unapohitaji ushauri wa kina, uchunguzi, au matibabu binafsi, wasiliana na daktari kupitia namba:+255758286584.Pia tufwatilie kupitia: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Guest Avatar

LATEST POSTS

Utafiti8 hours ago

Wanaume Wahimizwa Kupima Saratani ya Tezi Dume Kuanzia Miaka 50

Wanaume Wahimizwa Kupima Saratani ya Tezi Dume Kuanzia Miaka 50 Chanzo: CNN Health Mwandishi: Jacqueline Howard Tarehe: Novemba 12, 2026...

magonjwa ya watoto11 hours ago

Changamoto ya Ngozi Kwa Watoto,fahamu hapa

Changamoto ya Ngozi Kwa Watoto: Sababu, Dalili, Magonjwa Yanayoonekana Mara kwa Mara na Njia za Kuzuia Ngozi ni kiungo kikubwa...

Utafiti15 hours ago

Asilimia 63 ya Wauzaji wa Matunda Wanatumia Kemikali Kuchelewesha au Kuharakisha Kuiva kwa Ndizi na Nyanya

Wataalamu waonya kuhusu matumizi yasiyo sahihi ya kemikali katika kuiva kwa matunda, wakisema baadhi ya kemikali zinaweza kuwa na madhara...

WHO1 day ago

WHO yatoa Miongozo ya Kwanza ya Utambuzi na Udhibiti wa Kisukari cha Aina ya Kwanza kwa Watu Wazima

Shirika la Afya Duniani (World Health Organization – WHO) limetoa kwa mara ya kwanza miongozo ya kimataifa kuhusu utambuzi na...

magonjwa ya wanaume2 years ago

Madhara ya punyeto,Soma Hapa Kufahamu ukweli wa Mambo

Madhara ya punyeto,Soma Hapa Kufahamu ukweli wa Mambo Tabia hii imekuwa ikiwaathiri Wanaume Wengi kwa hivi Sasa,Je unazifahamu athari au...

magonjwa1 day ago

HPV ni Ugonjwa gani?,Fahamu hapa

Human Papilloma Virus (HPV): Maana Yake, Magonjwa Inayosababisha Na Athari Zake Kwa Afya Human Papilloma Virus (HPV) ni nini? Human...

Hospital1 day ago

Waziri wa Afya,amewapongeza watumishi wanne kwa kuokoa maisha ya mama na mtoto

Waziri wa Afya,amewapongeza watumishi wanne kwa kuokoa maisha ya mama na mtoto Waziri wa Afya, Mohamed Omary Mchengerwa, amewapongeza watumishi...

Ebola2 days ago

Ugonjwa wa Ebola ulivyoleta Athari kwa watoto DRC

Ugonjwa wa Ebola ulivyoleta Athari kwa watoto DRC Kufikia tarehe 4 Novemba, watoto 2,959 wenye umri chini ya miaka 18...

magonjwa ya wanawake3 days ago

Madhara ya kuvurugika kwa homoni za kike (Hormonal Imbalance in women)

Kuvurugika kwa hormone au vichocheo ni nini? Kuvurugika kwa hormone au vichocheo hutokea pale mwili unapozalisha homoni kwa kiwango kikubwa...

Hospital4 days ago

Muhimbili kufanya upasuaji wa kurejesha nguvu za kiume (Penile Implant Surgery)

Muhimbili kufanya upasuaji wa kurejesha nguvu za kiume (Penile Implant Surgery) Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imeendelea kuboresha huduma za kibingwa...