Connect with us

magonjwa

TATIZO LA VARICOSE VEINS ( KUVIMBA KWA MISHIPA YA DAMU) WAKATI WA UJA UZITO

Doctor Ombeni

Published

on

AFYA YA UZAZI

• • • • •

TATIZO LA VARICOSE VEINS ( KUVIMBA KWA MISHIPA YA DAMU) WAKATI WA UJA UZITO


Varicose Veins ni tatizo linalowapata baadhi ya wanawake wajawazito. Hili ni tatizo la kuvimba na kujikunja kwa baadhi mishipa ya damu hasa hasa kwenye maeneo ya miguu na mapaja. Pia linaweza kutokea kwenye maeneo ya njia ya haja kubwa na maeneo mengine.


CHANZO CHA TATIZO HILI LA VARICOSE VEINS


Mishipa ya Varicose kawaida husababishwa na kuwa na kuta dhaifu za mishipa na valves.  Ndani ya mishipa yako kuna vali ndogo za njia moja ambazo hufunguliwa ili kuruhusu damu kupita, na kisha kufunga ili kuizuia isirudi nyuma.  Wakati mwingine kuta za mishipa hukaza na kupoteza unyoofu, na kusababisha valves kudhoofika.



Hali hii hupelekea damu kusimama na kujikusanya sehemu moja ya mishipa na ndipo tatizo la kuvimba kwa mishipa huonekana.


MAMBO MUHIMU YA KUFANYA


– Ni vizuri kuongea na wamama na wadada katika ukoo au familia ili kujua kama hili tatizo liko katika familia yenu au la!


– Mama mjamzito inabidi ajitahidi kutokusimama kwa muda mrefu sana, Fanya mazoezi,tembea tembea na wala usisimame eneo moja kwa muda mrefu sana


 – Kuongezeka kwa msukumo wa damu au presha wakati wa ujauzito kunaweka stress kwenye mishipa ya damu,kitu ambacho huweza kuongeza uwezekano wa kutokea kwa tatizo hili


– kuongezeka kwa hormone aina ya Progesterone inalegeza misuli ambayo inaweza kusababisha kulegea kwa kuta,valves pamoja na kuvunjika kwa mishipa. 


Hata kama hukupata hili tatizo wakati wa ujauzito upo uwezekano wa kupata hemorrhoids au varicose veins baada ya kujifungua.


– Badala ya kukaa kwenye kiti kwa muda mrefu, jaribu kukaa chini kwenye style ya kihindi yaani tailor sitting.(kama nilivyoelekeza kwenye mada ya mazoezi) Pia jaribu kuweka miguu kuelekea juu/elevated.


– Fanya zoezi aina la Pelvic rocking. Lala chini huku miguu ikiegemezwa juu ya kochi, kiti au kitanda huku magoti yamekunjwa. Relax katika position hii kwa dakika 10 hadi 15 halafu simama kisha piga piga miguu kwa mikono taratibu.


– Fanya mazoezi ya yoga ambayo yanafanya miguu ikae kwa juu, lakini hakikisha una mtaalamu wa kukufundisha jinsi ya kufanya haya mazoezi vizuri.


– Kuogelea na kutembea pia ni mazoezi mazuri yanayosaidia kukupa mzunguko mzuri wa damu. Unaweza pia kupata massage ya miguu kwa dakika tano kila siku. 


– Usivae nguo za kubana, viatu virefu, jizuie kukunja miguu ukikaa, na kukaa kwenye kiti au gari kwa muda mrefu hivi vitu huzuia mzunguko mzuri wa damu


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.


✚

Ushauri,Elimu,Tiba

Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)

🏆Certified| Doctor from Afyaclass. Maudhui haya ni kwa ajili ya elimu ya jumla ya afya. Unapohitaji ushauri wa kina, uchunguzi, au matibabu binafsi, wasiliana na daktari kupitia namba:+255758286584.Pia tufwatilie kupitia: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Guest Avatar

LATEST POSTS

magonjwa ya Zinaa2 weeks ago

Ugonjwa wa Genital herpes,chanzo,dalili na Tiba

HERPES SEHEMU ZA SIRI: DALILI, NAMNA INAVYOAMBUKIZWA, KINGA NA MATIBABU Herpes sehemu za siri (Genital herpes) ni maambukizi ya zinaa...

magonjwa1 day ago

Ugonjwa wa Hepatitis C,chanzo chake,Dalili na Tiba

Ugonjwa wa Hepatitis C,chanzo chake,Dalili na Tiba Hepatitis C ni nini? Hepatitis C ni ugonjwa unaosababisha kuvimba na kuharibika kwa...

Uzazi&Ujauzito2 years ago

Dalili za mimba changa kuanzia wiki mbili hadi miezi mitatu ya ujauzito

Dalili za mimba changa kuanzia wiki mbili hadi miezi mitatu ya ujauzito. Fahamu Dalili za mimba changa kuanzia wiki mbili...

Ebola1 day ago

Baada ya kuthibitishwa kwa wagonjwa tisa nchini Kenya

Baada ya kuthibitishwa kwa wagonjwa tisa nchini Kenya Takriban wafanyakazi 5,000 wa sekta ya afya wamepewa mafunzo ya jinsi ya...

Ebola1 day ago

Hakuna haja ya hofu: Serikali ya Nigeria yasema baada ya mwanamke kupatikana na Ebola katika eneo la FCT

Hakuna haja ya hofu: Serikali ya Nigeria yasema baada ya mwanamke kupatikana na Ebola katika eneo la FCT Oktoba 20,...

Ebola1 day ago

Nigeria imethibitisha kisa cha Ebola katika mji mkuu Abuja

Nigeria imethibitisha kisa cha Ebola katika mji mkuu Abuja, baada ya mwanamke aliyewasili kutoka Uganda kukutwa na virusi vya ugonjwa...

Ukimwi2 days ago

Maambukizi ya virusi vya ukimwi

Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (Vvu): Njia Za Maambukizi Na Namna Ya Kujikinga Virusi vya UKIMWI (VVU) ni nini? Virusi...

magonjwa2 days ago

Maambukizi ya bakteria wa shigella: dalili, njia za maambukizi, Matibabu Na Kinga

Shigella ni aina ya bakteria wanaosababisha ugonjwa unaojulikana kama shigellosis, ambao huathiri mfumo wa mmeng’enyo wa chakula, hasa utumbo mpana....

magonjwa ya wanaume4 days ago

Mwanaume kushindwa kutungisha mimba

Tumezoea kwenye jamii Zetu Mara nyingi linapokuja Swala la kutokupata Mtoto,Lawama zote ni kwa Mwanamke,Lakini fahamu hata mwanaume anaweza kuwa...

Stars Health3 days ago

Papa aanza kurejea taratibu katika majukumu yake baada ya upasuaji wa Saratani ya Mapafu

Vatican, Oktoba 18, 2026 — Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa, Papa Leo, kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani mwenye umri wa...