KUCHA
• • • • •
CHANZO CHA KUCHA KUWA NGUMU KAMA BATI
Tatizo hili huhusisha kucha kuwa nene na ngumu kupita kawaida, je chanzo chake ni nini?
CHANZO CHA KUCHA KUWA NGUMU KAMA BATI
- Moja ya sababu ya tatizo hili la kucha kuwa ngumu kupita kawaida ni pamoja na;
✓ Maambukizi ya Fangasi ambayo hujulikana kwa kitaalam kama ONYCHOMYCOSIS,
Maambukizi ya YEAST n.k
✓ Kuumia kwenye kucha mara kwa mara, tatizo ambalo huwapata sana watu wa michezo kama vile; Wachezaji wa mpira wa Miguu n.k
✓ Yellow nail syndrome, tatizo ambalo husababisha kucha kubadilika rangi na kuwa manjano na hatimaye kucha kuanza kujikunja na kuwa nene
✓ Matatizo kwenye mfumo wa kinga ya mwili yaani Autoimmune disorder kama vile PSORIASIS,
huweza kusababisha kucha kuwa na mikunjo pamoja na kuwa ngumu
✓ Tatizo la kwenye ngozi kama vile Paronychia ambalo husababisha wekundu kuzunguka kucha pamoja na Kuvimba
✓ Pia tatizo hili la kucha kuwa Ngumu huwapata sana watu ambao wana Umri mkubwa
MATIBABU YA TATIZO LA KUCHA KUWA NGUMU
- tiba ya tatizo hili hutegemea na chanzo chake,Mfano kama chanzo ni maambukizi ya fangasi,basi mgonjwa hupewa dawa za fangasi N.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
afya
afyaclass
afyatips
magonjwa
magonjwa ya wanaume
magonjwa ya wanawake
magonjwa ya watoto
makala
muhimu
new
post
uzazi
videos
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!