Connect with us
Author 1 Author 2 Author 3 Author 4
Authors

EVENTS

Waliofichua namna ubongo unavyofanya kazi watunukiwa tuzo ya Nobel

Avatar

Published

on

Picha:BBC-Waliofichua namna ubongo unavyofanya kazi watunukiwa tuzo ya Nobel
337 Views
0 Comments

Daktari bingwa wa magonjwa ya akili na mfumo wa neva kutoka Marekani, Karl Deisseroth, pamoja na wanasayansi kutoka Ujerumani, Peter Hegemann na Georg Nagel, wametunukiwa Tuzo ya Nobel ya Fiziolojia au Tiba; ya mwaka 2026 kwa kazi yao katika taaluma ya optogenetiki.

Utafiti wao umewasaidia wanasayansi kuelewa kwa undani zaidi namna ubongo unavyofanya kazi, hatua inayochangia kuelewa kwa kina jinsi akili ya binadamu inavyofanya kazi.

Kamati ya Nobel imewasifu wanasayansi hao watatu kwa kuweka msingi wa enzi mpya katika sayansi ya mfumo wa neva, baada ya kufichua namna ya kuwasha na kuzima mizunguko ya neva inayohusika na kumbukumbu, hisia na tabia mahususi zinazohusiana na matatizo ya mfumo wa neva na magonjwa ya akili.

Katika tiba, watafiti wanatumia njia hiyo katika majaribio ya kurejesha uwezo wa kuona kwa watu wenye matatizo ya kuona.

“Ni jambo la ajabu kabisa. Optogenetiki imebadilisha kwa kiasi kikubwa uelewa wetu kuhusu ubongo,” limesema Baraza la Nobel.

“Kila siku huleta ugunduzi mpya, unaosaidia kutatua mojawapo ya mafumbo makubwa ya mwanadamu: jinsi ubongo wetu wa ajabu unavyofanya kazi.”

Washindi hao wamefurahi kupokea tuzo hiyo, wakieleza kuwa ni heshima kubwa kushirikiana tuzo hiyo na marafiki zao.

Wanasayansi hao watatu pia watagawana zawadi ya fedha yenye thamani ya paundi 900,000 za Uingereza (takribani Sh. 3.14).

Mwenyekiti wa Kamati ya Nobel ya Fiziolojia au Tiba, Per Svenningsson, amesema: “Optogenetiki inatoa fursa ya kuchora na kuelewa ramani ya ubongo kwa namna ambayo hapo awali tulidhani ni ndoto tu.”

Amesema kazi ya wanasayansi hao imesaidia kuelewa namna hisia, tabia na shughuli mbalimbali za mwili zinavyodhibitiwa na ubongo.

“Kwa kutumia mwanga, watafiti sasa wanaweza kuwasha au kuzima mizunguko mahususi ya neva katika ubongo. Wanaweza kuamsha kumbukumbu, kusababisha hisia, kuchochea tabia na kuchunguza aina mbalimbali za neuroni zinazohusika katika matatizo tofauti ya mfumo wa neva na magonjwa ya akili.”

Kamati hiyo imeongeza kuwa mbinu hiyo inatoa uelewa muhimu kuhusu namna mfumo wa neva unavyoshirikiana na seli mbalimbali katika maeneo mengine ya mwili, kama vile moyo na utumbo.

Kamati hiyo imesema watafiti hao wameanza kutumia optogenetiki kama njia ya matibabu.

Imesema katika majaribio ya kitabibu yanayoendelea, wanasayansi wamekuwa wakifanya kazi ya kurejesha uoni kwa watu ambao wamepoteza uwezo huo kutokana na retinitis pigmentosa, ugonjwa unaoharibu seli za fimbo na koni zinazopatikana kwenye retina ya jicho.

Kwa kuingiza protini maalumu katika eneo lililoharibiwa la jicho, baadhi ya wagonjwa wameweza kurejesha kiwango fulani cha uwezo wa kuona wanapotumia miwani maalumu inayotoa mwanga.

Mwanga huo huwezesha protini za miwani zilizotumika katika matibabu kufanya kazi.

OPTOGENETIKI

Ni mbinu inayofanya iwezekane kuwasha au kuzima shughuli za seli mahususi za neva katika ubongo wa kiumbe hai.

Kwa sasa, mbinu hiyo inatumika katika maabara mbalimbali duniani ili kufichua mafumbo yanayohusu utendaji wa ubongo.

WASHINDI

Mwanzoni mwa miaka ya 2000, watafiti Hegemann na Nagel waligundua channelrhodopsin, protini yenye sifa za kipekee.

Walibaini kuwa bila kujali aina ya seli ambamo waliingiza protini hiyo, seli hizo zilianza kuwa na uwezo wa kuitikia mwanga.

