Connect with us
Author 1 Author 2 Author 3 Author 4
Authors

afyatips

FAHAMU KUHUSIANA NA TATIZO LA KUTOKWA NA DAMU SEHEMU ZA SIRI (UKENI).

Doctor Ombeni

Published

on

109 Views
0 Comments

DAMU

• • • • • •

FAHAMU KUHUSIANA NA TATIZO LA KUTOKWA NA DAMU SEHEMU ZA SIRI (UKENI). 


katika hali ya kawaida mzunguko wa hedhi  kwa wanawake wengi ni kati ya siku 21-35 na damu hii hudumu kwa siku 4-5 katika hali ya kawaida na wingi wake ni wastani wa mililita 35 (20-80mls). Kutokwa na damu ukweni si ugonjwa bali ni dalili ya tatizo jingine  katika mwili. 


Yako matatizo mengi yanayolikumba swala zima la hedhi. Tatizo hili huwapata wanawake wa umri wowote kuanzia watoto mpaka wazee waliofika ukomo wa hedhi.  Baadhi ya wanawake huwa na mzunguko wa kawaida lakin mara zote mzunguko huo umekuwa wakitokwa na damu nyingi sana na hutokwa na damu zaid ya siku 7 mfululizo.  Idadi kadhaa ya wanawake hutokwa na damu katikati ya mzunguko wa hedhi,  na baadhi hutokwa na damu takriban mzunguko mzima.  Kuna wanawake ambao mzunguko wao huzidi siku 35 na kuna wale ambao ni chini ya siku 21.  Pia kuna asilimia ya wanawake hutokwa na damu mara baada ya kushiriki tendo la ndoa. 


Kalenda ni moja ya njia zitumikazo kuchunguza/kugundua mabadiliko ktk mzunguko wa hedhi. 


SABABU


sababu za kutokwa na damu ukeni kwa  wingi au kwa muda mrefu zimegawanywa ktk makundi makuu sita. 

1. Mabadiliko ya kimaumbile

2. Matatizo ya homoni

3. Maambukizi

4. Magonjwa katika sehemu mbalimbali za mwili

5. Madawa

6. Athari/ madhara/ changamoto za mimba. 

Kutoka kwenye makundi hayo juu tunapata sababu kama


1. Uvimbe katika via vya uzazi

2. Kujipandikiza kwa tishu za ukuta wa ndani wa mji wa mimba ktk misuli ya mji huo

3. Saratani katika mji wa mimba

4. Matatizo katika mfumo wa ugandaji wa damu. 

5. Mabadiliko ktk mzunguko wa hedhi yasababishwayo na homoni

6. Mimba (kuharibika,  kujipandikiza nje ya mji wa mimba nk) 

7.  Baadhi ya vifaa vitumikavyo katika panga uzazi huweza kuwa chanzo

8. Kushindwa kwa figo na ini kufanya kazi yake lakini pia matatizo katika tezi mbalimbali ikiwemo pituitari na thyroidi. 


JE UTAJUAJE KAMA UNATOKA DAMU NYINGI


Dalili za tatizo hili ni kama

1. Kutokwa na damu ya hedhi nyingi na/au kwa muda unaozidi siku saba. 

2. Kutokwa na mabonge mabonge ya damu ukeni

3. Kuongezeka kwa idadi ya pedi au vipande vya kanga wakati wa hedhi

4. Kuwa na dalili za upungufu wa damu mwilini


by Lwamayanga



109 Views
0 Comments

How we reviewed this article:

✚

Ushauri,Elimu,Tiba

Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)

🏆Certified| Doctor from Afyaclass. Maudhui haya ni kwa ajili ya elimu ya jumla ya afya. Unapohitaji ushauri wa kina, uchunguzi, au matibabu binafsi, wasiliana na daktari kupitia namba:+255758286584.Pia tufwatilie kupitia: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Guest Avatar

Health Topics Letters

QX
A

Makala za Herufi A (30)

C

Makala za Herufi C (90)

D

Makala za Herufi D (154)

F

Makala za Herufi F (144)

H

Makala za Herufi H (27)

J

Makala za Herufi J (104)

K

Makala za Herufi K (149)

M

Makala za Herufi M (350)

N

Makala za Herufi N (35)

S

Makala za Herufi S (76)

T

Makala za Herufi T (216)

U

Makala za Herufi U (294)

V

Makala za Herufi V (48)

LATEST POSTS

Afya News5 hours ago

Tanzania, Algeria kuanza ushirikiano uzalishaji wa DAWA nchini

TANZANIA, ALGERIA KUANZA USHIRIKIANO UZALISHAJI WA DAWA NCHINI Na Andrea Kadege, WAF–Dar es Salaam Tanzania na Algeria kuanza ushirikiano katika...

EVENTS7 hours ago

Waliofichua namna ubongo unavyofanya kazi watunukiwa tuzo ya Nobel

Daktari bingwa wa magonjwa ya akili na mfumo wa neva kutoka Marekani, Karl Deisseroth, pamoja na wanasayansi kutoka Ujerumani, Peter...

afyatips11 hours ago

Vitu vya kufanya na kuzingatia kwa mtu mwenye uzito mkubwa na Presha kubwa

Vitu vya kufanya na kuzingatia kwa mtu mwenye uzito mkubwa na Presha kubwa Lakini wakati mwingine hupata dalili hii Uzito...

magonjwa ya wanaume15 hours ago

Kwanini mwanaume anamwaga mapema

Kwanini Mwanaume Anamwaga Mapema? (Premature Ejaculation) Kumwaga mapema au premature ejaculation (PE) ni hali ambapo mwanaume hufika kileleni na kutoa...

afyatips5 years ago

SABABU ZA MTU KUKONDA

KUKONDA • • • • • • SABABU ZA MTU KUKONDA sababu za mtu kukonda kuweza kuwa za moja kwa...

WHO2 days ago

WHO yatoa Taarifa Mpya kuhusu Kipindupindu, Homa ya Uti wa Mgongo na Tauni Duniani

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti mwenendo mpya wa magonjwa matatu ya bakteria yanayoweza kusababisha milipuko na vifo—kipindupindu (cholera), homa...

magonjwa2 days ago

Magonjwa 5 ya MOYO yanayoweza Kuua haraka

Magonjwa ya moyo na mishipa ni miongoni mwa sababu kubwa za vifo duniani. WHO inaeleza kuwa magonjwa ya moyo na...

FEATURES3 days ago

Rubani Asimulia Jinsi Alivyopambana Baada ya Kuchomwa Kisu na Rubani Mwenza Kwenye Ndege ya Flydubai

Rubani wa ndege ya Flydubai, Captain Smit Machchhar, amesimulia tukio la kutisha lililotokea ndani ya chumba cha marubani baada ya...

Hospital3 days ago

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila hulaza wagonjwa kati ya watano na saba wenye kiharusi kila siku

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila hulaza wagonjwa kati ya watano na saba wenye kiharusi kila siku, hali inayodhihirisha ukubwa wa tatizo...

Utafiti3 days ago

Maambukizi Yanayozuilika Yasababisha Moja Kati ya Kesi Nane za Saratani Duniani

Utafiti mpya wa Shirika la Kimataifa la Utafiti wa Saratani (IARC), ambalo ni sehemu ya Shirika la Afya Duniani (WHO),...

110
0