Mtafiti mwingine, Deisseroth baadaye alibaini namna ya kutumia protini hiyo inayodhibitiwa na mwanga kuwasha seli za neva katika ubongo wa panya.

Deisseroth aliingiza jeni ya channelrhodopsin katika seli za neva zilizotokana na panya ambapo alipoangazia seli hizo kwa mwanga wa buluu, aliweza kuchochea ishara ya neva.

Baadaye, alifanikiwa kutumia “swichi” hiyo inayodhibitiwa na mwanga katika seli za neva za ubongo wa panya hai.

Mbinu hii ya kudhibiti ishara za neva kwa kutumia mwanga sasa inajulikana kama optogenetiki, na imepata matumizi makubwa katika utafiti wa kisayansi duniani.

Tangu wakati huo, watafiti wameweza kuchunguza seli na njia za neva katika wanyama, na hivyo kuona na kugundua kwa undani zaidi kazi zinazofanywa na seli hizo.

Chanzo: BBC/Nobel Prize

337 Views
0 Comments

How we reviewed this article:

✚

Ushauri,Elimu,Tiba

Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)

Karibu Afyaclass Jukwaa linaloongoza kwa utoaji wa elimu sahihi ya Afya. Hapa utapata Elimu na Updates mbali mbali za Afya Duniani. Pia Pata dondoo za afya kila siku kwa kufuatilia kupitia Mitandao hii hapa: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

Health Topics Letters

QX
A

Makala za Herufi A (30)

C

Makala za Herufi C (90)

D

Makala za Herufi D (154)

F

Makala za Herufi F (144)

H

Makala za Herufi H (27)

J

Makala za Herufi J (104)

K

Makala za Herufi K (149)

M

Makala za Herufi M (350)

N

Makala za Herufi N (35)

S

Makala za Herufi S (76)

T

Makala za Herufi T (216)

U

Makala za Herufi U (294)

V

Makala za Herufi V (48)

LATEST POSTS

Afya News4 hours ago

Tanzania, Algeria kuanza ushirikiano uzalishaji wa DAWA nchini

TANZANIA, ALGERIA KUANZA USHIRIKIANO UZALISHAJI WA DAWA NCHINI Na Andrea Kadege, WAF–Dar es Salaam Tanzania na Algeria kuanza ushirikiano katika...

EVENTS6 hours ago

Waliofichua namna ubongo unavyofanya kazi watunukiwa tuzo ya Nobel

Daktari bingwa wa magonjwa ya akili na mfumo wa neva kutoka Marekani, Karl Deisseroth, pamoja na wanasayansi kutoka Ujerumani, Peter...

afyatips10 hours ago

Vitu vya kufanya na kuzingatia kwa mtu mwenye uzito mkubwa na Presha kubwa

Vitu vya kufanya na kuzingatia kwa mtu mwenye uzito mkubwa na Presha kubwa Lakini wakati mwingine hupata dalili hii Uzito...

magonjwa ya wanaume14 hours ago

Kwanini mwanaume anamwaga mapema

Kwanini Mwanaume Anamwaga Mapema? (Premature Ejaculation) Kumwaga mapema au premature ejaculation (PE) ni hali ambapo mwanaume hufika kileleni na kutoa...

afyatips5 years ago

SABABU ZA MTU KUKONDA

KUKONDA • • • • • • SABABU ZA MTU KUKONDA sababu za mtu kukonda kuweza kuwa za moja kwa...

WHO2 days ago

WHO yatoa Taarifa Mpya kuhusu Kipindupindu, Homa ya Uti wa Mgongo na Tauni Duniani

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti mwenendo mpya wa magonjwa matatu ya bakteria yanayoweza kusababisha milipuko na vifo—kipindupindu (cholera), homa...

magonjwa2 days ago

Magonjwa 5 ya MOYO yanayoweza Kuua haraka

Magonjwa ya moyo na mishipa ni miongoni mwa sababu kubwa za vifo duniani. WHO inaeleza kuwa magonjwa ya moyo na...

FEATURES3 days ago

Rubani Asimulia Jinsi Alivyopambana Baada ya Kuchomwa Kisu na Rubani Mwenza Kwenye Ndege ya Flydubai

Rubani wa ndege ya Flydubai, Captain Smit Machchhar, amesimulia tukio la kutisha lililotokea ndani ya chumba cha marubani baada ya...

Hospital3 days ago

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila hulaza wagonjwa kati ya watano na saba wenye kiharusi kila siku

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila hulaza wagonjwa kati ya watano na saba wenye kiharusi kila siku, hali inayodhihirisha ukubwa wa tatizo...

Utafiti3 days ago

Maambukizi Yanayozuilika Yasababisha Moja Kati ya Kesi Nane za Saratani Duniani

Utafiti mpya wa Shirika la Kimataifa la Utafiti wa Saratani (IARC), ambalo ni sehemu ya Shirika la Afya Duniani (WHO),...

338
0